Mvua yaikwamisha taifa stars kucheza na sudani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MVUA kubwa iliyokuwa ikinyesha bali ni manyunyu, lakini hali hiyo ilisababisha mchezo kati ya Taifa Stars na Sudani uliokuwa ufanyike jana ukwame.


Taifa Stars na Sudani zilitarajiwa kuumana kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tano katika michuano ya soka nchi za Bonde la Mto Nile.


Hata hivyo eneo ambalo uwanja wa Polisi uliokuwa utumike kwenye mchezo huo lipo lina mazingira ya maji, hivyo muda mfupi manyunyu hayo yaliponyesha palijaa maji, hivyo kuonekana pasingefaa kuchezewa.



Baadaye Chama cha Soka cha Misri kilitoa taarifa fupi kwamba kingefanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda unaotarajiwa kufanyika saa 11 kwa saa za Afrika Mashariki.



Akizungumza baada ya tukio hilo, Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyeambatana na timu mjini hapa, Idd Mshangama alisema watasikiliza wenyeji wao watakavayoamua kuhusiana na suala hilo.



Licha ya kuonekaba kwamba ni mvua ndogo, lakini ilisababisha baridi kali na anga ilikuwa imetanda mawingu mazito kuashiria mvua kubwa ilikiuwa inatarajiwa kunyesha.Mechi nyingine za nusu fainali jana licha ya DRC na Uganda, ilikuwa kati ya Misri na Kenya ambazo zote zilitarajiwa kufanyika Uwanja wa petro Jet. Fainali itakuwa Jumatatu.
 
Back
Top Bottom