Muungano: Udhaifu unatitia, ufa unapanuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano: Udhaifu unatitia, ufa unapanuka

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Oct 15, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Oct 15, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi, mara nyingi tumeongelea muungano na madhaifu yanayotishia hatma yake

  Kwa hali na mwelekeo uliopo ipo haja ya kuzungumzia tena na tena ili wakati ukifika tusijejiuliza maswali yenye majibu leo hii

  Tatizo la muungano ni la muda mrefu likijitokeza kwa namna tofauti kila mara

  Katika uhai wa muungano, nchi hii haijaongozwa na chama kingine zaid ya CCM

  Ilitegemewa, kwa uzoefu mengi ya matatizo yangepatiwa ufumbuzi.

  Kinyume chake udhaifu unatitia, ufa unapanuka na hatma yenye mashaka ni dhahiri

  Serikali na chama tawala wanatafuta majibu , haionekani kama wamepata lolote

  Kinachojitokeza ni majibu yanayokoleza hoja zinazodhoofisha muungano kila siku

  Chama na serikali yake inaamini muungano ni 'mali yao' na wana haki ya kuulinda kwa nguvu na maguvu wakitumia mbinu zile zile zilizochoka na kuchokwa

  Kwa dhana ya kulinda muungano kwa nguvu, kauli za kutisha zimekuwa utamaduni.

  Mbinu za kuunda tume na kamati zinatumika kila mara ingawa yapata tume Zaidi ya 7 hazikutoa majibu na sasa ipo nyingine inayochochea udhaifu wa muungano

  Yapo maswali wasiyojiuliza viongozi wa chama na serikali zake za awamu tano

  1. Je, muungano ni mali ya CCM au ni mali ya wananchi?
  2. Je, ipo ridhaa ya wananchi wa pande zote kuhusu muungano?
  4.Je, muungano unalindwa na wananchi au maguvu kwa kutumia dola?
  5. Kwanini kwa miaka 50 na utawala wa chama kile kile matatizo yanaendelea?
  6.Ni wapi duniani muungano umehodhiwa na viongozi, umelindwa kwa nguvu?

  Tutakuwa na mabandiko endelevu tukichagizwa na kile kilichoitwa 'kutatuliwa kwa kero za muungano kutoka kamati ya pande mbili za chama na serikali moja''

  Kamati iliyotoa hoja zinazohitaji fikra na zinazoonyesha unyonge na udhaifu wa muungano

  Sehemu ya I inafuata
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Oct 15, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya I

  Miaka 50, muungano umepitia matatizo tofauti. Hakuna nyakati umekuwa na tatizo la aina moja.

  Inatosha kusema, matatizo ya muungano yanabadilika kutokana na nyakati

  Mengi ya malalamiko yanatoka upande wa Zanzibar na yamejengewa hoja tata kila mara

  Ukiwauliza Wazanibar ni nini hasa tatizo lao katika muungano, sababu zinazotolewa zinahitaji ''tafakuri''

  Kwa muda mrefu 'Watanganyika' wamekuwa kimya, kadri muda unavyosonga malalamiko ya Wznz yameamsha udadisi (curiosity) miongoni mwao. Hilo limeibua mambo mengi yaliyokuwa hayajulikani

  Ni kutokana na hali hiyo, kizazi cha leo ambacho sehemu kubwa kina weledi na sehemu nyingine hakina uvumilivu kimeweka hali ya muungano katika wakati mgumu kuliko nyakati zilizopita

  Kwa hili, Watanganyika wawashukur Wznz kwani hawakujua mengi ya yale waliyosingiziwa.
  Hawakujua gharama za muungano na uzito walioubeba.Hawakujua fadhila zenye ujira wa karaha

  Hilo lililazimu uwepo wa katiba mpya itakayoangalia masilahi ya pande zote kwa haki na usawa.

  TUME YA WARIOBA
  Tume haikulenga kuwa mworabaini wa matatizo, ililenga kutengeneza mazingira ambayo matatizo yatakayojitokeza kutokana na mbadiliko ya nyakati yawe na 'kitako' au template ya kuyashughulikia

  Katika tume, kamati n.k. vilivyowahi kuundwa kushughulikia muungano, ni ya Jaji Warioba iliyosimamia uandikaji wa katiba ambayo imekuja na sababu za msingi kabisa kutoka kwa wananchi kuhusu malalamiko ya muungano

  Tume na majibu
  Tume ya Jaji Warioba ilikuja na majibu ya maswali tuliyoorodhesha bandiko la 1

  Kwanza, tume ilibaini kuwa muungano si mali ya CCM na wala CCM haina hati maliki.
  Muungano unatokana na wananchi kutokana na sababu za kiasili, kiutamaduni, kijiografia na kijamii

  Pili,tume ilibaini kuwa kuna ridhaa ya wananchi wa pande mbili licha ya ukweli utihibitisha kwa kura.
  Hata hivyo, kwa kutumia mantiki, maoni , hekima na busara tume ilibaini Wzn wanataka muungano kwa asilimia kubwa. Walichodai ni muundo wa muungano

  Pamoja na maoni ya tume, ni ukweli Wazanzibar wa chama tawala au upinzani hakuna anayejitokeza na hoja ya kuvunja muungano. Wote wanasema kwa kauli zao wanautaka

  Tume ya Jaji ilibaini malalamiko si kwa Wzn tu, Tanganyika wanayo kiuhalisia ni zao la malalamiko ya Wznr.

