Muungano: Kuna nini ndani ya Hotuba za Marehemu rais Abeid Aman Karume?

Nimeshasikia baadhi ya hotuba zake. Kwa kweli sio za kizazi hiki cha uelewa maana zilikuwa za hovyohovyo na ubabe mwingi na hazina mvuto.
Nadhani ndio maana hawazitoi hadharani
 
Lazima zitakuwepo ila zimefichwa kimaksudi ili kuficha ukweli wa muungano.....Hizo ni janja za wabara

Hapana si janja za wabara, ni janja za wana siasa wa bara na visiwani. Unajua kuwa wapo wabara wengi tu ambao nao muungano unawakera sana? Nifahamuvyo mimi ni kuwa Visiwani pia wapo wana siasa ambao ukiwakata wanatoka damu ya kijani pia kama vile walivyo baadhi ya wana siasa wa bara. Na wanasiasa hao ndo watakuwa wanapinga hizo hutuba kuwekwa hadharani.
 
..nimezisikia zile ambazo Karume alikuwa akisifia Muungano na kuwabeza wale wanaoupinga.
 
Baadhi yetu tulihudhuria mikutano aliyohutubia Makamu wa Kwanza wa Rais, Abeid Amani Karume. Hotuba moja nakumbuka alisema hakutakuwa na Uchaguzi Zanzibar mpaka miaka hamsini ipite!

Wana harakati wa demokrasia walio wanaJF, mwasemaje juu ya kauli hiyo?
 
Naona wadau wengi mmetoa maoni yenu ila ukweli wanaujua hao ambao wemeficha hizo hutuba na kwakweli sio hutuba tu hata historia ya ukweli ya znz haiko wazi kila mmoja anasema kivyake wao walitutesa na wengine wanasema kuwa wao walitupindua na kututumbukiza kwenye visima basi ni mkanganyiko tu wa historia isio julikana ukweli wake ndio maana mpaka leo unaona znz hakuwelewiki ni politics au chuki binafsi na kutaka madaraka tu.
 
Nikiri mimi ni muumini wa kauli za mwl nyerere ila katika hotuba zake za kuhusu muungano sizikubali,hivyo naomba watu wa vyombo vya habari watuwekee vipindi maalum hotuba za abeid karume na abdul jumbe kuhusu muungano maana twataka tupate ukweli wa mambo,je mzee karume alikua na mtazamo gani juu ya muungano huu?Nasikia aliwahi kusema muungano mwisho wake kisiwa cha chumbe
 
sawa sawa, NAFIKIRI UPO SAHIHI TUPATE NA HOTUBA ZOTE ZA VIONGOZI WA UPANDE WA PILI, INGAWA NAKUMBUKA KUNA HOTUBA MOJA YA MZEE WETU KARUME NILIISIKIA KWA KWELI HAIKUWA NZURI WALA HAIKUWA NA BUSARA HATA KIDOGO, PENGINE HIYO NI SABABU YA KUTOKUWEKA HOTUBA ZAKE.
 
Hivi karume alikuwa anaweza kuhutubia kweli? Au alitegemea hotuba za mwlimu zimbebe
 
karume hakuwa na hotuba za kusisimua kuhusu muungano. Nyerere tu ndo aliweza

Wakati wa Karume kulikuwa na muungano wa nchi mbili lakini kuanzia 1977 muungano ulikuwa si muungano bali ni utawala wa nchi moja kwa mwengine! Hapo sasa ndio Nyerere alijaribu kuulinda utawala wake kwa ukali!
 
asili ya muungano huu ni Nyerere alitaka kuiteka Zanzibar ila kwa wakati ule hakuna aliyejuwa, alitumia ujanja kwamba Zanzibar haijakuwa na uwezo wa kujilinda wenyewe karume ndio akakubali kumwaga wino sasa Tanganyika imetuganda kama kupa haitaki kutuachia, karume mwenyewe aliuliwa
 
haha..nimeipenda hii ..km hukuilete ningeileta mimi..Yule mzinji kamfunika sana Sendeka.Aliuliza kirahisi sana bila mikaratasi km sendeka.Ila sendeka kwa upuuzi hakuelewa sana.MIjasho tuu ilimtoka.
 
Nikiri mimi ni muumini wa kauli za mwl nyerere ila katika hotuba zake za kuhusu muungano sizikubali,hivyo naomba watu wa vyombo vya habari watuwekee vipindi maalum hotuba za abeid karume na abdul jumbe kuhusu muungano maana twataka tupate ukweli wa mambo,je mzee karume alikua na mtazamo gani juu ya muungano huu?Nasikia aliwahi kusema muungano mwisho wake kisiwa cha chumbe

Tunaomba CV ya Karume kwanza kabla ya kusikiliza Hotuba zake!
 
Hivi karume alikuwa anaweza kuhutubia kweli? Au alitegemea hotuba za mwlimu zimbebe


Mzanzibari asiyesoma hata Darasa moja ni mahiri wa kuhutubia kuliko mbara wa darasabla saba. Wazanzibari wameiva kisiasa kuliko wabara na hawayumbishwi na rushwa kama bara.
Nyerere akimuogopa sana Karume pamoja na Elimu yake
 
Back
Top Bottom