Mama Ashrat
Member
- Apr 29, 2012
- 88
- 98
Attraction.
Mwenzi wako uliyenae anakuvutia kiasi gani?!Akikushika kwa hisia unatamani ukaribu wake au ni kama gari inayohitaji kusukumwa ndo iwake?!
Katika vitu ambavyo naamini vinaweza kusaidia sana kuimarisha mahusiano ni kuwa na mvuto wa kudumu kwa mwenzi wako.
Mahusiano mengi huwa yanakumbwa na dhoruba ya "kupeana adhabu" kwenye tendo la ndoa pale inapotokea mmoja amekasirika/zira kwa sababu azijuazo yeye au wakati mwingine zilizo wazi.Hili linatokana na watu kutokuwa na mvuto uliopitiliza kwa wenzi wao. Fikiria, kama mwenzio akivaa kagauni kakuvutua au kanga moja inayoonyesha mwili ukuvutiao akajishau mbele yako unashindwa kuzuia moyo na mwili wako kumtamani/kumtaka/kumhitaji wangapi ungewezaje kumnyima mkeo/mpenzi wako unyumba hata kama kakukasirisha na baadae akaamua kukuchokoza?! Kama bwan'kaka akikushika tu kidogo, akikunong'oneza sikioni ama akikupiga busu la kichokozi shingoni/sikioni anakupa hisia kali ungewezaje kumnyima mwenzio unyumba wiki nzima eti kisa sijui kakupunguzia pesa ya saluni ili mjenge?!
Inawezekana pengine wanaokuwa wamekasirikiwa hua hawajihangaishi kuwa'kamata' na kuwalainisha wenzi wao ila sio kosa lao pekee, yote ni kwasababu wanajua hisia zilizopo kati yao ni za kawaida sana hivyo bibie/bwana akinuna hamna linalowezekana.
Unadhani ni raha kiasi gani kumbusu na kumkumbatia mtu ambae una kahasira nae kidogo?! Hisia utakazokuwa nazo. . mapenzi na kahasira changanya pamoja, shughuli lazima iwe intensive.Kama ni kesi mtaendelea nayo baadae.
Usimpe mwenzio adhabu ya kutompa unyumba unless amekucheat(hapo unatakiwa uwe mwangalifu usije ambulia magonjwa), maana huo ndio mwanzo wa kumjazia mawazo ya kutafuta wakumpooza badala yako. Jenga hisia ambazo zitakuruhusu umpende hata pale anapokuwa amekukasirisha, badala ya zile za "I hate him/her". Mkubali, mpende, ruhusu mwili na moyo wake uvutiwe nae to the maximum.