Muungano utavunjwa kweli kwa style hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano utavunjwa kweli kwa style hii?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Saint Ivuga, Jun 1, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Muungano utavunjwa kweli kwa style hii?  05z.jpg 04.jpg
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wanao taka Kuuvunja Muungano watuwekee sababu kwa nini hawautaki,kisha na sisi Tunaoutaka tutawajibu kwa nini tunautaka,ujanja ujanja hautasaidia kikwara pia haitasaidia
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  labda kusiwepo na udini
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade Ivuga lengo la dini ni kutuweka pamoja na si kuhasimiana,kwa nini sisi dini haitusaidii kwa nini mihadhala ya kudai muungano uvunjike ianzie ndani ya masinagogi? kumbuka kauli hii ya Yesu/Issa ya Kisali (CCM,CDM,CUF etc) tumuachie Kaisali na ya Mungu (ukristo na uislam) tumuachie Mungu mwenyewe
   
 5. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa dini tofauti haiwezekani, kwani kila dini ina maudhui yake. Si unaona mambo ya sudan, nigeria.
   
 6. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Comrade Ivuga, lakini hii ni kwa ajili ya Ubinafs tu wa wanadamu,kujijali wao wenyewe wanadamu ndiko kunakotufikisha hapa kuna hadith nyingi za Mtume na Issa /Yesu kuhusu umoja,
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  Hujakosea kiongozi ila hapa ukweli ni kuwa kuna watu wana interest zao wanatumia udini ili kufikia matakwa yao.. Hawa ndio wa kuogopwa kama ukoma.
   
 8. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana Comrade lakini waonaje kwa nini Serikali ya CCM wasitoe Free Arena ya kuujadili Muungano tena kwa negative and pisitive then tuyachambue maoni yao inawezekana kabisa hata hao wana Uamsho hawana Hoja za Msingi za kuupinga Muungano,lakini kwa sababu hawataki kuwasikiliza basi wanaonekana wanahoja,
   
 9. T

  Taso JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Moja: Mimi Mtanganyika, siruhusiwi kisheria kumiliki ardhi ndani ya Zanzibar! Wao wanaruhusiwa kuja huku kwetu kumiliki ardhi, Muungano kwa hilo haunisaidii, unanidhulumu.

  Mbili: Mzanzibar anakuwa subsidized kwenye bili yake ya Umeme wa TANESCO wakati Zanzibar hawazalishi umeme, na wamekataa kuilipa TANESCO, na TANESCO ime capitulate ili "kulinda Muungano." Kwa hiyo bill yangu ya umeme ni kubwa kuliko ya Mzanzibar wakati Umeme unatoka kwetu. Dhulma nyingine kwa Mtanganyika.

  Tatu: Wazanzibar wana uwakilishi usioendana na uwiano wa watu. Kuna Wazanzibar milioni moja na ushee, kuna Watanganyika milioni na tano na ushee. Haiwezekani wakapewa wabunge 75! Watu wachache wanakuwa na sauti kubwa zaidi ya maamuzi. Katika mifumo ya kidemokrasia duniani kuna msingi mmoja unaoitwa "one man one vote" ukiwa na maana kwamba makundi ya wa watu wenye idadi inayokaribia kuwa sawa lazima yawe na wawakilishi wenye idadi inayokaribia kuwa sawa. Kuwezi kuwa na watu milioni moja wana wabunge 75! Hii ni dhulma kwa Tanganyika.

  Nne: Sasa hivi Tanzania kuna marais watano, Shein, Iddi, Kikwete, Hamad, na Billa! Tanganyika inabeba mzigo mkubwa kuhudumia viongozi wa juu wa nchi, madarakani na wastaafu, waliojaa kutokana na muungano. Na familia za viongozi wa Kizanzibar za wake wengi wengi ( Billa, Mwinyi) zinatuongezea mzigo usio na sababu. Tunawahudumia mpaka wafe! Mzigo!

  Tano:
  kutokana na mipaka ya mamlaka ya pande mbili za Muungao kutokuwa delineated, Wazanzibar wamo kwenye uongozi katika maeneo ambayo si ya Muungano, mfano Waziri Mwinyi, Afya. Kero!

  Sita: Wabunge wa Zanzibar wanapokea posho kukaa kwenye vikao ambavyo haviwahusu, mambo ambayo si ya Muungano. Hasara!

  Saba: kuna tofauti za kijamii na kitamaduni kati ya sehemu hizi mbili zinazosababisha maambukizi ya dhana za kijamii ambazo kwetu Bara zinaleta tatizo, na mwishowe utakuja ugaidi kutokea Zanzibar.

