Muungano wetu na Uchaguzi Kinondoni: Tafadhali wanasiasa msitutoneshe

chipa GM

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
1,769
2,858
Kuna dalili naanza kuziona mitandaoni kuhusu uzanzibar wa bwana Mwalimu na kugombea Kinondoni. Tafadhali sana kampeni zenu zisiuchafue Muungano wetu. Tafadhali chama chochote cha siasa kisikisimange chama kingine eti kumsimamishe mzanzibara...!! Kampeni zenu ziwe za kistaarabu zisiuguse Muungano wetu. Muungano wetu n mzuri sana, unachangamoto kweli..but kampeni hizi zisitugawe.

Sitegemei kusikia msimchague kwakuwa yule ni mzanzibara..Zanzibar siyo Nchi Bali ni sehemu ya Tanzania..wanaye Rais kwakuwa waliofanikisha Muungano waliona si busara kuwa na serikali moja ni kuizamisha Zanzibar; Hakuna muungano usio na changamoto dunia kote.

Nikiri tu wazi kampeni za Ccm ntazifatilia kila sentensi watakayoisema. Nataka nione political maturity ya CCM.

Usiku mwema.
 
Cdm ningependa wajipange vizuri pindi watakapokuwa wanapanda jukwaani, wapange watu mahiri wa kuongea. Napendekeza wajipange kwenye mambo manne. tuchukulie mkutano wa wa masaa mawili.
  1. Uchumi: Hapa waelezee hali ya sasa ya uchumi nchini, ikiwemo ajira, kilimo nk Wawe na mchumi mzuri kwa kuelezea hii redundancy inayoitwa vyeti fake bila nafasi hizo kujazwa. Mabenk kufilisika, mikopo ya wanafunzi, ahadi za ccm kutokutekelezeka kama 50m@kijiji/mtaa, Kwanini umeme wa stiegler gorge, wakati awamu iliyopita tuliambiwa gas ndio kila kitu mpaka tukawa tunaimbishwa nchi nzima kama wendawazimu kuhusu uchumi wa gas. Hapa zitumike dakika 20-25.
  2. Hali ya siasa hapa nchini: Hapa izungumziwe demokrasia inavyominywa ikiwemo vyama vya upinzani kunyimwakufanya siasa lakini ccm ikiachiwa kutamba. Kupotea kwa watu kama Ben saa 8, mwandishi wa habari, shambulio la Tundu Lissu na kunyimwa haki za matibabu nk. Nashauri hapa kuwe na vijembe vya kisiasa na sio kejeli na matusi na hasa ikibidi hilo jina la kumuita Magufuli dictator lisitumike sana kwani ndio wanapopata kisingizio cha kusumbua wapinzani. Hapa ielezwe madhara ya kujaza wabunge wa ccm kwani wanaunga mkono hata mikataba mibovu na itolewe mifano kama walivyopitisha sheria ya gas na leo hawazungumzi lolote, Itumike tafsida kuelezea udictator wake. Hapa dakika 20-25.
  3. Cdm watafanya nini: Hapa cdm inabidi wawe wazuri kuonyesha iwapo wao watapewa madaraka watafanya nini kwenye ajira, maendeleo ya watu kama kujenga nyumba bora kwa kupunguza bei za vifaa vya ujenzi, zahanati kila kata, elimu bure mpaka chuo kikuu bure, kurejesha demokrasia, kurejesha uhusiano mwema na wafanya biashara, nk Hapa dk 20-25. Pia wanaweza kuweka dk 10-15 za maswali wangalau matatu na majibu kila mkutano.
  4. Mgombea kuzungumzia jimbo analolipigania matatizo na utekelezaji wake. Ahakikishe anapata taarifa za jimbo lake kupitia madiwani mbalimbali walioko hapo. Yeye ajikite kwenye matatizo ya watu wa jimbo lake tu, na siasa nyingine za kitaifa aachie wengine kama nilivyoainisha hapo juu. hapa atumie dk 30
Cdm wahakikishe wanafanya siasa za kistaarabu bila woga, lakini wawe na watu mahiri kwenye kuongea majukwaani na sio yale mambo ya kusema ilani iko kwenye website. Kisha wawe na watu watakoaratibu kutoa habari kwenye uchaguzi kuanzia vyombo vya habari rasmi na kwenye mitandao ya kijamii. Hapa picha na ujumbe wa kampeni ufike vyema. Tukio lolote ovu liripotiwe kwa nguvu kubwa. Siku ya uchaguzi tatizo lolote lijazwe kwenye makabrasha husika. Kwa mtindo huu tutakuwa tumewabana ccm vyema na sio kampeni za kishabiki tu bila mpangilio mzuri.
 
Bro wewe umekuja kiukada zaidi..asante sana. Mawazo yako mazuri sana.
 
Kama CUF halali hawasimamishi mgombea wao ningependa sana kuona mshikamano wa UKAWA kwenye hizi kampeni kwa kuwashirikisha Viongozi wa juu wa CUF halali ili kuomba kura za wanachama na wafuasi wa CUF halali.
 
Hoja sio kwamba ni Mzanzibar hoja ni kuwa sio mkazi wa kisiasa wa Kinondoni wala mpiga kura wa eneo la kinondoni sasa anafahamu vipi mahitaji ya kisiasa ya wana kino?
 
Hakuna sababu ya kuficha hisia! Kama ilivyo wewe mtanganyika hauwezi kugombea chochote nasi tutawanyoosha kwa debe, wanataka kupigiwa kura na machogo? Mwalimu hapati hapati ubunge hakuna haja ya kuficha
 
Kwenye hili mmeingia kichwa kichwa na wababe wenu wako kimyaaaa! Siku ya matokeo kutakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Hoja sio kupiga kura its just a metaphor of which its symbolise the moral authority of a person to stand and asks the constituency to have a trust and community to submit their civic rights to an individual who will represent their interests in the Parliament of which this mwanasiasa is not the member either by residency or voters registration of the kinondoni constituency.
 
Nilikua namhoji mkuu aliyecomment kwenye post namba 11, amesema mgombea hayajui mahitaji ya KISIASA ya wana Kinondoni

Hoja sio kupiga kura its just a metaphor of which its symbolise the moral authority of a person to stand and asks the constituency to have a trust and community to submit their civic rights to an individual who will represent their interests in the Parliament of which this mwanasiasa is not the member either by residency or voters registration of the kinondoni constituency.
 
Kuna dalili naanza kuziona mitandaoni kuhusu uzanzibar wa bwana Mwalimu na kugombea Kinondoni. Tafadhali sana kampeni zenu zisiuchafue Muungano wetu. Tafadhali chama chochote cha siasa kisikisimange chama kingine eti kumsimamishe mzanzibara...!! Kampeni zenu ziwe za kistaarabu zisiuguse Muungano wetu. Muungano wetu n mzuri sana, unachangamoto kweli..but kampeni hizi zisitugawe.

Sitegemei kusikia msimchague kwakuwa yule ni mzanzibara..Zanzibar siyo Nchi Bali ni sehemu ya Tanzania..wanaye Rais kwakuwa waliofanikisha Muungano waliona si busara kuwa na serikali moja ni kuizamisha Zanzibar; Hakuna muungano usio na changamoto dunia kote.

Usiku mwema.
Hussein Mwinyi alikua mbunge mkuranga pwani na sasa mbunge Huko zanzibar na anaishi dsm bara.
Mbawara waziri bara wizara isiyo ya muungano
 
Back
Top Bottom