  Tatu, Tume iliona ni vema wananchi wakasikilizwa,ndio wenye muungano si dola.
  Katika hilo tume ikatoa maoni ya wananchi kama ilivyoyakusanya

  Nne, tume ikabaini kuunda tume na kamati hazitoi majibu. Muungano ujadiliwe katika katiba.

  Kwamba, yatakayokubali yazingatiwe kisheria na si kamati zisizo na nguvu za kisheria bali za kutengeneza mapendekezo ima kufurahisha au kupendeza baadhi ya watu au sehemu ya muungano

  Tano,Kwamba, matatizo ya miaka 50 yanatokana na kufanya mambo kienyeji na chini ya uvungu au uani

  Mwisho, tume ilibaini muungano ni mali ya wananchi na hakuna mahali duniani viongozi wamepewa uhodhi

  Haishangazi, kwavile CCM wanadhani wana hati miliki, bunge la katiba klikavurugwa ili watengeneze muungano na kuulinda kwa kutumia mbinu zile zile chafu zilizochakaa.

  Wameunda kamati chini ya ofisi ya makamu wa Rais wa JMT na Wizara ya muungano ya Mh J.Makamba

  Makosa yaliyofanyika huko nyuma, yanaendelea kufanywa, tena kwa ubaya na kuchochea hisia mbaya dhidi ya muungano. Hili ndilo tutajadili sehemu inayofuata kwa mmaamuzi yaliyotolewa hivi karibuni

  Inaendelea
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Oct 15, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya II

  KAMATI YA KERO ZA MUUNGANO YA AWAMU YA TANO

  Kwa kutishika na maoni ya tume ya Warioba, CCM wameharakisha kuunda tume wanayosema ni kero

  Hii ni katika dhana ya kwamba CCM inahodhi muungano, ni mali ya viongozi na unalindwa kwa nguvu

  Tukiwa hatujui ni lini mchakato wa katiba utaanza tena, ulazima wa tume hii ya kero ni wa nini?

  Tume hii imeundwa na viongozi wa serikali.CCM. Hili linathibitisha hoja ya CCM kudhani haki wanayo, na kwamba viongozi ndio wamiliki wa muungano kwa uwezo walio nao kiutawala

  Maswali Zaidi yanaibuka, ni nani amesema kero za muungano ni za Wznz peke yao?

  Nani atawaongelea Watanganyika ambao kiuhalisia Wznz wanaingia katika maamuzi yao?

  Je, suluhu ya ZNZ pekee itatoa majibu ya matatizo ya muungano?

  Nani amewapa wznz haki ya kuamua nini wanataka kiwe na nini kisiwe katika muungano?

  Je, kamati hii ipo kisheria na maamuzi yake yataingiaje katika sheria mama ya nchi?

  Nani alikuwa mwakilishi wa Watanganyika katika kamati hiyo na alipatikana kwa utaratibu gani?

  Tukiangalia kamati ya kero ambayo kwa minajili ya mjadala huu tutaipa heshima ya 'Kamati ya Makamba' kuna mengi yanayojitokeza kwa ubaya na ambayo mbele ya safari yataweza kudhoofisha kama si kuua muungano

  Awamu ya nne, ilifanya makosa ya kuruhusu Wznz kufanya maamuzi ya mambo ya muungano peke yao.

  Tumeona matatizo makubwa ya ukiukwaji wa katiba ya JMT na ile ya SMZ zinavyosomeka tofauti.

  Makosa hayo tultegemea yawe funzo, kinyume chake ''Kamati ya Makamba'' kwanza imeyarudia kwa kiwango cha juu, pili imezidisha ugumu wa baadhi ya masuala yanayotokana na hali ya kuacha ZNZ iamue inachotaka

  Maamuzi ya tume ya Makamba yamezingatia kuwafurahisha Wznz bila kujali madhara yake si za usoni

  Tunaweza kusema kwa uhakika kabisa, 'Kamati ya J.Makamba' imechagiza na kuamsha hisia kuliko majibu

  Tutaangalia matokeo ya maamuzi matatu yaliyofanywa na athari zake kwa undani

  Inaendelea
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya III

  ''KAMATI YA MAKAMBA''

  Tunaiita kamati ya makamba kwasababu inashughuikiwa na Mh Makamba

  Mara zote ametoa taarifa ya maendeleo bungeni au mikutano ya siasa kama alivyosema akiwa Zna karibuni

  Hii ni kamati iiyoundwa na serikali ya chama tawaa chini ya ofisi ya Makamu wa Rais

  Makamu wa Rais Mzanzibar, kwa sehemu kubwa ndio wenye malalamiko. Hii tu linaleta fikra

  HESABU ZA KISIASA

  Kabla hatujajadili kazi ya kamati, tujadili kwa uchache hesabu za kisiasa katika jambo hili

  Zipo sababu kuu mbili, sababu za muda mfupi na za haraka, na hesabu za muda mrefu

  MUDA MFUPI

  Kuharakisha ''utatuzi''kumelenga kuondoa hoja ya 'kero' maandalizi ya katiba pendekezwa ya CCM yakiendelea.

