Muungano ndio chanzo cha umasikini Zanzibar?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,802
94,311
hivi ni kweli kabla ya muungano zanzibar ilikuwa nchi ya pili africa kwa kipato cha mwananchi?
nini kilitokea?
ni kweli muungano ndo chanzo cha umasikini????

how?????????
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,781
Pia chanzo cha Umasikini Bara; Umeme woote unaokwenda Zanzibar angalau ungetumika Bara tusingekuwa na Maumivu haya ya Umeme
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,802
94,311
rajab_0.jpgZanzibar na Mauritius - kisa cha nchi mbili katika bahari moja…


Ahmed Rajab
7 Sep 2011
Toleo na 202


HAYA ni masimulizi ya nchi mbili: Zanzibar na Mauritius. Zote ni mchanganyiko wa visiwa vilivyo katika Bahari ya Hindi. Zote zina wakazi wapatao milioni moja na laki mbili. Zote zina watu wa mchanganyiko wa makabila. Zote zikitawaliwa na Waingereza. Zote zinapendwa na watalii wa kimataifa.
Wakati nchi hizo mbili zilipopata uhuru- Zanzibar mwaka 1963 na Mauritius mwaka 1968 zote zikitegemea mauzo ya zao moja tu (sukari ikisafirishwa na Mauritius na Zanzibar ikijinata kwa karafuu zake.)
Hii leo ukiyalinganisha maendeleo ya nchi hizo mbili utaona kwamba Mauritius imeipita sana Zanzibar. Mauritius ni nchi iliyoendelea yenye uchumi wa wastani, si wa kati na kati bali wa juu, ilhali wananchi wengi wa Zanzibar ni hohehahe hahehohe wanaishi kwa kasoro ya dola moja tu ya Marekani kwa siku. Wengi, mjini na mashamba, wanamudu mlo mmoja tu kwa siku.
Katika mfungo huu uliopita wa Ramadhani nilishangazwa sana kusikia kwamba kuna watu katika sehemu za mashamba ambao wamekuwa wakilia kwa ughali wa mhogo, seuzi wa vyakula vingine.
Hali hiyo ya ukosefu wa lishe bora itaziathiri vibaya hasa afya na akili za watoto wetu.
Tukiwaangalia wenzetu kwenye Bahari ya Hindi tunabakia tukizimezea mate hali za maisha yao wananchi wa Mauritius. Nathubutu kusema kwamba maisha yao ni ya hali ya juu kwa sababu kinyume na nchi nyingi za Kiafrika, Mauritius haikuwa na machafuko na machafuzi kama ya mapinduzi - si ya kiraia si ya kijeshi - na ilijiepusha na mfumo wa udikteta wa chama kimoja cha kisiasa.
Yote hayo yamechangia kuwafanya wananchi wa Mauritius hii leo wawe wanaishi maisha aali yaliyo bora ukilinganisha na yale ya wananchi wa Zanzibar. Wananchi hao pia wana matumaini mema kwamba mustakbali wao utakuwa mwema. Wananchi hao wameweza kuwa na hali hizo kwa sababu Mauritius imekuwa na uhuru wa kuzidhibiti kwa ukamilifu sera zake za kiuchumi na kijamii na majaaliwa yake kwa jumla.
Kwa ufupi, Mauritius inaweza kujipangia mambo yake yenyewe kwa ushirikiano wa wananchi wake wa itikadi tofauti za kisiasa.
Mauritius imesimama imara yenyewe; haikuwa kama Zanzibar iliyohaulisha madaraka yake muhimu kwenye Serikali ya Muungano baada ya Muungano huo kuundwa kutokana na njama za shirika la ujasusi la Marekani la CIA mwezi Aprili mwaka 1964.
Miaka mitano kutoka sasa yaani kufikia mwaka 2016 Mauritius itakuwa ni kisiwa chenye uchumi usiotoza ushuru. Hivi sasa Mauritius ina Jumla ya Pato la Taifa la dola za Marekani 7,000 kwa kila mtu na kima hicho kinatazamiwa kupanda na kufikia dola za Marekani 8,500 kwa kila mtu kufikia mwaka huo wa 2016.
Zanzibar, kwa upande wake, miaka 47 baada ya kuungana na Tanganyika, ina Jumla ya Pato la Taifa la dola za Marekani 360 kwa kila mtu na ni Mungu tu ajuaye mustakbali wake utakuwaje miaka mitano kutoka sasa kwa vile hatuna takwimu za kiuchumi zilizo sahihi na zenye kuaminika.
Tusisahau pia kwamba mwaka 1964 Zanzibar ilikuwa imeendelea kuipita Mauritius na ilikuwa ya pili baada ya Afrika ya Kusini katika eneo hili letu. Mwenye kuutaka ushahidi wa haya na aende akaangalie ripoti za serikali za nchi hizo mbili za wakati huo au ende kwenye Banki Kuu ya Dunia akaangalie takwimu za wakati huo zilikuwaje.
Swali linalozuka ni kwa nini basi Zanzibar ikawa iko nyuma sasa na Mauritius ikawa imeendelea ilivyoendelea na kupata sifa ya kuwa pepo ya utalii wa visiwa na kivutio cha wawekezaji?
