Mvi katika umri mdogo husababishwa na nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvi katika umri mdogo husababishwa na nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Kashaija, Jan 28, 2009.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tafadhali naomba msaada wenu Madaktari au kwa yeyote anayejua!

  Zamani nilikuwa na imani kwamba mtu anayestahili kuota mvi ni mtu wa makamo hasa kuanzia miaka 60 na kuendelea, lakini siku hizi nimegundua mawazo yangu hayo hayakuwa sahihi maana hata vijana wa miaka 30 wanaanza kuota mvi.

  Nini chanzo au nini husababisha mtu kuota mvi katika umri mdogo?
   
 2. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  It's in the genes. Genetic makeup and sometimes extreme stress!!
   
 3. mwanakwetu

  mwanakwetu Member

  #3
  Feb 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkubwa mi sio mtaalam wa tiba ila ni miongoni mwa wale walioathiriwa na tatizo hilo. Lakini mzee mi umri wangu ni miaka 30 na nimeanza kuwa na mvi toka nikiwa na miaka 20. Jibu nililonalo ni kwamba mvi katika umri mdogo husababishwa na genes (urithi). Mzee wangu yeye alikuwa nazo toka akiwa na miaka 15, naye alirithi toka kwa bibi yangu. Sifahamu sababu za kitaalam, labda wataalam wetu wa afya wanaweza kutuongezea ufahamu zaidi.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Watu wanasena ni chanzo cha kuwa bahati na kuukata!

  Ndo habari ya mitaani!

  Je wewe ulishaukata tayari ndugu? usitusahau ndugu yetu!
   
 5. Violet

  Violet Member

  #5
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na tofautisha mvi za kurithi( hizo za miaka 20,15) na kuna mvi za stress
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Udadisi ulimuua paka. Msiulizeulize sana msije mkatuletea balaa. Hii nchi si mnaijua wenyewe. Walianza na wenye vipara.
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mvi za kurithi ni kweli, hutokea kijana mdogo akawa na mvi na ukifuatilia utakuta kuna ndugu zake nao walikuwa hivyo. Kuna bwana mmoja tulisoma nae O level alikuwa nazo kibao. Pia unapokuwa na matatizo na kufikiri kwa kupitiliza unaweza onekana mzee kuliko umri wako, hivyo kama una msongo wa mawazo (stress) ama sonona (depression) inaweza leta uzee, na kwa kuwa mara nyingi uzee huambatana na mvi basi huenda pia misongo na sonona husababisha mvi.
   
 8. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mvi ni urithi, maana nina mtoto wangu wa miaka 10 anazo tayari na anazipenda sana kwa sababu babu yake anazo anasema yeye ni mkubwa kama babu. Sasa huyo ana stress gani? mimi mwenye zimejaa tele at my age (32).

  Jibu sahihi ni urithi.
   
 9. B

  Benypupah New Member

  #9
  Jun 22, 2016
  Joined: May 22, 2015
  Messages: 2
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Nadhani wachangiaji waliotangulia wapo sahihi tatizo la mvi katika umri mdogo ni sababu za kurihti ( hereditary) ingawa nimewahi kusikia pia kuwa zinasababishwa na ukosefu was virutubisho lakini Mimi sioni kama inaukweli, hiyo labda tupate uthibitisho wa kisayansi
   
Loading...