Mvuto!!!

Mama Ashrat

Member
Apr 29, 2012
88
98
Attraction.

Mwenzi wako uliyenae anakuvutia kiasi gani?!Akikushika kwa hisia unatamani ukaribu wake au ni kama gari inayohitaji kusukumwa ndo iwake?!

Katika vitu ambavyo naamini vinaweza kusaidia sana kuimarisha mahusiano ni kuwa na mvuto wa kudumu kwa mwenzi wako.

Mahusiano mengi huwa yanakumbwa na dhoruba ya "kupeana adhabu" kwenye tendo la ndoa pale inapotokea mmoja amekasirika/zira kwa sababu azijuazo yeye au wakati mwingine zilizo wazi.Hili linatokana na watu kutokuwa na mvuto uliopitiliza kwa wenzi wao. Fikiria, kama mwenzio akivaa kagauni kakuvutua au kanga moja inayoonyesha mwili ukuvutiao akajishau mbele yako unashindwa kuzuia moyo na mwili wako kumtamani/kumtaka/kumhitaji wangapi ungewezaje kumnyima mkeo/mpenzi wako unyumba hata kama kakukasirisha na baadae akaamua kukuchokoza?! Kama bwan'kaka akikushika tu kidogo, akikunong'oneza sikioni ama akikupiga busu la kichokozi shingoni/sikioni anakupa hisia kali ungewezaje kumnyima mwenzio unyumba wiki nzima eti kisa sijui kakupunguzia pesa ya saluni ili mjenge?!

Inawezekana pengine wanaokuwa wamekasirikiwa hua hawajihangaishi kuwa'kamata' na kuwalainisha wenzi wao ila sio kosa lao pekee, yote ni kwasababu wanajua hisia zilizopo kati yao ni za kawaida sana hivyo bibie/bwana akinuna hamna linalowezekana.

Unadhani ni raha kiasi gani kumbusu na kumkumbatia mtu ambae una kahasira nae kidogo?! Hisia utakazokuwa nazo. . mapenzi na kahasira changanya pamoja, shughuli lazima iwe intensive.Kama ni kesi mtaendelea nayo baadae.

Usimpe mwenzio adhabu ya kutompa unyumba unless amekucheat(hapo unatakiwa uwe mwangalifu usije ambulia magonjwa), maana huo ndio mwanzo wa kumjazia mawazo ya kutafuta wakumpooza badala yako. Jenga hisia ambazo zitakuruhusu umpende hata pale anapokuwa amekukasirisha, badala ya zile za "I hate him/her". Mkubali, mpende, ruhusu mwili na moyo wake uvutiwe nae to the maximum.

Mama Ashrat
 
Mama Ashirat hii ni kali na ya maana. Hata akikucheat mwafaka sio kumnyima unyumba maana yanazungumzika hayo. Kucheat katika mapenzi kunatokana na namna gani unampa nafasi ya kwenda kucheat!! Nimelipenda somo lako
 
Kama amecheat muhimu kuwa mwangalifu, unaweza pewa yasiyofaa!!
 
LizzY karibu umetoka rumande dear, poleeeee sikunyingine usicheke mpka unainua miguu modes hawapendi
 
Mama Ashrat this is wonderful!hakika mtu akiweza kumaintain haya atadumu milele kwenye mahusiano yake..
Nb.inataka moyo kwa kweli sometimes unakuta mwenzio kakuudhi kwelikweli hata tabasamu la kulazimisha halitoki lol..
 
Last edited by a moderator:
what a kiss yaani hata kama kaniuzi akinibusu tu mama watoto basi mi hoi mbaya..
hii inanikumbusha mambo ya kiss zito toka kwa adii..
 
Mama
Ashrat
this is wonderful!hakika mtu akiweza kumaintain haya
atadumu milele kwenye mahusiano yake..
Nb.inataka moyo kwa kweli sometimes unakuta mwenzio kakuudhi kwelikweli
hata tabasamu la kulazimisha halitoki lol..

Na ukishamzoesha ata-take it for granted,anakukosea halafu wala hafanyi jitihada za kusuluhisha anakunja nne anasubiri busu la hasira! Lol
 
Last edited by a moderator:
Mama Ashrat this is wonderful!hakika mtu akiweza kumaintain haya atadumu milele kwenye mahusiano yake..
Nb.inataka moyo kwa kweli sometimes unakuta mwenzio kakuudhi kwelikweli hata tabasamu la kulazimisha halitoki lol..

Kweli kabisa Purple.
Kama kila mmoja akiwa ameamua kweli kuridhika na kutulia na mwenzie alafu mkafanikiwa kupeana that "i'm mad at you but I still love you anyway" kinda feeling mahusiano yenu yatakuwa na nafasi kubwa sana kusurvive.

Sema sasa ni mtihani kupata mtu utakaevutiwa nae, nae wewe to that extent.
 
Last edited by a moderator:
what a kiss yaani hata kama kaniuzi akinibusu tu mama watoto basi mi hoi mbaya..
hii inanikumbusha mambo ya kiss zito toka kwa adii..

ndetichia
Nakuonea raha kuwa mmoja wa waliobahatika. Wengi hawapati hiyo bahati, wakinuniana tu kidogo mzungu wa nne na kuhama chumbani kunahusu.
 
Last edited by a moderator:
Na ukishamzoesha ata-take it for granted,anakukosea halafu wala hafanyi jitihada za kusuluhisha anakunja nne anasubiri busu la hasira! Lol
@Ennie
Kama anakupenda kweli hawezi kukutumia kwa style hiyo. Pakuomba samahani ataomba, pakubembeleza atabembeleza and so so.
 
Hivi inawezekana pia mtu ambaye uko naye kufa na kuzikana akawa ametoka kabisa kwenye moyo wako? Ikiwa hivyo kiafrika unafanya nini? Maana Ma Ashrat umegusia mtu akikutoka moyoni, kufanya ile kitu inakuwa ni adhabu.
 
Ndahani
Mkiwa ni kufa na kuzikana kweli ndio inakua hivi sasa, yani hata katikati ya ugomvi mnaweza mkajikuta mnacheka, mnafurahi na kupendana. Ila mahusiano mengi hayana hiyo, kukiwa na ugomvi ndo chakula kususiana, maneno kutupiana,kitandani kukimbiana n.k

Sasa hapo sijui wanakua wametoana moyoni kwa muda au wanakumbushana tu kwamba hamna aliyeukamata moyo wa mwenzie sawasawa.
 
Na maisha yetu yalivyo leo, watu wengi wanaangukia group gani? Separations au kuachana kabisa imekuwa kama kawaida tu. Au ndio watu kutotaka kuishi kwenye uhusiano unaofanana na adhabu adhabu vile!
 
Na maisha yetu yalivyo leo, watu wengi wanaangukia group gani? Separations au kuachana kabisa imekuwa kama kawaida tu. Au ndio watu kutotaka kuishi kwenye uhusiano unaofanana na adhabu adhabu vile!
Kutumiana aisee.
Wengi wako kutumiana zaidi, hamna kuwekana moyoni, ni mwendo wa "una nnachokitaka kwahiyo ntakuwa na wewe." Kupendana kweli kunabaki kuwa hadithi tu na sio zaidi.

Ukishakuwa na mahusiano kama hayo kuachana ni rahisi sana maana kuna siku alichofuata kwako kinaweza kisiwepo au ukaona mwenye ku-offer zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom