Muungano wetu na Uchaguzi Kinondoni: Tafadhali wanasiasa msitutoneshe

Hoja sio kwamba ni Mzanzibar hoja ni kuwa sio mkazi wa kisiasa wa Kinondoni wala mpiga kura wa eneo la kinondoni sasa anafahamu vipi mahitaji ya kisiasa ya wana kino?
Huyo anayeyajua mbona alikimbia ubunge sasa anarudi nini tena.Kutia gharama tuu wananchi
 
Hakuna mtego wala waya. Waende chambani huko
Wenye akili wanaona mtego wa kisiasa kwa CCM kuhusu Uchaguzi was Kinondoni vs Sera ya CCM kuhusu Muungano LOFa kama were huwezo kuona asilani ,kama amvavyo uuwezi kuona makalio yako!
 
Hoja sio kwamba ni Mzanzibar hoja ni kuwa sio mkazi wa kisiasa wa Kinondoni wala mpiga kura wa eneo la kinondoni sasa anafahamu vipi mahitaji ya kisiasa ya wana kino?
Tukiwa na akili kama hizi tutajikuta wote siyo wakazi halali wa Kinondoni.
 
Kuna dalili naanza kuziona mitandaoni kuhusu uzanzibar wa bwana Mwalimu na kugombea Kinondoni. Tafadhali sana kampeni zenu zisiuchafue Muungano wetu. Tafadhali chama chochote cha siasa kisikisimange chama kingine eti kumsimamishe mzanzibara...!! Kampeni zenu ziwe za kistaarabu zisiuguse Muungano wetu. Muungano wetu n mzuri sana, unachangamoto kweli..but kampeni hizi zisitugawe.

Sitegemei kusikia msimchague kwakuwa yule ni mzanzibara..Zanzibar siyo Nchi Bali ni sehemu ya Tanzania..wanaye Rais kwakuwa waliofanikisha Muungano waliona si busara kuwa na serikali moja ni kuizamisha Zanzibar; Hakuna muungano usio na changamoto dunia kote.

Usiku mwema.
Hoja si uzanzibara au uzanzibar, hoja ni kuwa sheria na katiba zinasemaje kuhusu kugombea ubunge kwa rfaia wa Tanzania? Tusisahau Wazanzibar ni watanzania ingawa Watanganyika uraia wao Zanzibar ni changamoto ingawaje hawakataliwi.
 
Cdm ningependa wajipange vizuri pindi watakapokuwa wanapanda jukwaani, wapange watu mahiri wa kuongea. Napendekeza wajipange kwenye mambo manne. tuchukulie mkutano wa wa masaa mawili.
  1. Uchumi: Hapa waelezee hali ya sasa ya uchumi nchini, ikiwemo ajira, kilimo nk Wawe na mchumi mzuri kwa kuelezea hii redundancy inayoitwa vyeti fake bila nafasi hizo kujazwa. Mabenk kufilisika, mikopo ya wanafunzi, ahadi za ccm kutokutekelezeka kama 50m@kijiji/mtaa, Kwanini umeme wa stiegler gorge, wakati awamu iliyopita tuliambiwa gas ndio kila kitu mpaka tukawa tunaimbishwa nchi nzima kama wendawazimu kuhusu uchumi wa gas. Hapa zitumike dakika 20-25.
  2. Hali ya siasa hapa nchini: Hapa izungumziwe demokrasia inavyominywa ikiwemo vyama vya upinzani kunyimwakufanya siasa lakini ccm ikiachiwa kutamba. Kupotea kwa watu kama Ben saa 8, mwandishi wa habari, shambulio la Tundu Lissu na kunyimwa haki za matibabu nk. Nashauri hapa kuwe na vijembe vya kisiasa na sio kejeli na matusi na hasa ikibidi hilo jina la kumuita Magufuli dictator lisitumike sana kwani ndio wanapopata kisingizio cha kusumbua wapinzani. Hapa ielezwe madhara ya kujaza wabunge wa ccm kwani wanaunga mkono hata mikataba mibovu na itolewe mifano kama walivyopitisha sheria ya gas na leo hawazungumzi lolote, Itumike tafsida kuelezea udictator wake. Hapa dakika 20-25.
  3. Cdm watafanya nini: Hapa cdm inabidi wawe wazuri kuonyesha iwapo wao watapewa madaraka watafanya nini kwenye ajira, maendeleo ya watu kama kujenga nyumba bora kwa kupunguza bei za vifaa vya ujenzi, zahanati kila kata, elimu bure mpaka chuo kikuu bure, kurejesha demokrasia, kurejesha uhusiano mwema na wafanya biashara, nk Hapa dk 20-25. Pia wanaweza kuweka dk 10-15 za maswali wangalau matatu na majibu kila mkutano.
  4. Mgombea kuzungumzia jimbo analolipigania matatizo na utekelezaji wake. Ahakikishe anapata taarifa za jimbo lake kupitia madiwani mbalimbali walioko hapo. Yeye ajikite kwenye matatizo ya watu wa jimbo lake tu, na siasa nyingine za kitaifa aachie wengine kama nilivyoainisha hapo juu. hapa atumie dk 30
Cdm wahakikishe wanafanya siasa za kistaarabu bila woga, lakini wawe na watu mahiri kwenye kuongea majukwaani na sio yale mambo ya kusema ilani iko kwenye website. Kisha wawe na watu watakoaratibu kutoa habari kwenye uchaguzi kuanzia vyombo vya habari rasmi na kwenye mitandao ya kijamii. Hapa picha na ujumbe wa kampeni ufike vyema. Tukio lolote ovu liripotiwe kwa nguvu kubwa. Siku ya uchaguzi tatizo lolote lijazwe kwenye makabrasha husika. Kwa mtindo huu tutakuwa tumewabana ccm vyema na sio kampeni za kishabiki tu bila mpangilio mzuri.
 