Nadhani kuna sababu kuu mbili. Bila ya shaka sababu ya kwanza inayonijia haraka kichwani ni machafuko ya kisiasa yaliyokuwa yameivaa Zanzibar tangu mwaka 1957 hadi mwaka 2010 ilipoundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Udhaifu huo wa hali ya kisiasa baadhi ya nyakati ulisababisha umwagaji wa damu na ulisababisha pia kuvunjika kwa taasisi muhimu za dola kama vile Utumishi wa Serikali, Mahakama na kuparaganyika kwa mfumo wa elimu uliokuwa umeendelea pamoja na kuoza kwa huduma za afya.
Isitoshe pakazuka hali zilizokuwa na uhasama na zilizowazuia Wazanzibari wasiweze kuwekeza na kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.
Mambo nchini Mauritius yalikuwa tofauti kabisa. Nimeyaeleza haya kwa marefu na mapana kwenye sahafu zilizopita na kama nilivyosema serikali mbalimbali zilizotawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1968, zikiwa pamoja na serikali za chama cha Kikomunistu, hazikuzichezea au kuzigeuzageuza taasisi za dola. Wala Mauritius haikuitangua au kuibatilisha katiba yake ya wakati wa uhuru.
Kadhia za nchi hizi mbili inaonyesha bayana tofauti iliyopo kati ya nchi yenye madaraka makamilifu na uwezo wa kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya haja ya ushauri au ridhaa ya dola ya kigeni na ile ambayo haina madaraka na uwezo huo.
Wazanzibari wanahitaji kusoma kutoka historia ya nchi yao na kutoka historia ya visiwa vingine duniani vilivyoendelea kupita sehemu za mwambao au za mabara zilizo karibu navyo.
Wanapaswa waangalie jinsi visiwa hivyo vilivyo na amani, usalama, utulivu na hali thabiti za kisiasa. Yote hayo ni muhimu kwa mandeleo ya kiuchumi ya nchi yoyote ile.
Jambo jingine muhimu linaloifanya nchi iendelee kiuchumi au kijamii ni mfumo wake wa elimu. Mfumo wa elimu wa Zanzibar ambao ulikuwa wa kupigiwa mfano ulifujwa ijapokuwa kweli kulikuwa na nia njema ya kuutanua mfumo huo na kuhakikisha kwamba watoto wengi zaidi wanakwenda skuli na kupatiwa elimu ya kisasa.
Nchini Mauritius hali ilikuwa tofauti. Mfumo wake wa elimu haukufujwa bali uliendelezwa kufika hadi kwamba sasa watoto wanaohitimu na kufaulu mitihani ya masomo ya sekondari wanakubaliwa moja kwa moja kuingia kwenye taasisi za kigeni za elimu ya juu. Tukija kwetu tunaona kwamba vyeti vinavyotolewa na taasisi za elimu ya juu za Zanzibar havitambuliwi hivyo duniani.
Kwa jumla, tunaona kwamba ni muhimu kuzihifadhi taasisi tulizo nazo na kama kuna haja ya kuzibadili basi mabadiliko yasifanywe kwa papara na yawe yanafanywa na watu wenye elimu inayohitajika, uzoefu na ujuzi na kamwe yasiachiwe watu wasiotambua athari za hatua zao.
Lau Zanzibar itaendelea na kupata mafanikio sawa na ya Mauritius basi haitokuwa na ufukara uliozagaa. Hii leo wananchi wa Mauritius wanaishi uzuri, wana elimu nzuri, wana huduma nzuri za afya, watu wake wasio na ajira hawafiki idadi ya asilimia 60 na zaidi kama ilivyo Zanzibar.
Si hayo tu bali uchumi wa Mauritius unastawi kwa kasi na huwasikii wananchi wake wakilalamika kuwa bei za vyakula ni za kuruka sana au kwamba hawamudu milo mitatu kwa siku. Ndiyo maana wachambuzi wa mambo ya kiuchumi na wataalamu wengine wanasema kwamba Mauritius ni mfano mwema wa maendeleo kuigwa na nchi nyingine za Kiafrika.
Zanzibar inaweza kuwa na fursa nzuri sana kuishinda Mauritius kuwa kitovu cha biashara na huduma katika eneo hili la Afrika. Mafanikio ya Zanzibar lakini yatategemea pakubwa juu ya jinsi zitavyoondoshwa tofauti zilizopo kati ya Tanganyika na Zanzibar zikiwa nchi mbili tofauti kila moja ikiwa na ajenda yake.
Endapo hali ya mambo itaselea kuwa kama ilivyo basi hatutokuwa na budi ila kujilaumu wenyewe kwa hali tunayojikuta nayo. Tukisema kweli katika miaka iliyopita viongozi Wakizanzibari waliokuwa wakiiwakilisha Zanzibar katika Muungano hawakutekeleza kazi zao sawasawa.
Ni muhimu kwamba katika siku zijazo Wazanzibari wanaopewa dhamana ya kuiwakilisha Zanzibar katika huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wawe wanahakikisha kwamba wanaitetea Ajenda ya Zanzibar na wala si sera za kisiasa za kichama au zao binafsi.