  Hili litasaidia kupunguza malalamiko ya wznz kwamba kero zimeshughulikiwa

  Harakati hizi ni katika kuonyesha kuwa serikali mbili hazina matatizo na zinakubalika, ndiyo hoja!

  Kwamba hakuna sababu ya kuwa na serikali tatu

  Pili, kwa hali ya siasa Znz kinachofanyika ni kutoa rasilimali kusaidia miradi ili kurudisha Imani ya wazanzibar kuwa CCM bado inafanya mambo 'makubwa' Kwa hali ya kiuchumi linafanyika makusudi ili kunyesha 'wanaweza'

  HESABU ZA MUDA MREFU
  Kwanza, kujenga Imani ya CCM kwa Wznz ambayo ilipelekea kutweka kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita

  Pili, baadhi ya viongozi wenye malengo ya kisiasa kwa muda mrefu, wanalitumia hili ili kutafuta umaarufu na kuungwa mkono na Wznz. Baadhi ya wana kamati hiyo waliwahi kugombea nafasi za Urais

  Tatu, ni kutaka kumaliza hoja za muungano kabisa si kwa nia ya suluhu bali 'kufunika' matatizo chini ya kapeti

  Hizi kwa mtazamo ndizo hesabu za CCM/Serikali bila kujali matatizo yatakayojitokeza siku za mbeleni

  Ni hesabu kama za Rais JK aliyeacha wznz wakiuke katiba ya muungano kwasababu za kisiasa zisizozingatia matokeo ya muda mrefu. Haiukuchukua muda matatizo yalijitokeza muda mfupi sana

  Hali imejirudia tena pale Baraza la wawakilishi lilippitisha sharia ya kutoza kodi bidhaa zinazoingia kutoka Bara

  Inaendelea...
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya IV

  KWANINI HESABU ZA ''KAMATI YA MAKAMBA'' ZINA MATATIZO?

  Hesabu za kisiasa katika bandiko la III hazitoi majibu ya matatizo ya muungano.

  Kwa upande mwingine hesabu hizo zinachangia sana kuamsha hisia kwa Watanganyika

  Inaonekana hoja za Watanganyika hazifanyiwi kazi
  Wznz wamepewa uwezo mkubwa wa kuamua nini wanataka kiwe na nini wanataka kupata kutoka muungano

  Hoja inayzunguka vichwani mwa watu wa Bara ni kuwa kwanini ZNZ ipewe uwezo wa kuamua inachotaka

  Haya ndiyo yaliyozua ile hoja ya G55 baada ya ZNZ kwenda 'solo'. Historia inajirudia kwa mlango mwingine

  Hoja nyingine ni hisia kuwa Watanganyika wanabeba mzigo mzito wa muungano na sasa wa SMZ

  Wasichoambiwa ni kuwa kipi ambacho ZNZ inatendewa kinyume katika muungano?

  Ni nini mchango wa ZNZ katika muungano?
  Na kwanini waamue wanachotaka ikiwa ni pamoja na rasilimali zisizo wahusu wao wakihdhi zao?

  HOJA ZA KAMATI YA MAKAMBA

  1. Mh Makamba alikaririwa siku za nyuma akisema ZNZ inapata 4.5% na bilini 29 zilishatolewa mwanzoni mwa mwaka huu na utaratibu huo utaendelea na budge support ya SMZ imeshatolewa

  Hizi wanasema ni mtaji wa asilimia 11 wa Bank ya ZNZ. Kwa hesabu za kawaida, kodi zinazokusanywa Tanganyika asilimia 4.5 uinakwenda ZNZ.

  Hicho ni kiasi kikubwa sana pengine afadhali hesabu zingepigwa wapewe sehemu iliybaki wawe na bank yao

  2. WZNZ waamua kutoza kodi bidhaa zinazoingia kutoka bara
  Hili ni haki yao kama wanaamua kuwa sisi ni sehemu mbili tofauti.

  Lengo la ZNZ ni kuhakikisha wanakusanya kodi kwa ajili ya SMZ na si kwa ajili ya JMT.

  Wazanzibar hao hao wanalalamika kuwa magari yanayoingizwa bara kutoka ZNZ yanatozwa kodi katika nchi moja. Kwamba, wanapotaka fursa za muungano sisi ni wamoja, wanapotaka fursa zao ni nchi mbili

  Awamu ya tatu iliwahi kujaribu kuruhusu magari kuingizwa. Kilichotokea ni SMZ kutoza kodi kidogo, kuacha mianya ya kuingiza magari hovyo na kuyaingiza bara bila kodi. Mpango huo ukafutwa kutokana na 'abuse'

  Kamati ya Makamba imeruhusu magari yaingizwe kutoka ZNZ kama sehemu ya nchi moja, ingawa WZN hao hao wanaodai nchi moja hawataki bidhaa ziingie ZNZ kutoka bara kama nchi moja

  Ni ZNZ ambayo leseni ya udereva haikubaliki hadi uwe na ya ZNZ katika nchi moja kama wasemavyo

  Hili ni jambo baya kwasababu lengo lake ni kutaka kutumia ZNZ kama mwanya wa kuingiza bidhaa bara huku Bara ikiwa haipati mapato yoyote. Kwa upande mwingine akina Makamba wamekubali bara wawe 'losers'

  3. TRA
  Kamati imeamua mapato ya TRA ZNZ yabaki huko. Cha kushangaza, wafanyakazi wa TRA ZNZ wtalipwa na JMT.

  Kwamba walipa kodi wa Tanganyika watalipa wafanyakazi wa kukusanya kodi ya SMZ

  Lakini pia kuna maswali. Ikiwa ZNZ ina TRA yake, mbona hatuelezwi mchango wake katika muungano ni upi?

  Tunajua muungano na mambo yote ni mzigo alioubeba Mtanganyika
  Kama ZNZ inapewa uwezo huo kwanini wasipewa majukumu yao wayatimize kwa kodi zao?

  Inaendelea...
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya VI

  TRA
  Kwa vile BLW limeamua kutoza kodi bidhaa kutoka bara, na mapato ya TRA kubaki huko, ni vema

  1. Zanzibar ikachukua majukumu yake kama serikali bila kupitisha mzigo huo kwa mlipa kodi wa Tanganyika

  2. Kamati ya Makamba iweke wazi mchango wa SMZ katika kuendesha muungano

  3. Wafanyakazi wa SMZ wakiwemo wa TRA ZNZ walipwe kwa malipo ya TRA ZNZ yasiyoingia muungano

  4. ZNZ ichukue jukumu la kuhudumia wabunge wakewanaokuja Dodoma

  5. Mapato ya rasilimali za bara yatengwe ili rasilimali zisizo za muungano zitumike eneo husika

  Mapato ya gesi yanayoingia muungano yanatoa 4.5% inayokwenda ZNZ, ZNZ wameamua si jambo la muungano.

  Kama wao wana mafuta na gesi yao, kwanini ya bara iende huko kwa kupitia 4.5%?

  6. ZNZ isipewe budget support kutoka bara.
  Ina uwezo wa kukusanya kodi zake zikabaki huko, ina uwezo wa kukopa nje ya nchi bila kutumia JMT

  7. ZNZ inapokopa nje ya nchi mzigo huo usipitishwe kwa udhamini wa JMT ambayo ni Tanganyika yenyewe

  8. ZNZ idhamini wanafunzi wake bila kutumia taasisi za muungano.

  Kama ZEHSLB inapata rasilimali kutoka SMZ inayokusanya kodi yake na kukopa yenyewe, kwanini mzigo wa wanafunzi wa ZNZ aubebe Mtanganyika?

  10. Wafanyakazi wa muungano wanaotoka ZNZ kwa asilimia 21 wahudumiwe na SMZ.

  11. ZNZ ichukue jukumu la kulipa bill zake kama za umeme, bila kutwisha mzigo Tanganyika

  Hakuna maana wafanyakazi wa muungano wanaopatikana kwa Uzanzibar walipwe kwa kodi za Mtanganyika

  Haya yanatokana na ukweli kuwa kamati ya Makamba haijaonyesha ZNZ inachangia nini katika muungano

  Maswali na hoja kama hizi zinazunguka katika vichwa vya wananchi wa pande zote kwa mitazamo tofauti

  1. Watanganyika wakiona kudharauliwa, na kubebeshwa mzigo wa Muungano na kuendesha SMZ
  2. Wazanzibar wakiona wana haki Zaidi katika muungano na uwezo wa kuamua nini wanataka
  3. Baadhi ya Wznz wakiona nchi yao inakuwa tegemezi na kumezwa, huenda ikapoteza identity

  Inaendelea...
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  NINI HASA HOJA ZA WATANGANYIKA?

  Bandiko lililotangulia tumeeleza kuhusu hoja na mitazamo ya watu kwa pande zote. Tuzipitie kwa uchache

  Watanganyika
  Wana hoja ya kuhdarauliwa. Kitendo cha Wazanzibar kuamua wanachotaka kupitia serikali au bunge lao bila kujali upande wa muungano kwa mambo ya muungano ni dharau iliyokubuhu

  Tukiwa ''nchi moja'' kwa baadhi ya nyakati na nchi mbili kwa wakati mwingine, tuna nyaraka moja inayotusimamia katika muungano, Katiba. Katiba zote mbili ya JMT na SMZ zimezungumzia mambo yanayohusu muungano

  Pande zote zinapaswa kuheshimu katiba bila kujali mambo mengine
  Wazanzibar kama ilivyokuwa 2010 wameendelea na ubabe wa kujipa haki ya ukuu katika muungano

  Jambo hili linawaudhi na kuwakera Watanganyika ambao kwa uhalisia pengine wangekuwa na ukuu huo

  Pili, Watanganyika wanajiuliza kwanini ZNZ isitumie rasilimali zake katika kutekeleza mipango yake?

  Tatu, kwanini rasilimali za Tanganyika ni za wote kwa maana ya muungano, na za ZNZ ni zao wenyewe?
  Iweje mapato ya gesi ya Mtwara, yatoe gawawio kwa ZNZ ambayo haitaki suala hilo liwe la muungano?

  Kwanini vyanzo vya ajira view vya muungano, wakati ZNZ ikipiga marufuku suala hilo kwa Watanganyika?
  Yanapokuwepo masharti ya 'Znz ID' ni ubaguzi katika nchi ile ile wanayosema ni moja penye mahitaji

  Kwanini kodi za Tanganyika ambazo ni tozo kwa Watanganyika, zitumike ZNZ kwa budget support?

  Kwanini ZNZ ipewe 4.5% ikiwa haina gharama zozote zile za kuendesha muungano?
  Wizara ya ulinzi, mambo ya ndani, nje na zile za muungano zinachangiwaje na ZNZ?

  Kubeba Mzigo
  Ikiwa ZNZ ina vyanzo vya mapato iweje gharama za baadhi ya taasisi zilipwe na muungano?
  Katika kuendesha muungano, wapi mchango wa ZNZ unapoonekana ambao pengine hatuujui?

  Kwa uchache huo, suala linalojitokeza ni Tanganyika kubeba mzigo wa muungan peke yake, na sasa inabeba mzigo mwingine wa kuendesha SMZ. Kulipa mishahara ya TRA ya ZNZ kwa makusanyo ya ZNZ ni mfano mzuri

  Hayo na mengine yakiwekwa pamoja na Watanganyika ambao wana nguvu ya kweli katika muungano hilo ni sawa na kuweka 'rehani' muungano huu. Siku Watakaposimama kuhoji kukiwa hakuna majibu, itakuwa ngumu

  Penye matatizo watu husikilizwa, yanazungumzwa na kumalizwa. Kamati ya Makamba haikusikiliza hoja za Watanganyika. Ilichofanya ni kutafuta njia za kuwafariji wznz na matamanio ya kisiasa siku za usoni

  Kama sivyo hivyo, kamati ya Makamba itueleze, ukuu wa znz katika muungano, mchango wa znz katika muungano, dhararu za znz katika muungano, matumizi ya rasilimali za Tanganyika katika muungano yametetewa na nani, yamesikilizwa vipi na yametoa majibu gani.

  Inaendelea....
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  HOJA ZA WAZANZIBAR
  Bandiko la VI tumeeleza hali ya Wznz kuona wanayo haki kubwa ndani ya muungano kuliko wenzao

  Pengine ni kwasababu ya kuwakuwa na vyombo vyao kama BLW

  Hata hivyo, vitendo vya kuchukua maamuzi kana kwamba wana haki ya muungano peke yao si sahihi

  Pale Wznz wanapochukua maamuzi ya nchi yao, maamuzi hayo yasiathiri upande wa pili

  Kwa mfano, kamati ya Makamba imeamua magari kutoka ZNZ yaingie tu Tanzania bara kama 'nchi moja'

  Hili linaathiri kwa Tanzania bara kwasababu ZNZ itakuwa uchochoro wa kukwepa kodi kama ilivyowahi tokea

  Pili, Tanzania bara ina taasisi ya viwango (TBS) kutathmini bidhaa na mali zinazoingia nchini kwa ubora/viwango

  TBS ina taratibu zake ikiwemo wa ukaguzi wa magari kabla hayajaingia nchini.

  Vipo vigezo vya kufikiwa katika viwango ikiwemo 'umri wa gari' n.k.
  Haya ni katika kulinda masilahi na usalama wa Tanzania bara

  Zanzibar wana ZBS ambayo haijulikani ilianzishwa kwanini ikiwa sisi 'ni nchi moja' kwa mujibu wa Waznz
  ZBS inaweza kuwa na vigezo vyake ambavyo havikidhi vigezo vya TBS

  Kamati ya Makamba haikuona matatizo yanayoweza kujitokeza kwani TBS itakuwa imefungwa mikono na maamuzi ya wanasiasa wachache walioamua tu magari yaingie kutoka popote

  Muda si mrefu tutaanza kuona mgari ya miaka 20 au 30 yakiingizwa kutoka Zanzibar, wakati huo huo sharia ikizuia Watanzania bara kuingiza magari Zaidi ya miaka 10. Haya ndiyo maamuzi ya WZNZ yanayathiri Tz bara

  Tatizo jingine la maamuzi ya Wznz ni kuamua kubakiza makusanyo ya TRA huko kwao.
  Hilo si kosa . Kosa ni Wznz wanaposhinikiza wafanyakazi wa TRA yao walipwe kwa kodi kutoka Tanzania bara

  Kamati ya Makamba imeridhika kwa dhati kuwa kuna haki ya ZNZ kukusanya mapato yao, na ni haki ya makusanyo ya Morogoro, Mtwara, Kigoma n.k. kulipa mishahara ya wafanyakazi wa ZNZ-TRA

  Hoja ni kuwa ZNZ wnapofanya maamuzi yao,wasimamie maamuzi hayo kwa gharama zao

  Ni makosa kufanya maamuzi yanayotuathiri Tz bara licha ya uzito wa mizigo iliyobeba

  Hili linaeleza dhana ya haki na ukuu wa Wazanzibar katika muungano kwa kudhani wanayo haki ya kutaka na kupata chochote kwa hoja za kubabaisha za kero.

  Dhana ya kwamba wznz wanapohitaji 'tunakuwa nchi moja' nje ya hapo ni nchi mbili ni ya hatari

  Inaendelea...
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Oct 17, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  HOJA YA WZNZ

  Ni kutoka bandiko VI, kwamba wapo wznz wanaoona utegemezi unapoteza ID ya ZNZ

  Katika mambo yanayozungumzwa na wznz ni kuhusu identity, yaani utaifa wao.

  Ni moja yanayochagiza kuchagua serikali 3. Wanadhani ZNZ inapoteza ID na kuwa Tanzania

  Wznz hajitambulisha kwa Utanzania ispokuwa pale tu Utanzania utakapokuwa na manufaa.

  Maamuzi ya kamati kama ya Makamba yanapokelewa na baadhi kama faraja hasa wale wanaonufaika na fursa wazipatazo iwe kwa misaada , mafao n.k. kutoka JMT

  Kwa mfano, wabunge, mawaziri, na viongozi wa juu wote watafurahia kupata misaada, kukwepa majukumu ya muungano n.k. ili waendelee kudumu na vizazi vyao kwa raha

  Kwa upande mwingine, utegemezi unaangaliwa na kundi jingine kama njia ya kupoteza Identity
  ID haijengwi kwa majina, au taasisi tu bali uwezo wa Taifa kuamua na kupanga.

  Hofu inayolikumba kundi hili la wznz ni nchi imekuwa tegemezi tu ndani ya muungano.
  Imefika mahali uchumi mzima unaendeshwa kwa utegemezi na hilo linawanyang'anya wznz nguvu(bargain)

  Miaka ya 1970 na 1980 znz ilikuwa na nguvu za uchumi ikititishia kuvunja muungano kila mara.

  Nguvu za kiuchumi hasa wa karafuu na biashara zilipoanguka, wznz haina tena hoja ya kuvunja muungano.
  Wana hoja ya muundo wa muungano

  Waliotaka muundo wa serikali 3 walikuwa na hoja hiyo, kwanza ya Identity na pili kujiwezesha
  Kwa namna nyingine kundi la wahafidhina limeamua kuishi kwa utegemezi kila siku

  Tendo la kuomba favor, kutochangia muungano zinaondoa ile ''bargaining power''

  Kwa maamuzi ya 'kufaraji' kama ya kamati ya Makamba, ipo siku Watanganyika watayaona haya kwa jicho la pili na kwavile wana nguvu wata dictate terms.

  Pengine litakuwa jambo zuri kwani tutaelekea nchi moja serikali moja, znz ikiwa ni sehemu tu kama ilivyo mikoa mingine

  Inaendelea
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Nov 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  MAAMUZI HAYA SASA YANACHOSHA

  NANI KAIPA ZNZ MAMLAKA ZAIDI JUU YA MUUNGANO?

  Jana Rais wa znz amesaini mswada unaodai mafuta na gesi si mambo ya muungano

  Kwa mujibu wa katibaJMT 1997, nyongeza ya kwanza, namba 15 inasema

  '15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia'

  Kama ilivyokuwa 2010 jambo hili limefanyika kupitia BLW na kusainiwa na Rais wa ZN

  Hatuna tatizo na znz kumiliki rasilimali zake. Tuna tatizika na taratibu zinazotumika kufikia hilo

  Kuondoa jambo la muungano, huku likisomeka tofauti katika katiba mbili ni dharau

  Hili linaonekana kwamba, ZNZ ina mamlaka makubwa juu ya muungano kwa kufanya inachotaka

  ZNZ inayotaka rasilimali zake zitumike huko, inatumia rasilimali za Tanganyika kwa kivuli cha muungano.

  Kuna mifano hapa kwa uchache

  1. Mafuta au gesi na mapato yatakayopatikana Tanganyika, yataingia katika mfuko wa JMT

  Mfuko huo ndio unaotoa 4% kwenda ZNZ kwa hoja ya hisa za BOT zikiwemo kodi za Watanganyika.

  Kwa maneno mengine ongezeko la pato la Tanganyika ni neema isiyo na jasho kwa ZNZ

  2. ZNZ yenye choyo ndiyo inayopata bajeti sapoti kutoka Tanzania ambayo basically ni Tanganyika

  Tunaelewa, kwa takwimu na kwa mujibu wa BoT, znz haina mchango katika muungano

  3. Rasilimali za Tanganyika zimekuwa sehemu ya muungano.
  Madeni ya ZNZ yanalipwa na JMT mbayo kwa mchango wake ni Tanganyika pekee

  4. Gharama za kuendesha shughuli za muungano, zinatokana na rasilimali za Tanganyika

  Hii maana yake rasilimali zetu zinazogharamia muungano ni rasilimali za Tanganyika pekee

  5. Gharama za taasisi kama HESLB ambako Watanganyika wenye rasilimali zao na walipa kodi wanabanwa kurudisha mikopo, kwa ZNZ wanafunzi wake hawatakiwi kurudisha mikopo isipokuwa ZHESLB

  Mifano hii michache sana inaonyesha jinsi rasilimali za Tanganyika zinavyotumiwa na ZNZ ingawa ZNZ haipo tayari kwa rasilimali zake kutumika katika muungano.

  Hili ni tatizo ambalo Tume ya Warioba ililiona, na kuamua iwepo Tanganyika ili kuwe na haki na usawa, na kusiwepo 'kuviziana' kusiko na faida kwa pande zozote za muungano

  Inaendelea
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Nov 16, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  MAAMUZI YANACHOSHA

  Inaendelea..

