Mvua Kubwa Dar na maeneo mengine nchini...

Mvua Kubwa Dar na maeneo mengine nchini...

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,479
Reaction score
40,120
Mvua zimeanza kuanguka kwa wingi jijini Dar.

attachment.php


Hapa ni Jijini Dar mvua ikifanya mambo yake.

Mamlaka ya Hali ya Hewa walishatoa tahadhari ya mvua kubwa zitakazoanza leo hadi tarehe 7.

attachment.php
 

Attachments

  • DSC00318.JPG
    DSC00318.JPG
    776.6 KB · Views: 1,798
  • MVUA.png
    MVUA.png
    24.8 KB · Views: 315
  • mvua.png
    mvua.png
    34.7 KB · Views: 1,617
Wambie jamaa wa wliojenga bonde la jangwani waanze kuhamisha chombo kimoja kimoja kabla ya dhahama haijawakuta, na kwasasa serikali haina ela za kuwasaidia chakula na malazi kwani ela yote ipo ktk bunge la katiba.
 
Nawasikitikia pia wakazi wa Kijitonyama, Mwananyamala, Mbezi, Tegeta sambamba na wale wote wenye mahaba na mabondeni.

Kuna dalili kwamba ardhi imetota maji hivyo kutokea mafuriko na madhara dhidi ya binadamu ni jambo lisilozuilika.

Nawakumbusha wale ambao chemba zao zimesumbua na kujaa, huu ndo wakati wake wa kudumisha utamaduni uleeee...
 
Hii mvua kunyesha kidogo kitaa kuna maji balaa ajabu yananuka harufu ya mkunyo,hii hatari sana Mungu atuepushe kwa kipindupindu na kichocho.
 
Hapa wa2 wanaoishi mabondeni wanatakiwa kuhama haraka sana.
 
Jamani wapendwa habari za asubuhi.

Hivi jamani hii mvua ni kwa hapa Dar tu au mikoa yote? watu tunashindwa hata kwenda kazini, watoto shule ndo hakuendeki, foleni ndo usipime huko barabarani.

Mamlaka ya hali ya hewa tunaomba mtujuze mwisho lini au zinaendelea.
 
Kiongozi uko Dar yapi ambako kuna mvua kubwa sana?mm mbona nimeenda kazini na kuna mvua ya rasha rasha tu?
 
Hali ya hewa walitoa tamko kwa mvua kubwa pwani kote mpaka Ntwara
 
Watu wa Dar kwa kumkufuru Mungu! yaani wanaona kua hapa hapapaswi kabisa kunyesha mvua kwa vile watu ni wafanyakazi, ila wamesahau kuwa hiyo mvua ndio inayoleta neema kwa wakulima ambao ndio wanatuzalishia chakula tunachokula? Hao mamlaka ya hali ya hewa hawana mamlaka ya kuzuia mvua, je ikinyesha mwezi si utamtukana Mungu kabisa. Wewe utakua mkazi wa mabondeni maana unaogopa uenda itakuja mvua kubwa uchukue tahadhari ila unaposema leo kuna mvua kubwa hadi sasa bado sijaiona.
 
kwa habari nilizonazo,itanyesha siku 3 mfululizo ukanda wa pwani
 
mvua ipo lakini sio ya kutisha kiasi cha watoto kutokwenda shule na wafanyakazi/wafanyabiashara kutokwenda kazini, sema kuna foleni za hapa na pale kama kawaida. Ila tunashukuru jamani kwa mvua, hali ya hewa inakuwa nzuri sana, hakuna joto, na wenye mashamba kwa kweli ni shukrani kwa Mungu tu, kila siku joto tuuuu, hii safi shida ni wanaokaa mabondeni, poleni sana
 
Back
Top Bottom