[h=2]Wasomaji[/h] 914

Wasiliana
na mwandishi
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
5,372
Mauritius walijikita zaidi katika biashara za manufacturing. In other words they diversified. Zanzibar baada ya Karume hawajawahi kupata uongozi mzuri. Hata zile nyumba alizojenga Karume zilikaa bila kukamilika muda mrefu baada ya kifo chake. Zanzibar wana viwanda gani? Wenyewe walitaka short cut. Wanunue finished goods Dubai watuuzie sisi mainland.
 

NgomaNgumu

Senior Member
Nov 20, 2010
194
24
Mambo ya Zanzibar na Tanzania bara ni magumu kuyajadili kwani ni muhimu kuzingatia pande mbili. Upande wa kwanza ni ule wa kisiasa ambao wengi wanaojaribu kuulezea hawajui siasa na wala hawana information za kutosha matokeo yake wanatumia dhana wanapotea hao wenyewe na wanawapoteza watu wengine.

Ingia ktk youtube andika mapinduzi ya Zanzibar 1964 alafu msikilze karume anamwambia mzungu kua hatutaki kutawaliwa na watu wachache. Baadae kuna upande wa kidini ambao nao una maneno mengi. Kila mmoja kati ya Tanzania bara na visiwani anamuhitajia mwenzie ni bora likafahamika hilo ili ipigwe hatua mbele badala ya kusema wanzanzibar wangapi wanabiashar bara na wabara wangapi wako Zanzibar. Hata kila mmoja akirudishwa kwao bado atahitaji kusafiri tena kwanini tunakwenda China?
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,405
2,956
Tukiuvunja muungano baada ya miaka 2 tu,mutajua kuwa umasikini ni muungano au laaa.

