sikuzamwisho
Member
- Apr 12, 2019
- 48
- 185
Muziki wa dansi hakika Unarejea mdogo mdogo kwenye Hadhi yake kama ilivyokuwa zamani,pamoja na kupotezwa na Wadau ili muziki wa kizazi kipya ushike chati lakini ni faraja kubwa kwa Sisi wafia dansi kuona Vipindi vya dansi vimerudi maredioni na kwenye TV [emoji342] mbalimbali hakika Tunaona mwanga Jumamosi na jumapili ni sikukuu za muziki wa dansi vipindi kama vyote Tunajivunia Watangazaji na DJS ambao Wanadamu ya Muziki wa dansi na Wanajitoa kuupambania muziki huu mzuri,Wanamuziki pia hawapo nyuma kuachia ngoma kali ambazo pia Zinapatikana YouTube kama Mama wa Kambo na Nakuita wa Boggos Musica aka nyumba ya Baba chini ya Nyoshi El Sadaat aka Raisi wa milele,Yawe na mwisho wa mwezi za CP academia aka Ngwasuma full dose,Usiku wa manane wa mjengoni classic band,Samatta na Rekebisha za Twanga pepeta,2 way Traffic wa Ally Choki na Kaa la moto na Happy za Juma Kakere hakika dansi imerudi kama kawaida,Tunafurahia pia damu mpya za Kizazi kipya cha dansi kama Muu Bella wa Boggos,Kelly Hasso,Piano wa twanga na Wanamuziki wengine wanaokuja juu na kuifanya dansi ibaki kileleni,Nenda kwenye maonyesho ya Msondo Ngoma Uone Tx Moshi Junior na Rijo Voice wakiwasha moto hakika Utakubali japo bado Tunapambania viingilio kwenye maonyesho ya dansi Hatutaki KIINGILIO bia au kinywaji yaani huu muziki ni Mtamu balaa