  Kwavile ZNZ inataka kutumia rasilimali zake, hakuna sababu ya kuwa kikwazo.
  Hata hivyo ipo sababu ya ZNZ kuonyesha mchango wake katika muungano

  Tunashauri haya yafanyike kwasababu Watanganyika tumechoka kuona jeuri na dharau ya aina hii

  1. ZNZ ihudumie taasisi zake. Kwamba Wabunge wake waondolewe katika payroll ya kodi za Tanganyika

  2. BLW ZNZ lipitishwe mswada wa kuondoa Elimu ya juu katika mambo ya muungano

  3. BLW lipitishe mswada wa kuondoa ulazima wa ZNZ kupata udhamini wa JMT wakati ikikopa nje

  4. SMZ ichukue dhamana ya mishahara ya watumishi wa muungano wanaofanya kazi ZNZ

  5. SMZ ihudumie taasisi zake zenye sura za muungano ambazo zinalipiwa na muungano

  6. Ardhi isiwe suala la muungano ili znz iweze kumiliki rasilimali zake za ardhini bila kikwazo

  7. Ajira zisizo za muungano ziondolewe kwa Wazanzibar ili Watanganyika wanufaike kama ZNZ

  8. Madeni ya ndani ya ZNZ yalipwe na SMZ kwa kutumia rasilimali zake

  9. Baraza la mitihani na mitaala ya elimu isiwe jambo la muungano tena

  Orodha inaendelea.

  Muhimu ni Tanganyika iwe na utaratibu wa kuratibu mambo yake bila kuingiliwa na ZN

  1. Wabunge wa ZNZ wasijihusishe na kamati zisizo za muungano kama rasilimali na nishati

  2. Wabunge wa ZNZ wasichangie hoja za railimali za Tanganyika, na wasishiriki mijadala

  3. Shughuli zisizo za muungano zitengenezewe utaratibu usio washirikisha Wazanzibar

  4. Masuala kama bajeti sapoti yawe misaaada na si sharti kama ilivyo sasa

  5. ZNZ ipewe hisa zake kwa kuangalia gharama za muungano na mchango wake

  6. Mgao wa asilimia 4 ukiwepo,uzingatie pato la BoT na si rasilimali za Tanganyika

  7. Tanganyika ipewe nafasi ya kuamua hatma ya mambo yake

  Kwa hali ilivyo, tunakokwenda hali ya muungano ni mbaya sana.

  Kunapotokea muungano unabebwa na mmoja, dharau upande mwingine,inaudhi

  Ni wakati wabunge wa Tanganyika, wasimamie na kutetea rasilimali za nchi yao

  Hali iliyopo ya uchoyo na umimi huku 'chako ni chetu changu ni changu' inakosa uvumilivu

  Na kwa upande wa ZNZ, hakuna haja ya kufanya mambo nusu nusu.

  Ni wakati sasa watumie BLW kuitisha mswada wa kura ya maoni

  Tusemezane
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Nov 17, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  KATIBA YA NCHI

  'DOUBLE STD'

  Umekuwa ni utamaduni Zanzibar kuchukua maamuzi yasiyojali au kuzingatia katiba ya JMT

  Tunasema haya kwasababu jambo lililorodheshwa katika katiba ya JMT linaathiri pande mbili

  Hata yale yaliyopo katika katiba ya SMZ, yapo yanayoingiliana na katiba ya JMT

  Matatizo yaliyotokea 2010,ZNZ kwenda solo katika mabadiliko ya katiba hayaonekani kuwa somo

  Ukisoma katiba ya JMT na ya SMZ kuna mambo yanayotofautiana bila ulinganifu

  Hii ina maana ZNZ imepewa au inajipa haki ya maamuzi yanayoathiri JMT

  Hatuna tatizo na maamuzi yanayohusiana na ZNZ, tuna tatizo na kuchezewa katiba ya JMT

  Katiba ya JMT ina athari kwa watu milioni takribani 45. Katiba ya ZNZ ni ya watu milioni 1

  Wznz wakichezea katiba ya SMZ kwa kadri wanavyoweza si tatizo la watu milioni 45

  Tatizo ni 'uchezeaji' unapogusa masilahi ya watu milioni 45 bila sababu za msingi

  Dharau dhidi ya katiba ya JMT ni dharau dhidi ya wananchi milioni 45

  Dharau inaifanya katiba ya JMT kuwa na viwango tofauti 'double std'

  Wznz wakinyofoa vifungu vya katiba visivyo na masilhai kwa hilo ni sahihi
  Watanganyika wanawajibishwa na katiba hiyo kwa mambo yenye masilahi

  Tumezungumzia suala la diaspora katika uzi wa 'awamu ya tano na yanayojiri'

  Hoja zinazotumika kujadili diaspora ni 'hilo ni suala la kikatiba' na bunge linajukumu

  Je, Bunge limeshirikishwa kikamilifu kwa haya yanayotokea Zanzibar?

  Kwanini suala la diaspora liwe la kikatiba zaidi kuliko haya ya ZNZ yaliyopo kikatiba zaidi?

  ZNZ ina set precedent mbaya kuhusu katiba. Inaifanya iwe nyaraka chini ya hadhi yake

  Tuwaulize walioapa kwa katiba JMT, huu ndio ulinzi wa katiba walioapa kuutumikia?

  Nguvu ya znz inapatikana wapi kiasi kuweza kuamua tu wanalotaka bila kujali katiba?