Ila mambo yote yako wazi ,kama wataka kujua muungano huu ulivyo imaliza zanzibar,ingia mzalendo.net nenda video,utakuta makongamano ya katiba,utaona jinsi gani wanasheria wanavyo uchambua muungano na kabla ya muungano na hasara za muungano.

Imefikia hali wananchi wa zanzibar hatuutaki tena muungano,kabla ya muungano,zanzibar ilikuwa mwanachama kabili wa umoja wa mataifa,Tanganyika ilipata uhuru 1961 lakini hakuwahi kuomba uwanacha wa UN,alichokifanya kwa ujanja wake,alienda umoja wa mataifa na kupeleka barua ambayo ilisainiwa na rais wa tanganyika kuwa muungano wetu unatambulika kama TANZANIA,kwa maana hio,zanzibar iyondolewe katika UN na kiti chetu kukaliwa na Tanzania.

Tujiulize kwa nini Palestina wanataka kujiunga na Umoja wa mataifa ?

Uchumi wa zanzibar ulitegemea karafuu,na biashara,na biashara inaenda kimataifa,sasa ikisa sisi wanzanzibari na zanzibar imekosa mwanachama wa UN vipi atakuwa na internatinal relation na nchi nyengine kibiashara ?
Vipi zanzibar itapata misaada kutoka UN ,kama Wizara ya afya,elimu,Miundo mbinu,na mengine ? Misaada yote inaangukia katika mikono ya tanzania ambayo ndio tanganyika,zanzibar huambukizia patupu.

Baada ya hilo serikali ya muungano imetumia pesa kwa kuwafanya wachache wetu wazanzibari kuwa watumbwa wa mkoloni mweusi tanganyika,wakipewa vimilioni kazaa na madaraka basi wao ni ukirindimba wa kisiasa,kuwafukuza wapemba katika serikali ya SMZ,na kuwajiri wanamaskani ambao hawakusoma leo hii ndio hao walitusababishia vifo vya mamia ya watu.

Kuna mengi sana ambayo yameibana zanzibar kwa kupitia muungano,lakini pia nyerere alitumia kura moja ambayo ndio hiyo imefika miaka 47 toka muungano,kuweza kupiga hatua,moja ni kuwagawa wazanzibari baina ya pande mbili ya visiwa,pia kuleta ukabila eti cuf wataleta uwarabu.

Hayo ndiyo yaliweza kuimaliza zanzibar,lakini kwa wakati huu hayana nafasi tena,naweza kusema kuwa sasa tuko kitu kimoja katika kudai taifa letu,naamini iko siku tutafika huko huko tulikotoka,na kutambulia taifa huru la wazanzibari na kujikomboa na umasikini.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
26,814
46,435
..umasikini wa Zanzibar umetokana na kuanguka kwa zao la karafuu.

..wa-Zenj badala ya kujadili tofauti na matatizo yao, wameamua kusingizia kila kitu kwa Watanganyika na Nyerere.

..wanafikiri hiyo ndiyo njia ya kuleta maelewano na umoja miongoni mwao.

..Nyerere hakuwavika wa-Zanzibar[Kassim Hanga,Azizi Twala,Mdungi Ussi,...] nanga na kuwatosa baharini.

..kuna kipindi Nyerere aliumbuliwa kwenye mkutano wa non alligned baada ya Iran kutoa malalamiko kwamba kuna viongozi wa Tanzania[Zanzibar] wanaona kwa nguvu wanawake wenye asili ya Kiarabu. Ilibidi Mwalimu akawakemee wajumbe wa baraza la mapinduzi waliokuwa wakijihusisha na vitendo hivyo. Hata hivyo according to Nyerere, utetezi wa Karume ulikuwa "..lakini mbona wao nao walilazimisha kuoa dada zetu kwa nguvu?"

