Muungano wa Mkataba na Mtiririko wa Kisheria.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Written by Harith Ghassany // 22/03/2012 // Habari // No comments


Muungano wa Mkataba utapitaje bila nao kuwa na mtiririko wa Kisheria? Hakuna katika muswada/rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala Katiba ya Zanzibar ya 2010, kipengele cha Muungano wa Mkataba.
Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inaeleza wazi wazi katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza kwamba: “Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar”.
Ipi ina mtiririko wa Kisheria: Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo imetajwa ndani ya Katiba ya Zanzibar, au Mkataba wa Muungano ambao haumo ndani ya rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wala ndani ya Katiba ya Zanzibar ya 2010?
 
Back
Top Bottom