  Mfano, Mbunge wa Zanzibar - bora angekuwa wa Bara - Mbunge wa Zanzibar alisimama Bungeni akauliza ni lini Tanganyika itakuja mahakama ya kiislamu. Sasa Zanzibar kuna Mahakama ya Kadhi, Zanzibar is a predominantly Muslim region, ndo maana unaweza kuchoma Kanisa Zanzibar with impunity, bila adhabu, kwa hiyo haina tatizo ukiwa na Mahakama ya Kiislamu kwenye nchi ambayo watu wake ni Waislam anyway. Sasa huku Bara, Mahakama ya Kislamu itakuwepo katika utaratibu gani ambapo nusu ama zaidi ya nusu ya watu ni Wakristo? Hapa kuna tofauti za kijamii ambazo Zanzibar wanataka kuziambukiza Bara. Kwa hiyo, kama ugaidi wa Wahabi extremism utakuja Tanzania, utatokea Zanzibar!

  Nane:Zanzibar haichangii chochote kwenye uchumi wa Tanzania. Zanzibar ina uchumi mdogo kupita wilaya ya Kahama, ndani ya Shinyanga! Na siwalaumu manake hakuna kitu! Sasa, unaniuliza, Mtwara inachangia kwenye uchumi sawa na Shinyanga ambapo kuna Kahama? Na jibu lake ni la hasha, lakini Mtwara wala Mwanza hawajajitangaza kwamba wao ni nchi! Ndio maana hatuulizani huku Bara eti wewe wa Mtwara unachangia nini kulinganisha na Mbeya? Hapana, kwa sababu Mbeya na Mtwara na Shinyanga na Mwanza, yote ni mikoa ya Watanzania! Zanzibar nayo, kwa vile inabebwa, ilibidi iwe mkoa!

  Tisa:
  Zanzibar wanapewa "affirmative action" quotas kwenye nafasi za elimu ya juu pamoja na uongozi. Zanzibar hawana chuo kikuu cha maana, kwa hiyo inabidi kuwatengea nafazi kwenye vyuo vyetu, hali kadhalika kwenye nafasi za uongozi, uwaziri, ubalozi n.k. Kwa hiyo ni raisi zaidi kupata nafasi za elimu na za uongozi ukiwa unatokea Zanzibar. Na hauhitaji elimu za juu saaana kufika mbali kama wewe ni Mzanzibar. Na Mtanganyika ukitaka kupanda ngazi haraka, jifanye Mzanzibar (Jaji Augustino Ramadhani, Rais Mwinyi!) Hii si haki.

  Kumi:
  Wabara na tamaduni zetu na dini zetu hatutakiwi Zanzibar, Zanzibar wanafukuza Watanganyika, wanachoma makanisa, wanachoma visu wenye ma baa ya pombe, which begs the question why give them liquor license in the first place? Unapopewa leseni ya kuanzisha kanisa au ya biashara ya kuuza pombe na unailipia fees zote na kodi ni lazima upate ulinzi na msaada wa serikali. Lakini hakuna anaechukuliwa hatua kwa mateso ya Watanganyika visiwani. Muungano wa nini hapo?

  Kumi na moja: Hakuna kiongozi ama mtu yeyote aliyeko tayari kutuambia faida za Muungano ili tuweze kupima bora ni kipi. Ukiuliza faida za Muungano, unaambiwa sisi na Wanzazibar tuna historia ya udugu. Really? Historia! Sio mustakabali,historia! Wakenya hatuna historia na udugu nao? Angalau Kenya tuna share asili ya "uweusi," Zanzibar wengi asili yao Waarabu! Kama ni udugu tuungane na Kenya basi?! Na kama tuna asili ya udugu na Wazanzibar mbona chokochoko haziishi toka tuungane, kwa nini ni Muungano wa kuvutana? Maana tuna natural connections, udugu, nilitegemea Muungano uwe seamless! Hakuna anaejua faida. Kama huyo hapo juu aliyesema "tutajieni hasara zake na sisi ndio tutataja faida zake..." Kwa nini usitaje faida kwanza kama zipo?