  Tusemezane
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Nov 17, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  HSITORIA NI MWALIMU MZURI

  YA OIC , ZNZ NA MUUNGANO 'YANAJIRUDIA'

  Viongozi hawajifunzi kutoka historia na ni wepesi wa kusahau
  Historia haitengenezwi inajitengeneza,haina huruma wala kuonea. Ipo kama ilivyo

  Kwa wa zamani mtakumbuka 'fukunyuku' zilizoaa mtikisiko wa muungano
  Zanzibar iliachwa ifanye inavyotaka, hasira zikijijenga miongoni mwa Watanganyika

  Malalamiko kuhusu Zanzibar na 'uhuru' wa kufanya watakalo yalianza wakati wa Mwalimu
  Watanganyika hawakuwa na fursa ya kuyazungumza hadharani, huku yakijijenga mioyoni

  Kipindi cha Mzee Mwinyi ukatokea mtafaruku wa ZNZ kujiunga na OIC
  Likazaliwa kundi la G55 kutaka uwepo wa Tanganyika

  G55 haikutokea kwasababu ya OIC pekee, ni hasira za muda zilizotafutiwa sababu halali
  Kwamba, ni wakati Tanganyika ikawa na serikali ili kuamua hatma ya mambo yake

  Hoja ya G55 pamoja na nyingine ni, muungano hauheshimiwi na katiba haiheshimiwi
  Mwalimu alibaini nguvu ya G55 akazima hoja kwa mantiki si sera ya chama

  Mwl alisema suala la katiba linawahusu wananchi, lini wameulizwa?
  Kosa la Nyerere ni kudhani, nguvu za dola zinaweza kuulinda muungano zenyewe

  Mwl alisahihisha kosa . Akachukua mkondo wa kueleza mtikisiko wa muungano kimantiki

  Mwalimu alijifunza kutoka historia, kwamba, grievances zikijijenga zinaweza kuibuka katika wakati usiotarajiwa na nguvu zote za kuuzima zikawa zimechelewa

  Miaka 15 baada ya kifo cha Mwl makosa yale yale ya kuchezea katiba kama ilivyokuwa OIC yanajirudia kwa mtindo mwingine. Yale ya ZNZ 2010 na hili la mafuta na gesi

  Viongozi wasidhani ukimya wa Watanganyika ni jawabu.

  Kinyume chake ni makusanyiko ya vionyongo
  Bungeni tunawasikia Watanganyika wakikosa ustahamilivu dhidi ya wenzao

  Hata wabunge wasiosema, wanapopiga makofi ni dalili ya kukubaliana na msemaji

  Ipo siku hasira hizo zitapata sababu.
  Kama ilivyokuwa OIC Watanganyika watakosa subira

  Hakutakuwa na nguvu nyingine zaidi. Muungano utavunjika kama glass

  Tusipojifunza kutoka historia,tusubiri historia ituhukumu! tusijemlaumu mtu

  Tusemezane
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2016
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hili la juzi lina baraka zote za Tanganyika ndio maana Profesa Muhongo alikuwa pale, hapa wanachotwa akili Wazanzibar huu ni mradi wa ccm ili Shein aonekane ni Rais halali.
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Mar 11, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  YA KAMATI ZA KERO NA MAKAMBA YANAONEKANA

  UMEME NAO NI KERO?

  Kama mtafuatilia,tumeongelea sana kamati za kero zilizoongozwa na Mh Makamba
  Tulisema miaka 50 hazikutatua kero, iweje ghafla tuambiwe kero zimetatuliwa?

  Tukasema kamati zinazoundwa hazina majibu ya matatizo mapana ya muungano

  Majibu ni kuuangalia muungano kwa miaka 50 na ku review kama unahitaji ukarabati

  Tumesema kamati zinalenga kuwafariji Wazanzibar zikupuuza hoja za Watanganyika

  Wakati huo huo kamati zinapuuza ukweli kuwa muungano umebebwa na Tanganyika

  Watanganyika wanaweza kupuuzwa kwa baadhi ya nyakati, ikifika wakati litakuwa tatizo

  Kauli ya Rais kuzitaka taasisi na mashirika kulipa ada Tanesco imeleta mtafaruku

  Wazanzibar wakiona wamedhalilika, Watanganyika wakjisikia kuongelewa ya maoyoni

  Rais Shein kasema deni lipo miaka 20 na analifahamu tangu akiwa makamu wa Rais

  Swali, ikiwa kuna kamati za kero nyingi tu zilizoundwa, hili lilifikaje hapa bila suluhu?

  Hili si suala la muungano, ni suala la uchumi, bahati mbaya Wazanzibar wanalifanya la kisiasa wakiamini ni turufu ya kukwepa ukweli kama ambavyo wametumia tume za kero

  Wanaamini deni likifanywa kero, kamati za Mh Makamba zitatafuta namna ya kulifuta

  Somo linalopatikana hapa, hatuwezi kutibu dalili za maradhi kila siku kwa tume za kero

  Ni lazima tutibu ugonjwa ambao ni muundo wa muungano.

  Kuna ulazima wa kukaa chini na kuangalia tena muundo wa muungano.

  Lengo likiwa moja,muungano ubebe maana halisi ya kushirikiana, kusaidiana, kuwajibika na kubeba majukumu

  Na liwe fundisho kwa wanaoamini kuulinda muungano kwa silaha wanafanya makosa

  Jambo dogo linaweza kuleta hisia na tatizo likawa kubwa lisiloweza kuzimwa kwa silaha

  Tusemezane
   
Loading...