Baada ya kutangaza kutekeleza maazimio ya Baraza kuu ya kutomtambuwa Dr Shein Kama Rais halali wa Zanzibar na kuwataka wafuasi wao kutowapa ushirikiano seikali ndivyo hali halisi ilivyo.
Kule Pemba yanayoendelea hayasemwi lakini ni wazi yanaisumbuwa serikali ya Dr Shein. Viongozi wake na wasaidizi wake wanataabika sana bila ya mafanikio. Viongozi wa mikoa na wilaya hawasikilizwi na hata watu wa dini wamewakataa kabisa.
Migomo na kususiana kijamii (Social boycoat) imeshika kasi na jamii imeparaganyika.
Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wanalalama na kuilazimisha serikali ichukuwe hatua. Wanamlalamikia Maalim Seif na CUF kuwa ndio Sababu.
Serikali haina pesa Kutokana na kunyimwa baadhi ya misaada ya maendeleo. Biashara zimekuwa ngumu na hali ya kisiasa haitabiriki.
Viongozi wakuu wanalazimika kupishana kwenda kujaribu kutuliza hali. Bado mnyukano unaendelea na watu hawasikii kabisa.
Vyombo vya ulinzi viko busy na harakati za kisiasa za CUF , ni kana kwamba serikali yote inacheza ngoma inayopigwa na CUF bila kutaka.
Tumemuona Dr Shein akilazimika kwenda kuzungumza na wanachama wa chama chake sijui kulikuwa na ratiba hio au ni baada ya mdundo wa Maalim Seif kule Zanzibar.
CUF wanaendelea kupiga ngoma na serikali inaendelea kuicheza.
Mwisho wa mdundo huu ni nini?