Wanitakiani
JF-Expert Member
- Apr 18, 2008
- 641
- 135
" hujui kama karibu gulf coutries zote zimejengwa/kuendelezwa na waZanzibari, baada ya mapinduzi wengi wao walipokimbilia sehemu hizo? ikiwa tumeweza kuzi transform nchi hizo kwa nini tusiweze kwetu? serikali moja hata hao madalali CCM Znz hawalitaki hili, sisi sasa tumo kupanga kupangua kuuvunja kabisa huu Muungano. HATUUTAKI kabisa!!"
habari ndo hiyoEneo la Unguja na Pemba kama ilivyo Mafia kijiografia ni sehemu ya ardhi ya iliyokua Tanganyika...
"nafikiri sahihi kusema eneo lote la Tanganyika lilikuwa ni ardhi ya Zanzibar. sijui wajua kama dola ya Zanzibar ipo kabla ya hiyo yenye kuitwa Tanganyika?"
Pili, asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wa Pemba na Unguja asili yao ni kutoka kwa mikoa ya iliyokua Tanganyika, tofauti ya tamaduni imetokana na tawala za kikoloni zilizokuwepo visiwani na bara.
"tupo wenye asili ya kutoka bara, lakini si kwa asilimia kama hiyo usemayo wewe. sijajua hili la utamaduni, nijualo kwa kweli utamaduni wetu ni tofauti kabisa na wa huko Tanganyika, lafudhi, chakula, tabia, nk. wapo waZenji wenye asili ya Tanganyika na bado wanaendelea na mila zao"
Hivi ushawahi jiuliza kabla ya uvamizi wa Waarabu ni kina nani walikua wakiishi katika visiwa vya Pemba na Unguja?
" ulipokuja huo uvamizi wa waarabu uuitao wewe, tayari Waarabu walikuwepo miaka mingi nyuma, tokea asili visiwa hivi ni mchanganyiko wa watu wa makabila mbali mbali tabu kusema nani kaja mwanzo. unajua nani kaupa jina mji wa Dar es Salaam? na ni neno la lugha gani na lina maana gani?"
Aisee, vunjeni hata sie hatuutaki kabisaaaaa! Sijuwi hao wanasias wanaofaidika nao. Kuna vyeo na maslahi wanayoyapata muungano ukiwepo. Lianzisheni wallah tutawasapoti!
Capital city dunia nzima huambatana na Ikulu. Sisi ni wa kwanza Duniani ambao mji mkuu na Ikulu viko sehemu tofauti
Paka hakamatwi sharubu bwana kiufupi hatutaki tena muungano haukuletwa na mungu,muungano huu unatambulika makaburini huko!
Ndugu Watanzania wenzangu. Jambo lisipingika kuwa hoja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imo mawazoni mwetu karibu kila siku. Mara Watanganyika wanalalamika na mara nyingi sana Wazanzibari wanalalamika zaidi. Wote hawa wanalalamika kwa kuwa kuna nchi mbili na kila moja anaona mwenzake anapata zaidi.
SULUHU YA MATATIZO YA MUUNGANO ni kuwa na NCHI MOJA TU badala ya nchi mbili kama ilivyo sasa. Kwa kuwa na nchi mbili tumesababisha yafuatayo:
1. Malalamiko yasiyoisha
2. Mgogoro wa CCM na CUF uliodumu kwa miaka zaidi ya 10 hivyo kuzorotesha maendeleo,
3. Kuwepo kwa Serikali mbili ya Muungano (ambayo ndani yake pia ziko mbili(Muungano na Tanganyika)) na ya Zanzibar
4. Uwepo wa viongozi wengi. Tunalazimika kuwa na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu bila sababu hivyo kuongeza gharama kubwa kwenye serikali.
5. Nchi moja kulazimika kuendesha mabunge mawili yaani lile la Muungano na lile Baraza la Wawakilishi.
6. Halama za kamati mbalimbali za pamoja za serikali na za vyama mbalimbali.
Kwa ujumla gharama ni kubwa sana zitokanazo na huu mfumo kuliko faida yake. Wakati tunaangali mchakato wa katibu mpya naomba pia tupate nafasi ya kuuangalia hili suala.
we ni mpemba asilia,mkivunja muungano na zanzibar inameguka vpande vwili unguja na pemba...
bro/sis: sisi tayari tumeshalianzisha zamani, linaendelea na halina kusita hadi kieleweke, support yenu ni muhimu sana kufanikisha hili. ni habari kubwa ipo Znz sasa, japo vyombo vya habari havitaki kuzitoa, kwa kukusaidia kidogo, tembelea "mzalendo.net" utapata mwanga wa jambo hili
Najua unataka kuwaudhi wazanzibari, hii sio suluhisho, tunahitaji serikali tatu. Hivi mafia ina mjumbe baraza la wawakilishi. Ni Tanzania bara ua visiwani?