mvua inayoendelea katika jiji hili la Dar es salaam ni Neema kwa wapendanao.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Kwa siku tatu mfululizo hapa dsm kuna mvua kubwa karibia kila eneo. Mvua hii imeketa madhara makubwa baadhi ya sehemu mbalimbali za jiji, Lakini kwa wapendanao, Wapenzi, Wachumba na wanandoa ni jambo la heri kwao.

Kwa wale wenye wapenzi waliokuwa wamekorofishana, hawaongei usiku, hawasogeleani, hawakumbatiani na wala hawapeani haki ya msingi ya ndoa siku hizi tatu uvumilivu umewashinda mambo hayo yatakuwa yametokea mubashara bila chenga.

Mvua kwa wapendanao inawafanya wajisikie kama dunia ni yao, wanajiona wao ndo wao, wanapeana maneno matamu wakiamini anayeweza kusikia ni mwenyez mungu tu binadamu wa kawaida wamelala makwao hata wale wazee wa chabo hawapo.

Mvua inafanya usikie sauti tamu ya mpenzi wako, akikusifia na kukupongeza, akitoa shukrani kwa utamu unaompatia, sauti hiyo huwa ya juu huku wakiamini hakuna mwingine anayoisikia zaid ya mwenyezi.

Mvua inafanya upate joto la mpenzi wako kwa kiwango cha juu hapo ndipo unapogundua tofauti ya joto litokanalo na moto au jua na lile unalopata toka kwa mpenzi wako.

Kama kuna watu wanaichukia mvua hasa za usiku ujue hao hawana wapenzi maana hata kama ulikorofishana naye mvua itawapatanisha. ULE WIMBO WA MVUA NA JUA BORA NINI NIMEPATA JIBU LAKE BORA MVUA.
 
Sisi tusio na ma-baby ni mda mzuri wa kuomba dua,,,zina uwezekano mkubwa wa kukubaliwa...

Labda na sisi tutajaliwa wenza tuenjoy mautraaam na haka kabaridi
 
Na vibaka je mbona umewasahau, wengine mvua ikinyesha tunalala nusunusu
 
Kama wewe unategemea mvua ndio mpeane mauhondo matamu na mpenzi wako una tabu kweli aisee
 
Back
Top Bottom