Mvua kubwa, upepo mkali, mawimbi baharini

Active

Content Quality Controller
Jan 30, 2008
639
964
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwamba kuanzia kesho kutakua na mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi kwa maeneo ya pwani.

Mikoa inayotajwa kuwa na uwezekano wa kuwa na mvua kuzidi milimita 50 katika saa 24 ni 'baadhi' ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma. Morogoro, Lindi na Mtwara.
 

Attachments

  • Tahadhari%20ya%20MVUA.jpg
    Tahadhari%20ya%20MVUA.jpg
    38.6 KB · Views: 1,086
Watanzania tunapenda kubishana sana. Taarifa za El Nino ambazo mzee WA Upako alizishushua hazikua zimetolewa na Wataalam WA Tanzania pekee na kwamba waliotoa taarifa hizo ni Wataalam WA Kimaataifa ambao ndio waliokuja kuona kwamba taarifa zimebadilika kutokana na kuwapo kwa mabadiliko ya ajabu baharini. Hayo ni mambo ya kawaida Duniani vinginevyo Japan na Marekani wasingekufa kwa Maafa maana mara nyingine taarifa zinakua na utata.
 
Taarifa hiyo imetaja mikoa husika.
Dar es Salaam wala Pwani haipo, kama ni mtihani mshafeli wote
 
Hata kama TMA ni wachemkaji, tuchukue tahadhari tu, tusije kuvuliwa kwa boti kama wale wa Jangwani na Jangwani
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwamba kuanzia kesho kutakua na mvua
kubwa, upepo mkali na mawimbi kwa maeneo ya pwani.

Hawa shwaini ni sawa na mshauri mkuu wa baba ritz (sheik yahya).
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwamba kuanzia kesho kutakua na mvua
kubwa, upepo mkali na mawimbi kwa maeneo ya pwani.

Ikifika kesho watasema,pepo za kus zimebadilika,kutakuwa na ukame karibia na jangwa
 
"Kiwango cha uhakika -Wastani"
Ni kiwango cha uhakika wa taarifa au mvua kunyesha? Kiswahili kigumu.
 
Back
Top Bottom