Mvungi: Kafulila anashauriwa na 'shetani' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvungi: Kafulila anashauriwa na 'shetani'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 29, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk. Sengondo Mvungi,
  Alisema chama hicho kinasikitishwa na hatua ya mahakama kwa kuwa kinafahamu kuwa uamuzi huo umembomolea nyumba yake mwenyewe Kafulila huku kukiwa na ‘shetani’ anayemshauri.

  “Sisi tunasema aendelee kushauriwa tutafika tu,” alisema Dk. Mvungi.

  “Taarifa za agizo hilo tumezisikia kupitia watu wetu waliotupigia simu na wao habari hizo walizipata kwenye mtandao, sijui walimshawishi vipi Jaji, lakini sisi hili hatutashughulika nalo tena kwa kuwa amri hii imemuweka huyo Kafulila mwenyewe pabaya bila kujijua,” alisema Dk. Mvungi.

  ::HabariLeo
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nilishangazwa na ukimya wa mwalimu mvungi kwenye sakata zima la kafulila na nccr toka mwanzo,kumbe lilikua halijafika kwenye angle yake,sasa ndio limemfikia..
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Lugha ya "shetani" ni ya kichungaji zaidi kuliko ya mwanasheria.
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa nini unasema hivyo.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 28th December 2011 @ 14:50 - Habari Leo  CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema kitendo cha Mbunge wa Kigoma, Kusini David Kafulila na wenzake kuweka pingamizi la Mahakama, kuzuia hatua yoyote isichukuliwe kuhusu uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Chama kumsimamisha uanachama, ni sawa na kujimaliza mwenyewe.

  Pia chama hicho kimesema kufuatia amri hiyo kimefungwa mikono hivyo kinasimamisha hatua zozote kilichoanza kuchukua katika kutafuta suluhu ya suala hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk. Sengondo Mvungi, alisema hata hivyo chama hicho kimeshangazwa na agizo hilo la Mahakama Kuu ambalo limesikiliza upande mmoja wa Kafulila pekee.

  "Taarifa za agizo hilo tumezisikia kupitia watu wetu waliotupigia simu na wao habari hizo walizipata kwenye mtandao, sijui walimshawishi vipi Jaji, lakini sisi hili hatutashughulika nalo tena kwa kuwa amri hii imemuweka huyo Kafulila mwenyewe pabaya bila kujijua," alisema Dk. Mvungi.

  Akifafanua kuhusu hilo, alisema mara baada ya kikao cha Desemba 17, mwaka huu kumvua uanachama Kafulila na wenzake watatu, kuwavua wanachama wengine madaraka watatu na 17 kupewa onyo kali, siku hiyo hiyo, Kafulila aliandika barua kwa Mwenyekiti wa Taifa, James Mbatia akiomba uamuzi huo urejewe.

  Alinukuu barua ya Kafulila iliyosema "kutokana na uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa kuniondoa uanachama kwa unyenyekevu mkubwa naomba niwasilishe ombi kwa Halmashauri kwa misingi kuwa nimejitetea vya kutosha, nimeomba radhi kwa niliyokosea chama, Mwenyekiti na Katibu Mkuu…."

  Alisema kutokana na barua hiyo, chama hicho tayari kilishaanza maandalizi ya kuandaa Mkutano wa Halmashauri hiyo, lakini baada ya amri hiyo ya Mahakama, mkutano huo itabidi usitishwe hadi hapo kesi ya msingi itakapomaliza kusikilizwa.

  "Nawaambia kwa amri hii Kafulila amekula sumu, ilikuwa halmashauri ikutane na kurejea tena uamuzi wetu dhidi yake na wenzake, lakini kwa amri hii ya Mahakama haiwezi kukutana na sasa tumefungwa mikono, na tunaendelea na uamuzi wetu wa kumsimamisha hatutachukua uamuzi mwingine hadi kesi ya msingi iishe," alisema Mwanasheria huyo maarufu.

  Alisema chama hicho kinasikitishwa na hatua hiyo kwa kuwa kinafahamu kuwa uamuzi huo wa Mahakama umembomolea nyumba yake mwenyewe Kafulila huku kukiwa na ‘shetani' anayemshauri.

  "Sisi tunasema aendelee kushauriwa tutafika tu," alisema Dk. Mvungi.

  Alisema anashangazwa na wale wanaoshangilia huku akivishutumu vyombo vya habari kushabikia amri hiyo ya Mahakama na kudai kuwa uamuzi wa chama hicho kumsimamisha Kafulila, haukuwa wa kukurupuka na wala chama hicho hakikuufurahia.

  "Kwa masikitiko makubwa tumezuiliwa tusimsaidie Kafulila na wenzake na tunafurahi uamuzi wetu wa kumsimamisha uanachama haujatenguliwa na Mahakama kama inavyodaiwa, tunachosubiri ni kukutana mahakamani Januari 21, mwakani," aliongeza.

  Juzi Mahakama Kuu kupitia Jaji Alis Chingwile ilitoa amri ya kusitisha kutekelezwa kwa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR wa kumsimamisha Kafulila hadi kesi aliyoifungua itakapomalizika.

  Katika kesi hiyo, mbunge huyo anasimamiwa na Wakili Daniel Welwel.
   
 6. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lugha ya sheria ni ipi? Learned brother "know all". Hata mie naamini huyu jamaa amepagawa kutokana na kuutema ulaji wa dezo. Kimsingi, Kafulila is fighting a losing battle. In the end he will bite the dust comprehensively so to speak. He crossed Rubicon without being aware. Let him now face the music.
   
 7. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwanini Kafulia hataki kukubali ukweli kuwa amefulia na hawezi kujinasua? Kafulia go back to square one and divise new strategies if you have any. Otherwise you are a kicking ass. Shame on you for not underscoring that what you did to CHADEMA was totally ungentlemanly.
   
 8. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo siasa huwa chungu kwao na ndio mwanzo wa kufulia yeye kama aliwasilisha barua kwenye Nec ya nccr kwanini hakusubiri uamuzi kutolewa na ndo akaenda mahakamani?sasa ndo hatajua mshahala wa dhambi ni mauti.
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  huyu Dr. Mvungi sijui sheria kama anazifahamu vizuri...................au ni cheo tu cha udaktari......................yawaje Halmashauri kuu tena irudie maamuzi yake yenyewe.................yaani ikubali kula matapishi yake yenyewe...........alichofanya Kafulila kiko wazi kabisa hana imani kuwa NCCR itamtendea haki na mahakama tu ndicho chombo cha kuwasikiliza wanyonge........

  Hadi kesi ya kimsingi isikilizwe utakuta tumekwishaingia kwenye 2015...................na njama za kumvua ubunge kafulila zitakuwa zimeota mbawa.................................na hilo ndilo lengo hapo...........................kesi za bongo hazzishi leo wala kesho..........ni miaka 10 na kuendelea.........
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  Huyu Mvungi mpuuzi nini? Atasemaje wanataka kurejea uamuzi wa Nec yao wakati yule mpuuzi mwingine anayeitwa Ruhuza Samwel alishamwandikia barua spika kuhusu uamuzi wao? Ruhuza amenukuliwa mara kadhaa kuwa kashamwandikia barua spika na suala la Kafulila limeshafungwa Mbinguni na Duniani sasa huo uamuzi wa kurejea 'hukumu' kafulila angeusubiria wapi?
   
 11. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Shetani anatambuliwa siku hizi kwenye fani ya wanasheria hadi anaweza kuwa quoted na mtaalamu aliyebobea kama DK.Mvungi? je Dk Mvungi anaweza kumwita kutoa ushahidi mahakamani huyo shetani kuthibitisha kuwa yeye ni mshauri wa kafulila.

  Kama hadi magwiji wa sheria wanaamini kuna mashetani ambao ni washauri wa wabunge fani ya uanasheria iya wazawa iko hatarini.
   
 12. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Je imekuwaje huyo 'shetani' hakujionyesha katika kikao cha kamati kuu na sasa wanamuona wakati mahakama inapom-favor \kafulila over the party. Ina maana wao hawana 'shetani'!? Ni mawazo gani yanayopendekeza kuwa aombaye msamaha ASISAMEHEWE kama si ya 'shetani'!?
   
 13. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa wakuu niaje?

   
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Imetoka kwa gazeti la mwananchi, je huu ndo ushetani? Kwa Mbatia, Msajili wa Vyama na Mahakama.

   
 15. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kafulila mshauri wake ni Zitto kumbe Zitto ndio nanihi... duh! bora Mvungi umetujuza nasi tutamwepuka Zitto
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Namshauri Zitto awe anafikiria mara mbilimbili kabla ya kukimbilia FB.
   
 17. Jephta2003

  Jephta2003 JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2008
  Messages: 3,584
  Likes Received: 1,885
  Trophy Points: 280
  Let him fight for his life,walitaka afe kibudu bila kuparangana?,go kafulila go!
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Na mweyekiti wa NCCR anashauriwa na David Cameron aka David Matakka.
   
 19. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mvungi kaongea neno hilo kama mwanasiasa na sio kama mwanasheria.
  we dont believe the existence of devil ktk tasnia ya sheria.
   
 20. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huwa namkubali Mwl. wangu Dr. Mvungi, nadhani yeye ndio anastahili kuwa Mwenyekiti wa NCCR lakini kwa hivi vyama vyetu vilivyojaa umangimeza 'kichwa' kama Mvungi kinakua Mkuu wa ka idara. Tutafika?
   
Loading...