RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,052
- 529
Fanyia kazi huu ushauri haraka sana na wakati mwingine toa mkataba wa muda mfupiNikweli unapaswa kumpa kiunua mgongo kwani amekutumia tangu mwaka 2020 mpa leo.Kitaalamu ulipaswa umpe mkataba wa miezi mitatu mitatu ili kuepuka kumpa kiinua mgongo cha kufanya mpe hiyo 150 muachane tu ila akienda kukushtaki kwenye swala la kazi utalazimika kumlipa zaidi ya hiyo.Me nimuajiriwa niko serikalini taratibu za kazi nazijua
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
KajichanganyaUmejifanya nice guy
Ni bora tuu umpatie hiyo pesa! La sivyo wewe mwenyewe tangulia mahakama ya kazi utalipa zaidi hata ya milioni 100Wanajamvi habarini za asubuhi,
Nilifunga mkataba na muuza duka wangu kwa ajili ya kazi ya duka langu.
Mkataba tuliufunga kwa mtendaji wa kijiji tarehe 7.1.2020.
Mkataba ulikuwa na mashahidi upande wake na mimi.
Pia alidhaminiwa na mtu mmoja mwenye mali zisizohamishika.
Tulikubaliana nitakuwa namlipa tsh 50,000/= kwa mwezi.
Kwa kuwa nina kamgahawa tulikubaliana atakula hotelini kwangu ugali samaki au nyama mara mbili kwa wiki, na siku zingine wali maharage na mbogamboga angepewa kama zitakuwepo.
Pia kwa kuwa alikuwa anatokea wilaya nyingine tulikubaliana nimpe makazi, kitanda na neti na kiwe na umeme ambapo nagharamika mimi.
Makubaliano tulivyoandikishana ilikuwa kwamba nisiporidhika na utendaji wake nina haki ya kumwachisha kazi na niwe nimemlipa malipo yake yote ya 50,000 kwa kila mwezi.
Kwa kuwa utendaji wa kijana umekuwa duni sana na imeshindikana kujirekebisha nimeamua kumwachisha kibarua.
Sasa kijana ananivimbia eti siwezi kumwachisha kazi ghafla bila kumpa mafao ya kuacha kazi na atanishtaki labda nimpe malipo ya miezi mitatu (150,000) ili ajipange kupata kazi sehemu nyingine.
Sheria ya ajira za namna hii inasemaje ndugu wana JamiiForums?
Lukonge
Aendelee kuwa na kiburi wakamlipishe hela nyingi hadi akomeHakuna mshahara wa 50,000 unaotambulika senta ya umma au binafsi.
Kima cha Chini cha mshahara ni zaidi ya hiyo.
Hivyo mpe tu hiyo 150,000 muachane kiroho Safi.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Hadi msosi wanahesabiana.Watu mko serious na mikataba[emoji28].
Mpe hiyo hela kwa maandish iachane nae Chief asije kukuletea jauWanajamvi habarini za asubuhi,