NB:

..majuzi hapa Prof.Shivji kawapasulia "jipu" wa-Zenj kwamba aliyetia saini muswada wa kuyatumbukiza mafuta ktk masuala ya muungano ni Sheikh Abeid Amani Karume!! Nyerere alikuwa yuko nje ya nchi na Karume alikuwa ndiyo Kaimu Raisi wa Jamhuri wakati huo.
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
bora muungano ufe uoze kabisa ili tuepukane na migogoro ya kidini ambayo inachipuka na kuota mizizi kila leo.
 

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,365
2,055
ni kweli muungano ndo chanzo cha umasikini????
Kama Wanzanzibar wanaamini hivyo basi tuwaache wajitafutie maendeleo yao kivyao, kwa nini tunawalazimisha Wazanzibar na kuwa nasi kwenye Muungano, why?

 

Kiponya

Member
Nov 20, 2010
34
1
I declare interest! Mi ni mtanganyika, kuna mambo kadhaa huwa najiuliza kila mara hivi ni kweli we are the source of their poverty? (Wanzanzibari!) think of their life style, think of their attitudes towards work, think of their traditional values. Ni Tanganyika inayowafanya Wanzanzibar wawe na akili za ajabu walizonazo leo? Hivi kweli tuna uwezo mkubwa namna hiyo? Jamaa wanataka kuwa kitovu cha biashara!!!!!!!!! Kitovu cha biashara gani ya watu 1.2? Au mnadhani sisi ndo tutakuwa wateja wenu like we used to be? After tax harmonization you know what you are facing? Mahitaji yenu ya kila siku hata viungo vya msosi mnafata bara, guys lets be serious! As a matter of fact you need us than we need you. Kutulaumu sie kisa uvivu wenu kufanya kazi sio sawa.
 

Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,001
589
Suala kubwa wanalosahau wazanzibar ni kuwa wana tatizo kama la huku bara,kupata viongozi wenye maono ya maendeleo-endelevu...Tumefunikwa wingu la kuchagua eti 'zimwi likijualo' hata kama linakupeleka shimoni.Viongozi wanaotenda kimazoea bila ya ubunifu miaka nenda miaka rudi wanakalia kubinafsisha viwanda na mashirika waliojenga wenzao hawafanyi lolote la maana lakini sisi wananchi tumewakumbatia kwa kuwapigia kura kila uchaguzi,je tunawawajibisha ipasavyo? jibu ni hapana..tutakalia kulialia eti tuvunje muungano tukitegemea nafuu ya kwenda kujipendeka kwa waarabu na wazungu waliotufanya watumwa wao..wakati wao tunaokwenda kuwalamba miguu wanajiimarisha katika muungano (chukulia mf.EU) siye tunafanya kila njia eti tuuvunje.,Umaskini wa Zanzibar au Tanganyika hausabibishwi na na muundo wa muungano perse bali utekelezaji mbovu wa sera na makubaliano ya pande zote mbili na kutokuwajibika vilevile kwa viongozi haswa wakisiasa wanaopelea utendaji mbovu kwa watendaji wa serikali na sisi wananchi kushindwa kutekeleza wajibu wetu..
Ni mpaka pale wananchi tutakapotambua nafasi yetu juu ya masuala muhimu yanayogusa maisha yetu na haki na wajibu wetu katika kusaidia yafanyike vile tunavyotaka ndipo hizi lawama zinazosababishwa na ufukara wa kipato zitakapo patiwa ufumbuzi..
 

