Mvua kubwa inaendelea kunyesha Geita

Mvua kubwa inaendelea kunyesha Geita

Lipijema

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2015
Posts
953
Reaction score
1,540
Watu tumo ndani ya majumba na wengineo wakiangaika kuokoa mali zao.

Mvua inanyesha Buseresere na Katoro Geita, ni mvua kubwa sana ni ya mawe na upepo mkali, imeanza ghafla tu mida ya saa6 mchana huu.

Tukiwa ndani tunashuhudia miti ikikatika na baadhi ya bati zikiezuliwa, watu wanajaribu kuokoa mali zao.Kwani maji yanakuja kasi kama mto hatujajua maeneo ya mabondeni na yenye miti ikoje, hata hivyo kwa sasa ninapomalizia taarifa hizi yaelekea kukata kwa mvua hii iliyonyesha takribani lisaa moja.
 
Poleni sana ila huko ndio kule mlikoongoza kwa kuwaua alibino.
 
Inashangaza sana.
Huku kwetu jua kali hata nje tunaogopa kutoka
 
Vipi gorofa yangu hapo lubambe haijaanguka,make mi nipo mbali sana
 
Aisee bni zile zilizotabiriwa na mamlaka ya hali ya hewa ama ni msimu tu huko?kwa maana huku Dar tokea wamesema ule ubashiri wao hakuna tone lililodondoka!Hawa watu wa hali ya hewa wanaweza kukuingiza kwenye hasara ukifuata ushauri wao ni hatari sana.
 
isije ikawa ndio zile za kutengeneza. Alafu wanasiasa wajitokeze kutoa rushwa ya misaada.

Kujitaftia kick ya kuchaguliwa maana sikuizi siasa ni mahesabu.
 
Na hili nalo kuna watu watasema tatzo CCM

We ndo uliyesema,
au uko kitengo cha propaganda?
Kiasi kwamba kila posti ni lazima utaje hilo dubwana lako?

Poleni sana wanakatoro/Buseresere, tuombe kusiwe na madhara makubwa.
 
Mhhh! maajabu hayo! mbona hapa Geita mjini naona vumbi tu linatimka! hakuna cha wala nini. Kilio kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa geita ni tatizo la kukatika kwa umeme yani imekuwa ni janga.
 
Back
Top Bottom