  Kumi na mbili:
  Wazanzibar kwanza ni wanafiki pili hawana shukrani au wanaona hakuna cha kushukuru. Wanafiki kwa sababu hawataki Muungano lakini Tundu Lissu aliposimama bungeni kuu lambast Muungano Wazanzibar wakalia wakamlaani. Ni kama mke ambae hakutaki lakini anaogopa kwenda kuanza maisha mwenyewe! Hawana shukrani kwa sababu Wamejaa Kariakoo, Namanga, Ilala, Buguruni, all over the place wanafanya shughuli zao hakuna anaewaghasi, lakini wao ndio wa kwanza kutu distract na kelele za kutotaka Muungano, sasa kwa nini tuwabebe watu ambao hawaoni wanachohisaniwa? Ni sawa na binadamu na Punda wake. Binadamu anadai shukrani kwa kumtunza Punda, Punda yeye anaona umempandia mgongoni, shukrani ya nini? Anakupiga mateke. Basi haina haja kubebana migongoni wala kupigana mateke, tutengane!

  Kumi na tatu:
  Katika mapendekezo ya marekebisho ya Muungano hakuna structural formulation ambayo ni viable au haipingwi. Serikali moja inapingwa Zanzibar. Hawatakubali yagudu! Serikali tatu sio fiscally feasible, haiwezekani, Tanzania ni nchi ndogo sana kuwa na serikali tatu. Sasa hivi tuna marais na makamu wao watano, na mawaziri wa Bara na Visiwani karibu 80, kwa serikali mbili. Tukiwa na serikali tatu tutakuwa na maraisi kumi na mawaziri mia mbili? Ni mzigo wa gharama. Serikali mbili ndio tutarudi hapa hapa tulipo! Ridiculous.

  Kingine katika mapendekezo ya formulation ya Muungano mpya ambacho hakiwezekaniki, ni kwamba Zanzibar wanataka uhuru zaidi. Wanadai, kwa mfano, autonomy kwenye Mambo ya nje. Kama vile, waingine EA Community kivyao, au FIFA, au OIC, kivyao. Wanataka na mfumo wao wa kodi. Na Benki Kuu. Na Bandari. Na elimu ya juu. Na jeshi pia wanahoji, kwa nini dola yao haina jeshi. Sasa swali, ni je, kama kila kitu tunataka kila mtu awe kivyake, Muungano wa nini sasa? Hahahahaa....

  Kumi na nne: Zanzibar wana Baraza la Wawakilishi, na wana Wabunge Dodoma. Wale wabunge 75 wa Zanzibar pale Dodoma wana ongeza mzigo kwa nchi! Zanzibar ingetosha kuwa na wabunge watano tu! Unguja na Pemba jumla yake inaingia mara tano ndani ya Masasi na Nachingwea! Ambazo ni wilaya ndogo sana ndani ya Mtwara, mkoa mdogo kupita yote Tanganyika ukiondoa Dar-es-Salaam. Mzigo!

  Kumi na tano:
  Tanzania kuna TRA na Zanzibar kuna ZRB. Mbongo ukifanya biashara Zanzibar unakong'otwa kodi TRA na ZRB. Kwa nini kila mtu asiwe na sarafu yake na mambo yake?

  Kumi na sita:
  Zanzibar wana bendera yao, wana Rais wao, wana timu yao ya mpira, wana bunge lao, wana nembo yao. Muungano gani huo wenzetu wana bendera, Tanganyika kwa nini hatuna bendera, hatuna bunge letu, hatuna Rais wetu?

  Kumi na saba:
  Ukikutana na Mzanzibar nchi za nje yeye anaji identify kama Mzanzibar. Lakini kamwe mimi siji identify kama m-Mtwara au Mmakonde. Mtanzania kwanza, umakonde wangu baadae. Hawa Wazanzibaar hawajisikii kama wenzetu, kwa hiyo hata akiwa anatangaza nchi yetu hatawaambiwa watu "Karibuni Tanzania," atasema "Karibuni Zanzibar." Mimi nikiwa nje ya nchi nataka kuwavutia watu siwaambii karibuni Mtwara! Natangaza Tanzania yetu. Wazanzibar hawafanyi hivyo, si wenzetu!

  Kumi na nane: Mzanzibar ana haki ya absentee balot ambayo mimi sina. Kwa nini? Mimi siruhusiwi kupiga kura nikiwa Zanzibar eti nachagua Mbunge wa Bara au Rais, sheria ya Zanzibar hainitambui, sheria ya Zanzibar ime define nani Mzanzibar na nani sio! Lakini Rais Shein alipiga kura yake kugombea Urais wa Zanzibar akiwa Bara, how come? What the ....?! Usawa uko wapi?

  Kumi na tisa: Zanzibar hawataki kugawana potential ya chochote walichonacho. Mtafiti mmoja kawaambia kuna mafuta. Dooooo! Balaa! Ikawa "Hatutaki Muungano! Hatutaki Muungano!" kisa? Mafuta! Potential ya mafuta! Basi waachwe waende zao na mafuta yao na ka nchi kao, tutatua mzigo mkubwa mno.

