Mvuto huchangiaje katika mapenzi


Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,611
Points
1,225
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,611 1,225
[h=5]Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Bristol umebaina kwamba mwanaume au mwanamke akiutwika huwaona wengine wanavutia sana.
Mwanaume huona wanawake wanavutia na ni warembo kwelikweli, na wanawake huona wanaume ni handsome wa nguvu.
... Pombe zikimtoka Guess what? ............................

Tume ya uchaguzi hapa Canada mwaka 1974 iligundua kwamba wagombea uchuguzi wenye sura zinazovutia walipata kura mara mbili na nusu ya wale ambao sura zao zilikuwa za kutisha hasa pale wanapolingana uwezo.
Hivi hii Tanzania haijawahi kutokea watu wakampigia kura mgombea kwa ushindi wa Tsunami? Maisha bora kwa kila mtanzania
Sura inayovutia acha kabisa!

Mwanamke anapotumia pills husababisha kupunguza uwezo wa kunusa, hii inatokana na utafiti uliofanywa a chuo kikuu cha Liverpool kwa wanawake kunusa (sniff) mashati 100 ya wanaume.
Kawaida mwanamke huvutiwa na mwanaume tofauti na genetics zake (harufu tofauti).
Wengine hata jasho la kwapa kwao wao ni faraja

Tafiti za kisayansi zinasema si binadamu wote huvutiwa na binadamu wengine, inasemakana kuna binadamu ambao huvutiwa na vitu wala si wanyama bali vitu visivyo na uhai.
Hawa watu huweza kusisimka, kupenda (fall in love) na pia huwa committed kuishi navyo au kuishi hapo vilipo.
Eija-Riita Berliner-Mauer yeye ameolewa na ukuta wa Berlin tangu mwaka 1979.
Duniani kuna vituko!

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Pennsylvania mwaka 1980 waligundua kwamba watuhumiwa waliokuwa wanavutia sura zao walipata adhabu laini zaidi ukilinganisha na watuhumiwa wenye sura zilizikuwa zinatisha.
Yaani kwa sura nzuri wanakuhurumia?

Wanawake wanapojipamba sana kwa vipodozi huweza kupunguza uwezo wa wanaume kuvutiwa nao hasa wakiwa wapo fertile.
Wanawake huwa na aina ya harufu (scent) ambayo huvutia wanaume hasa mwanamke anapokuwa kwenye siku za ovulation.
Kama hutaki kusumbuliwa na wanaume basi ukiwa fertile siliba vipodozi (makeup) vya nguvu finish!

Unavyojionesha kwa mara ya kwanza ni muhimu sana (first impressions).
Wengi huweza kutoa uamuzi wa mwenzake kuwa partner hasa kutokana na alivyojieleza dakika 4 za kwanza kuonana.
Siyo kujieleza maneno tu bali ni vitendo vya mwili unapoongea, maneno unayoongea na sauti unayoongea.
Maneno unayoongea kwa mara ya kwanza huvutia asilimia 7 tu, vitendo vya mwili unapoonga (body language) ni asilimia 55 na aina ya sauti na jinsi unavyoongea ni asilimia 38.

Je, unadhani mpenzi wako alikuvutia kitu gani siku ya kwanza ulipokutana naye?[/h]

AMEN..............!
 
prianka

prianka

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2012
Messages
684
Points
195
Age
27
prianka

prianka

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2012
684 195
mapenzi hajali mvuto wa mtu ila hujali upendo na hisia za mtu na katika kupenda kila mtu huwa anavutiwa na vitu tofauti kwa mfano mwingine anampenda mwanamke mwenye macho makubwa lkn upendo ndo ulio tangulia kwanza na akazama kihisia ndani yake
 

Forum statistics

Threads 1,295,171
Members 498,180
Posts 31,202,230
Top