Wewe Chipa GM,
Hapa si kwamba kuna kuchafua Muungano bali ni kutekeleza yale yaliyomo kwa mjibu wa katiba ya jamhuri ya muungano huo. Katika katiba hiyo imebainisha wazi mambo ambayo ni ya muungano na yale ambayo si ya muungano. Masuala ya wabunge wa majimbo ya bara si ya muungano na yanatekelezwa na ZEC kule visiwani na NEC huku bara. Wapo watu kutoka bara ambao makazi yao ni Zanzibar na pia kuna watu kutoka visiwani ambao makazi yao ni huku bara. Chaguzi za nafasi za uwakilishi za ubunge au udiwani unazingatia makazi ya mgombea wala si uzanzibari au uzanzibara wake. Sasa huyo mliomteua si mkazi wa huku bara. Wabunge wa bunge la JMT kutoka Zanzibari wanachaguliwa kupitia majimbo yao ya Zanzibar na si kupitia majimbo ya bara. Huu ndiyo utaratibu kwa mjibu wa katiba yetu. Mkubali tu kwamba kwa hili mmekurupuka!
 
Hiyo katiba inayosema hayo labda ya kwako wewe lakini ya Tanzania, hakuna hitaji la ukaazi. Hitaji la pekee ni uwe Mtanzania. Ndiyo maana Hussein Mwinyi alikuwa mbunge wa Mkuranga, Lyatonga Mrema alikuwa mbunge wa Temeke, Rostam alikuwa mbunge wa Igunga, n.k.
 
Ili uielewe katiba inabidi uielewe yote in its totality na si kwa kutafuta kipengele specific. Huwezi ukaisoma katiba in piaces halafu ukadhani unafahamu katiba. Ndiyo maana kuna mamlaka za kuitafisiri ambazo ni pamoja na mahakama ya kikatiba. Subiri mgombea wenu atakapowekewa pingamizi ndipo tutakapopata hiyo tafisiri angalao ya upande wa NEC ambayo imesheheni wanasheria na inaongozwa na majaji wastaafu.
 
Cdm wahakikishe wanafanya siasa za kistaarabu bila woga, lakini wawe na watu mahiri kwenye kuongea
Point zako zote ni irrelevant
Huwezi kuongelea uchumi kwenye uchaguzi wa jimbo moja,na ukiongelea tundu lissu ndio kabisaa
Makosa yenu ni yale yale,mambo ya kitaifa kupeleka kwenye kampeni ya jimbo,mwisho wa siku mtalia mmeibiwa
 
Kuna dalili naanza kuziona mitandaoni kuhusu uzanzibar wa bwana Mwalimu na kugombea Kinondoni. Tafadhali sana kampeni zenu zisiuchafue Muungano wetu. Tafadhali chama chochote cha siasa kisikisimange chama kingine eti kumsimamishe mzanzibara...!! Kampeni zenu ziwe za kistaarabu zisiuguse Muungano wetu. Muungano wetu n mzuri sana, unachangamoto kweli..but kampeni hizi zisitugawe.

Sitegemei kusikia msimchague kwakuwa yule ni mzanzibara..Zanzibar siyo Nchi Bali ni sehemu ya Tanzania..wanaye Rais kwakuwa waliofanikisha Muungano waliona si busara kuwa na serikali moja ni kuizamisha Zanzibar; Hakuna muungano usio na changamoto dunia kote.

Nikiri tu wazi kampeni za Ccm ntazifatilia kila sentensi watakayoisema. Nataka nione political maturity ya CCM.

Usiku mwema.
Hahahahahaaaa. 2015 agombee zanzibar halafu mara pap 2018 Kinondoni. Hiyo big noooooo.
 
Kuna dalili naanza kuziona mitandaoni kuhusu uzanzibar wa bwana Mwalimu na kugombea Kinondoni. Tafadhali sana kampeni zenu zisiuchafue Muungano wetu. Tafadhali chama chochote cha siasa kisikisimange chama kingine eti kumsimamishe mzanzibara...!! Kampeni zenu ziwe za kistaarabu zisiuguse Muungano wetu. Muungano wetu n mzuri sana, unachangamoto kweli..but kampeni hizi zisitugawe.

Sitegemei kusikia msimchague kwakuwa yule ni mzanzibara..Zanzibar siyo Nchi Bali ni sehemu ya Tanzania..wanaye Rais kwakuwa waliofanikisha Muungano waliona si busara kuwa na serikali moja ni kuizamisha Zanzibar; Hakuna muungano usio na changamoto dunia kote.

Nikiri tu wazi kampeni za Ccm ntazifatilia kila sentensi watakayoisema. Nataka nione political maturity ya CCM.

Usiku mwema.
Well said. But hiyo ni dhambi dhidi ya Muungano inawarudia. Wakati wa Mchakato wa Katiba, kupitia kwa Mwanasheria wenu msomi, alidai kuwa hakuna Muungano bali ghiliba za waliozoea kudanganya na hakuna hata Hati Halisi ya Muungano.

Kauli hizo zilikwenda mbali hadi kumtukana Baba wa Taifa, ambaye in his absence, hakukuwepo mtu wa kumtetea.

Kwa mantiki hiyo, kwa mujibu wa Imani ya CHADEMA, hakuna Muungano kwa sababu kulikuwa na ghiliba.

KUNA MAISHA NJE YA UONGO.
 
Hoja sio kwamba ni Mzanzibar hoja ni kuwa sio mkazi wa kisiasa wa Kinondoni wala mpiga kura wa eneo la kinondoni sasa anafahamu vipi mahitaji ya kisiasa ya wana kino?

raisi wa inch ana tokea chato je shida za tanga ana zijua?jibu ni hapana ana wakuu wa mikoa changanya na wa wilaya ongeza na wizara!! na yeye pia madiwani wapo-acha kujibu hoja ki baguzi mkuu
 
Hussein Mwinyi alikua mbunge mkuranga pwani na sasa mbunge Huko zanzibar na anaishi dsm bara.
Mbawara waziri bara wizara isiyo ya muungano
Kaisome vizuri yale mambo ya muungano utaona Telecommunication na mambo ya bandari ni Muungano. Nimegundua wengi wa watu hapa hawajui mambo gani ya Muungano na yepi siyo..
Hata Hussein Mwiynyi katika wizaya yake kuna mambo si ya Muungano kama JKT kwani Zanzibar wana lao JKU. Wizara ya Elimu kwani Elimu ya Juu ni Muungano sasa siku ambayo atashika mzanzibar mtasema wizara si ya Muungano?
Someni vizuri
 
Point zako zote ni irrelevant
Huwezi kuongelea uchumi kwenye uchaguzi wa jimbo moja,na ukiongelea tundu lissu ndio kabisaa
Makosa yenu ni yale yale,mambo ya kitaifa kupeleka kwenye kampeni ya jimbo,mwisho wa siku mtalia mmeibiwa

Nimeanisha nini cha kuongea na kwa muda gani. Sasa hivi hakuna kufanya siasa nchi nzima, hivyo hiyo ni platform ya kufafanua vaadhi ya mambo yaweze kufikia wananchi wengi.unadhani hilo jimbo sio sehemu ya Taifa kiasi hawatakiwi kusikia mambo ya uchumi? Kumuongelea Tundu Lissu ni kuvunja sheria gani!?
 
Back
Top Bottom