  Ishirini: HATI YA MUUNGANO IKO WAPI? Kwa nini Muungano umejaa usiri na ukiuliza ******* kizuizini? (Hamad, Jumbe, Doorado n.k.) The only evidence of the union treaty which is being prolmugated ni kiambatanishi kilichowekwa kama adendum kwenye Union Act of 1964, ambacho kilichakachuliwa kabla ya kuchapishwa! The original hati ya Muungano imeteketezwa!

  Hati ina umuhimu gani? Well, kwa sababu Muungano hauna solid legal foundation (Hati ya Muungano wala kura ya maoni wala sheria ya Baraza la Wawakilishi ya kuridhia Muungano) chokochoko zitokanazo hazitaisha, zitaendelea kula national attention ya nchi na kutu distract, kututoa kwenye focus ya mambo muhimu, tunabaki tunaongelea Zanzibar, Muungano, Zanzibar, Muungano kila siku wakati ni sehemu ndogo tu ya Tanzania. Wakati hauna faida yeyote, hasara tupu.

  Hatutaki Muungano.
   
 10. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Taso namba 6,17,1 uko 100% barabara
   
 11. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Well said Comrade Taso nimezingatia hoja zako baadhi zinamashiko makuu baadhi ulizitoa kwa ababu tu unahasira,za matukio ya hivi karibuni kule kisiwan hata mimi sikufurahishwa na hali ile,lakini lilo kuu hapa hoja zako zote zenye makuu kwa mfano "usawa wa kumiliki ardhi,kulipa kodi"na mengine mengi ambayo yakijadiliwa mezani muafaka chanya waweza kufikiwa.Haiwezekani Comrade kila mtu akawa na kila kitu ndo maana yake wale wana mafuta sisi tuna gas hoja hapa ni sera za usimamizi tu

  Comrade kwa nini tusianze kuuzungumzia Muungano kwa kurekebisha kasoro then tuki fail ndipo tuanze kuujadili kuuvunja? Watanganyika na Wazanzibar wapewe arena ya kuujadili Muungano wao tena kweupe kabisa tukishindwa
  kufika muufaka basi kama tuliungana kwa heri kwa nini tutengane kwa shari?
  Hali ilivo sasa kila mtu toka angle yake anajadili kivyake namaanisha wanaoutaka na msioutaka matokeo yake mkikutana
  ni ugomvi,
  tukae pamoja tujadili tutafika tu muufaka,naamin Comrade Taso hata wewe unaamini kwamba kuungana ni jambo jema
   
 12. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wakipewa nafasi ya kuujadili peupe...Ndio hauta vunjika kabisa..kwani naona hakuna hoja ya msingi ingawa ukivunjia ni hatari sana kwa tanzania in term of security...

  Next thing wazanzibar ni wavivu wanataka kutawaliwa all they need muungano uvunjike wapate misaada kutoka nchi za kiarabu..Huyu aliye waambia kuna mafuta ndio kawatibua akili zako kabisa..
   
 13. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  So Comrade Buswelu we need to help our fellow,nawashangaa sana hawa jamaa,kama kuuvunja tutauvunjaje bila kuujadili? kama ukivunjika wanajua kwamba wapemba wote walioko bara watarudi kwao na kuanza taratibu za uhamiaji? vivo hivyo kwa watanganyika walioko kule? au imekaaje hii Comrade
   
 14. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Gwankaja Gwakilingo

  Yaani wakiwa kule kwao hawawazi kuhusu tanzania(Tanganyika) Hawaangalia wenzao ambao wamesha ji establish uku na waishi maisha na kufanya biashara...acha kufanya kazi....kwamba watarudi zanzibar na kuanza kuomba uraia upya tanganyika na sioni kama watapewa kwa kuwa ndio wenzao wanataka uvunjike...

  Sababu za wao kutuhitaji sisi ni kubwa kuliko sie kuwahitaji wao...Hili litawafanya kuona ugumu wa kuvunja muungano...na wengi wanaopinga muungano hawajakaa na kutafakali sana madhara ya kutokuwa nao....wakati mwingine nafakiri upepo huu wa kutaka kuvunjika muungano...ni ule ule unao vuma mombasa ambao na wao wanataka kuwa na jamhuli ya mombasa. Kenya hawawezi itika hilo juu ya mambo ya kiuchumi zaidi...hawana bandari.....Sie wala hatuna tatizo zaidi ya kuwa ni mzigo tu kwa tanzania.

