Tundu Lissu ameongea na waandishi wa habari, afafanua vitisho vya Amsterdam kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na suala la kuunga mkono Ushoga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,632
218,062
Mkutano na Waandishi wa Habari Mahali_ Makao Makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa Kino ( 640 X 640 ).jpg

Hii ndio Taarifa mpya inayozunguka duniani kwa sasa .

Endelea kutegea sikio

===

Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Demakrasia na Maendeleo (Chadema) Ndugu Tundu Lissu leo amekutana na Waandishi wa habari ambao walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali ambapo Mgombea huyo aliyajibu.

Wakimuuliza kuhusu Wakili wa Kimarekani aliyeitwa Amsterdam kumtisha Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini, Tundu Lissu alisema "Bob Amsterdam mwenye Ofisi London na Washington DC ni Wakili wangu na wanashughulika na masuala yangu yote ya kisheria ya nje ya nchi hii. Wanafuatilia kwa ukaribu haya yanayoendelea katika nchi hii kwahiyo kama tume imeandikiwa barua na Bob Amsterdam kuhusiana na masuala yote ya Uchaguzi huu ni kwa sababu Bob Amsterdam na Washirika wake ni Mawakili wangu wa kimataifa.

Anaongeza "kama nilivyosema ndugu zangu Uchaguzi huu hatutaki mchezo, kama tukiendelea na huu mchezo wa kupigwa pigwa Mabomu kuna watu watakaa milele maisha yao Tanzania, wakitoka nje tu wanadakwa. Kwahiyo, hivyo sio vitisho na sio wao tu hata ndugu zao wakitaka kwenda nje hakuna Visa, business Associate wao wakitaka kufanya International Transactions wanashughulikiwa.

Aidha, akijibu swali kuhusu masuala ya Ushoga Tundu Lissu amesema, "Kuhusu masuala ya Ushoga hii wamekosa hoja kabisa, hoja ambazo kwa miaka mitano ya utawala katili katika historia ya nchi yetu haina majibu, hoja ya kwamba wametapanya pesa za Watanzania haina majibu, sasa niseme nilichosema all along tangu walipokuwa wameleta hii hoja. Katiba ya muungano wa Tanzania kama ilivyo sasa hivi inasema kila mtu ana haki ya kulinda falagha yak, The Right to Privacy haki ya kuwa na falagha kwenye maisha yako ya chumbani na mkeo na yeyete yule mkishajifungia chumbani Serikali ni marufuku kuchungulia hiyo ndiyo katiba ya Tanzania kama ilivyo. Sasa nimesema na naendelea kusema mimi naunga mkono msimamo huo wa katiba kwamba sio business ya Serikali kuchungulia kwenye vyumba vya watu, tukiiruhusu Serikali kuchungulia vyumbani kujua tunafanya nini na wenza wetu maana yake itafika hatua watasema sasa wewe mbona ufanyi sawa sawa.

Anaendelea kuwa, Masuala ya Privacy (falagha) yanayofanyika kati ya watu wazima ni masuala ya falagha serikali ni marufuku kuingilia, Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba kama ilivyo leo na kama ilivyotungwa miaka ile. Kwa hiyo msimamo wangu ni huukama kweli wanapinga ushoga waondoe hii kanuni inayolinda kuchungulia vyumbani mwetu na katiba hii ni katiba ya CCM tunalalamiaka miaka yote, wayafute basi. Pili, kama kweli wao wanapinga ushoga watuambie lini, walimkamata nani, wakamshitaki nani kwa ushoga. Mimi Mwanasheria napatia mkate wangu Mahakamani, sijawahi kusikia mtu amefungwa ushoga vikampeni vya kijinga kabisa vya watu ambao wameishiwa hoja kabisa.

Kuhusu kukosa Wagombea katika maeneo mengi Nchini, Tundu Lissu amesema, " Kwa mara ya kwanza katika historia ya kugombea nchi hii sisi Chadema tuliweka Wagombea wa Ubunge katika maeneo yote ya Tanzania Bara na tuliweka wagombea 30 wa Ubunge Zanzibar, hatukuweka Wagombea katika Majimbo 20 tu yaliyopo Zanzibar kwingine kote tuliweka Wagombea, sasa mnafahamu zile mass discualification zilivyofanyia zile siku tatu. Wagombea wetu wa Ubunge walioenguliwa walifikia 63, tumepiga kelele ikiwamo kukata rufaa kuna wagombea 21 bado hawajarudishwa. Wengine rufaa zimeshaamuliwa kama majibo matatu hivi kwamba hawagombei. Sasa ni ajabu kwamba waandishi wa habari tumemaliza mwezi mmoja wa kampeni na Tume haijafanya maamuzi ya rufaa zao, hao Wagombea watakaporuhusiwa. Kwenye jimbo la Mnyeti wagoimbea wetu wote wa ubunge na Udiwani wamekuwa disqualified. Sasa tutachokifanya kwenye majimbo ambayo hayana Wagombea tutaweka mawakala ambao watasimamia kura za Urais


Aidha, kuhusu suala la kutangaza ushirikiano, Tundu Lissu amesema `hatutotangaza ushirikiano (hatuna Coalission). Kitu ambacho tumefanya ni tutafanya ni kuungana mkono katika maeneo ambayo sisi hatuna maslahi nayo. Hatuna maslahi kwenye Uchaguzi wa Urais wa Zanzibar, tumetangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif kama ambavyo Lytonga Mrema ametangaza kumuunga mkono Magufuli. Hiyo haikatazwi na sheria. Ingekuwa tumeungana tungeoaswa kupeleka makaratasi katika tume ya Uchaguzi lakini tunachiokifanya kumuungana mkono pale ambapo hatuna maslahi.

Kuhusu kuitikia wito wa Chama Lissu amesema kwakuwa wito haujamfikia yeye na kanuni zinaeleza kuwa anapaswa kuletewa yeye mwenyewe hivyo hakuna wito na anaendelea na kampeni.

Kuhusu suala la kuunda Serikali ya Mseto endapo atachaguliwa kuwa Rais, Tundu Lissu ameeleza Sisi wa Upinzani miaka yote tumesema kwamba katiba tuliyonayo haikidhi mahitaji ya kidemokrasia ya Vyama vingi, masuala ya Serikali ya mseto ni ya kawaida kabisa kwa nchi zinazofuata utaratibu wa kidemokrasia. Katiba yetu kimsingi ni katiba ya Chama kimoja bila katiba mpya hilo haliwezi kuwezekana.
 
Ongeeni na WANANCHI mubashara mnajaribu kuita waandishi wa Habari, hawazipi kipaumbele habari zenu, wanahabari wote wamepakatwa.

NB: Sasa hivi ninyi mnajiuza hakuna mabango wala nini,hutubieni Taifa ,andaeni utalatibu wa tumchangie ili muwe live TV,achaneni kabisa na wanahabari.
 
Msiache kukubali ofa ya ajira kwa Lisu ambayo Magufuli alitoa,

Kwamba Magufuli akipata awamu nyingine basi lisu atapata kanafasi ka kumfaa kwani Urais hatoshi.
 
All the best, natumai watatoa tathmini ya awamu ya pili ya kampeni waliyoimaliza jana, wazungumzie Lissu kuitwa na Tume, na mipango yao ijayo.
 
Back
Top Bottom