GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 5,222
- 7,075
Tanzania tumefikwa na msiba mwingine wa kuzama kwa meli MV Nyerere inayofanya safari zake katika ziwa Victoria. Katika kipindi kisichozidi miaka kumi tumeshuhudia ajali za namna hii zikijirudia kwa kufuata mlolongo wa matukio yanayofanana na hatimaye kupoteza idadi kubwa ya watanzania ambao kwa namna yoyote ile hawawezi kuepuka kutumia usafiri wa majini.
Tukio la kuzama kwa meli ya MV Nyerere ni uthibitisho tosha unaoisuta jamii jetu kwa kushindwa kujifunza kutokana na majanga yaliyopita ili kuzuia hatari ambazo zingeweza kuzuilika na labda pale inaposhindikana kupoteza idadi ndogo ya waathirika.
Vyombo vingi vya usafiri viko katika hali ya uchakavu wa hali ya juu, meli zote zinazotoa huduma ziwa Victoria na Tanganyika ni chakavu kuliko hata umri wa Tanzania. Pamoja na uchakavu huo makosa ya kibinadamu ndiyo yanayochukua sehemu kubwa kwenye vyanzo vya ajali karibu zote.
Mwaka 1995 niliwahi kusafiri kwa MV Liemba kutoka Mpulungu hadi Kigoma. Kati ya mambo yaliyonishangaza sana ni ukongwe wa meli hiyo ukijumlisha na mzigo inaobeba katika safari zake kwenye maeneo yasiyofikika kwa njia ya barabara. Pamoja na ule msemo wa ukubwa ni dawa, bado meli hii inaendelea kupiga kazi kwa kudra za mwenyezi mungu... Tuombe tu mungu atunusuru na majanga haya LAKINI tuchue hatua madhubuti kwa kujifunza kupitia makosa yetu.