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Hakuna kosa wa ubaya wowote kwa Zanzibar kutaka kuwa nje ya muungano. Ni kweli kwamba muungano ni moja ya sababu ya wao kurudu nyuma kimaendeleo, hilo halina ubishi. Kabla ya kuungana hizi zilikuwa nchi mbili jirani tu; inawezekana kwa mazingira ya wakati ule pengine ilikuwa sawa kuungana lakini si leo. Watu wanahofia uongo wa Nyerere kwamba muungano ukifa hatutakuwa salama; ikumbukwe kuwa huyu mtu alikuwa dikteta aliyetumia sana propaganda na kunyima watu elimu. Kwa mfano, hivi inaingiaje akilini unapowaambia watu kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi halafu watu wanalimia jembe la mkono, hakuna matrekta, combine harvesters, mitambo ya umwagiliaji, uwekezaji wala utaalamu?
Halafu pia si sahihi kulinganisha umoja wa Ulaya na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. EU ina misingi kadhaa ya kuungana kwao, mfano si nchi zote zinatumia sarafu ya Euro. Kuna nchi ambazo mtu anaweza kusafiri kwa kutumia visa ya Schengen wakati nyingine haziitambui visa hiyo. Isitoshe ukiwa kwenye nchi mwanachama bado utaifa na uraia wa nchi ile unabaki kama kawaida, hakuna nchi mwanachama aliyeshusha bendera yake na kupandisha ya EU.
Ni unafiki kuamini kuwa kuna muungano hapa kwetu, infact wala hatuhitaji kuwa nao. Wazanzibari kazeni buti mjiondoe, ila karafuu peke yake haitaleta maendeleo, mnapaswa kuvutia uwekezaji hasa wa viwanda na pia mbadili mfumo wa elimu na mpunguze influence ya dini vinginevyo mtaendelea kucheza makida makida.
 

think more eat less

New Member
Mar 8, 2012
1
0
Ninachokiona tofauti yetu na MAURITIUS ni rangi ya watawala kwani inaonekana wazi nchi nyingi zinazotawaliwa na watu weusi zipo kwenye dimbwi kubwa na zito la umasikini.kwani sisi badala ya kuweka sera nzuri na kuzitekeleza tunaendeleza ubaguzi tu kila kona kuanzia kwenye maofisi ukiingia tu ofisi yeyote iwe ya serikali au binafsi basi ukitaka kujua BOSI wa hapo anatoka wapi ,basi tazama wafanya kazi walio wengi hapo wanatokea pande zipi basi utajua tu.PIA kwenye nchi hizi utekelezaji sawa wa sheria huwa mgumu sana.,Mfano tokea nipo form one hadi leo GRADUATE kuna watu wao ni viongozi tu hawabadili wala hawashuki chini na watoto na wajukuu zao wanapatiwa nafasi nyeti na nzuri kwa kuwa wazee wao wamo kwenye system tu.
...MIMI NAONA WATU WAKUBALI SHERIA IFANYE KAZI KWA USAWA NA WAONDOSHE UBAGUZI NA UBINAFSI .....
 

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
247
Muungano unatia umaskini pande zote, zanzibar na tanganyika. Viongozi wanaacha kupanga mbinu za kuinua uchumi wanakalia kila siku oo kero, kero za muungano ambazo hazina hata tija kuzijadli. Muungano usingekuwepo kusingekuwa na visingizio vilivyopo sasa.
 

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Wazanzibar mmechelewa sana kutambua kuwa Muungano ulikuwa na malengo makuu mawili

a. Udini wa nyerere; nyerere alihofia sana waislam na uislam unavyokua katika eneo la africa mashariki na kwa kutumia na crusaders wenzake aliweza kudhoofisha nguvu la taifa hili la kiislam, bila muungano zanzibar ingekuwa islamic state, wakoloni wengi hawapendi jambo hili na nyerere alikuwa kibaraka wao..proved amefanya kazi vema sasa hivi ni st...

b. Wanafiki wa zanzibar; wazanzibar wachumia tumbo wameongoza nchi hiyo tangu uhuru wametumika na wanatumika kama toilet paper na watanganyika, hilo litaendelea kuwa donda ndugu hadi mtakapobadilisha CCM kuwachagulia viongozi kutoka dodoma; otherwise mtayumba tu...
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom