Mvua yaua watu wawili Unguja

Mvua yaua watu wawili Unguja

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Matolori ya kuuzia ice cream yakionekana kununiwa leo,huku wapita njia wakiendelea kupiga mbizi kwenye maji hayo mjini magharibi Unguja.
Hivi karibuni mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa Zanzibar iliwataka wananchi na mamlaka husika kuchukuwa tahadhari kutokana na msimu wa mvua za masika kutarajiwa kuanza wakati wowote.

Unguja. Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyosababishwa na mvua kubwa za masika zilizoanza kunyesha visiwani hapa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharib Unguja, Thobias Sedeyoka amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Aliwataja waliofariki kuwa ni mtoto, Hassan Mohamed (4) aliyezama kwenye dimbwi la maji ya mvua karibu na nyumba yao katika Shehia ya Jang’ombe na Skachi Abdallah Zahor (26) mkazi wa Kidongo Chekundu baada ya kuanguka na pikipiki (bodaboda) aliyokuwa amepakiwa katika eneo la Mazizini mjini hapa kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua.

Alisema jitihada za polisi kumtafuta dereva wa bodaboda aliyehusika na ajali hiyo hazijafanikiwa kwa kuwa alikimbilia kusikojulikana.

Kamanda Sedeyoka alisema kijana huyo alipata majeraha makubwa sehemu za kichwani na kuvuja damu nyingi na maumivu makali na kusababisha kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja.

Hivi karibuni mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa Zanzibar iliwataka wananchi na mamlaka husika kuchukuwa tahadhari kutokana na msimu wa mvua za masika kutarajiwa kuanza wakati wowote.

Mkurugenzi wa Kamisheni ya Maafa Zanzibar, Makame Ali Makame amewataka wananchi kuhama maeneo hatarishi au yalio karibu na maji katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za masika.

Swahili hub
 
Huyo kafa kwa ajari ya bodaboda au kwa ajiri ya mvua!?, na ni lini mvua imenyesha kiwango kikubwa kiasi hicho hapa jang'ombe mpaka mtoto huyo kufariki dunia!??

Nasema hivi hii habari ni ya kubuni tuu.HOVYO KABISA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa interested, kuja kuisoma ni upuuzi mtupu, yaani mtu amedondoka na bodaboda wanasema kazama na maji, dah!
 
Back
Top Bottom