  Hawa wanauamsho watakuwa na mfusukumo toka nchi za kiislam ambazo zenyewe tu zinamatatizo lukuki...kwani baada ya wazanzibar kujitenga kupandikiza kirusi kingine cha upemba, na uunguja kabla hawajajisimamia ni rahisi sana...kama maji ndio wanaona ni mpaka mkubwa sana....
   
 15. T

  Taso JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Kuungana ni jambo jema?

  Gwankaja, nina ombi kwako, kwa heshima na taadhima zote. Kwamba, wewe na mimi na jirani yako mmoja tuhame nyumba zetu wote watatu tukajenge jumba kubwa tuishi na wake zetu, tusomeshe watoto wetu kwa pamoja, na kila mke wa mtu atakuwa ni "jambo la Muungano"! Usiseme mi chizi, wait a second, Muungano si ni jambo jema? Haya, tuungane!

  Unadhani kwa nini shamba la kijiji cha ujamaa lilishindikana kulimwa? Kwa saab shamba la kijiji uliua individual enterprise ya Mtanzania! Soma historia yetu. Point is, sio kila muungano ni jambo jema. Inategemea unaungana 1) katika mazingira na makubaliano gani 2) Kwa manufaa gani? Ingekuwa kila kuungana ni jambo jema USA ingeshaungana na Canada na Europe ingekuwa nchi moja. Kuna wakati kutengana ni better than kuungana. Leo asubuhi kuna bomu limepigwa kanisani northern Nigeria huko, now if you ask me, Nigeria better split into two, Sectarian South and Secural North! This bears repeating, sio kila muungano una manufaa!

  "Tukae mezani tuzungumze, turekebishe kasoro, tufikie muafaka chanya..." mara ngapi? Kaka, unajua Rais Kikwete aliunda "Wizara ya Kukaa Mezani Kuzungumza Kurekebisha Kasoro za Muungano Kufikia Muafaka Chanya"!? Unaijua hiyo wizara? Yako wapi? Ndugu, watu hawajaanza "kukaa kuzungumza" leo wala jana. Wakina Abdu Jumbe washafukuzwa Zanzibar early 80's huko kwa kuzungumzia kurekebisha Muungano, kina Hamad, wote hao.

  Hizo "kasoro" za Muungano, the biggest kasoro iliyopo hamtaki tuiguse kwenye mazungumzo! Kasoro yenyewe ni kwamba watu hawajawahi - na hairuhusiwi - kuulizwa kama 1) wanataka kuungana 2) kama wanataka, kivipi?
   
 16. Ipyanah

  Ipyanah Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Once people enter into the marriage instution, they are meant to beleive it will last forever, if not fight it does so, well thats my beleive in marriage.
  Even after oil discoveries in Zanzibar, if we let it go sooner or later Mtwara would want to be its own state, then eventually Morogoro will claim sisal can enable them to run on their own.

  However, Taso, not that i disagree with all the 20 excuses we need to know and weigh not necessarily appreciate reasons, as to why Zanzibar itself is far more importatnt attached to the mainland. Surely, you do believe there must be a reason/reason's that withhold this "marriage".
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Nadhani una point nzuri sana lakini nakupata kwa mbaaali sana, unaweza kunirahisishia kidogo Kiingereza hicho?


   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Unajua kuna watu wanasema na kuomba kitu wasichokijua...angalia wapiga kelele wengi wanaotaka muungano uvunjwe...wanakaa Dar na kuendesha siasa Zenj. Ngoja uvunjike wataona.
   
 19. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Hao Uamsho wanaweza kuwa wanatumika bila wao kujijua kwa sababu ya ufinyu wa uelewa. Mimi ninahisi watu kama Maalim Seif Sharif Hamad wanaweza kuwa nyuma ya hizo vuguvugu. Nia ni kuirudisha Zanzibar kwenye pre-revolution era. Maana yake ni kufuta kabisa malengo na mafanikio ya Mapinduzi. Bahati mbaya hata viongozi wengine wa SUK kutoka pande zote mbili wanashabikia wasichokijua. Wakija kutambua itakuwa too late. Usicheze na madevu anatekele strategy yake hatua kwa hatua. Hatua ya kwanza ilikuwa kuingia serikalini, ya pili ni kuvunja Muungano, ya tatu itakuwa CUF kuwa na serikali isiyo ya umoja na baada ya hapo anaweza kufanya atakavyo kwa kuwa hatakuwa na wa kumzuia. Je, inakushangaza kuona kuwa viongozi wa harakati za kuvunja Muungano ni wale wenye asili ya Kiarabu kama akina Salehe, Ahmed Rajab, Jusa, Hamad mwenywe,nk? Hawa (familia zao) kabla ya mapinduzi ndo walikuwa Hizbu.
   
Loading...