Muungano: Kuna nini ndani ya Hotuba za Marehemu rais Abeid Aman Karume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano: Kuna nini ndani ya Hotuba za Marehemu rais Abeid Aman Karume?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sonara, Apr 25, 2009.

 1. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na mikakati kwa miaka mingi kuhakikisha hotuba zote za Marehemu Abeid Aman karume,zinazo zungumzia mungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR zisisikike na kuwafika wananchi huku za Mwalim julias zipo hewani ,hapa tujiulize nini kinafichwa ikiwa viongozi wa pande mbili hizi walikubaliana Mungano ?wanaficha Mkataba wa Mungano,ingekuwa jambo la Busara tukawa tunamsikia nini alikuwa anauzungumzia kuhusiana na Mungano huu kama vile tunavyomsikia Mwalim julius Kambarage Burito Nyerere.walikubaliana Mungano ?
   
  Last edited: Apr 25, 2009
 2. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na mikakati kwa miaka mingi kuhakikisha hotuba zote za Marehemu Abeid Aman karume,zinazo zungumzia mungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR zisisikikena kuwafika wananchi huku za Mwalim julias zipo hewani ,hapa tujiulize nini kinafichwa ikiwa viongozi wa pande mbili hizi walikubaliana Mungano ?wanaficha Mkataba wa Mungano,ingekuwa jambo la Busara tukawa tunamsikia nini alikuwa anauzungumzia kuhusiana na Mungano huu kama vile tunavyomsikia Mwalim julius Kambarage Burito Nyerere.
   
 3. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sonara!

  Wacha utani!
  Marehemu KARUME AMAN ABEID never went to a formal school beyond darasa la nne and some sort of mdrasat just like many other buddies of his time!

  Wako wengi hata Kawawa who is alive and kicking sijasikia hotuba zake na he has never complained!

  What kind of hotuba you would like to quote form the semi illitrate and long dead Karume RIP!

  Please don't misuse this forum ukidai tutangaze hotuba ambazo they were never there! Kama zipo kuna wajanja walimwandikia akasoma!!

  Usilete malumbano yasiyokuwa na msingi! Lets the union die its natural death!!
   
 4. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 487
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 60
  sonara kama unazo tuwekee hapa na tutazifikisha sehemu husika ili zisikilizweee
   
 5. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukienda maktaba ya Sauti ya Tanzania Zanzibar au Television ya Zanzibar unaweza kupew kopi. Maana wao wanazo nyingi tu kuanzia Audio hadi Video.

  zikikaribia sherehe za muungano huwa wanaonyesha/wanaweka hotuba ktk vyombo hivyo vya habari vya serikali; cna hakika kwa mwaka huu.
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shule na kujua kuongoza watu ni vitu tofauti; Mzee Karume pamoja na kuwa hakwenda shule, kuna baadhi ya mambo ya maendeleo ya wananchi aliyaongoza na kuyasimamia vizuri yakaenda sawa kama alivyotaka.

  Pamoja na yote hayo hakukosa weakness za watawala wengi wa kiafrika kunyanyasa watu, ukatili uliopindukia mipaka n.k
   
 7. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Let the guy Rest In Peace. Hotuba za zamani hazina maana yoyote kwa maendeleo ya kisasa.
   
 8. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa Nyerere jee, the counter part don't u want him to rest in peace also, why u worry us with his hotubas at this time. sasa hili ndio tatizo lenu- la Muungano -ni la pande mbili. Hi supremacy attitude inatoka wapi- jamani?
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya si malumbano yasiyo na msingi. Why u quote from Nyerere kuhusiana na Muungano huu. We need kusikiliza hotuba za Karume pia- yeye hakusoma kama unavyosema wewe, lakini wasomi wa Kizanzibari hivi sasa wanaweza kuchambua hotuba zake na kupata msimamo wa mambo mengi tu. Kwa mfano kuna hotuba pale Karume alimfukuza Amir Jamal (Waziri wa Fedha wakati huo) Anasema na kariri ( Huyu Nyerere huyu ati anatuletea huyu mhindi mwizi aje atuibie asilan hatukubali). Wewe, Wizara ya Fedha ya SMT (Jamal huyo) mpaka leo inatuibia na mfumo wake wa kodi na mambo mengi tu. Usiponde hotuba za Karume - hizo ni hadidu reje kwetu- Tena zipo pale tumezihifadhi STZ na tunazisikiliza kila mara.
   
 10. S

  Stone Town Senior Member

  #10
  Apr 25, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalamu alaykum.

  Mie katika hili nitasema mambo machache tu ingawa nakubaliana na elimu ni muhimu sana lakini naamini elimu ni kitu kimoja na kuitumia elimu yenyewe ni kitu cha pili unaweza ukasoma lakini elimu yako isikunufaishe kwa maana ukawa huitumii elimu yako. na unaweza usisome lakini mambo utakayofanya unaweza kuwashangaza wengi hasa wasomi na hilo ndio lililotokea kwa Mzee Karume ingawa mambo mengi aliyoyafanya sikubaliani nayo hasa ya ukiukwaji wa haki za binaadamu lakini kwa wakati ule yalifanyika sana na hakukuwa na uhamasa huo wa kuepusha mambo hayo lakini katika suala la kutaka maendeleo alikuwa mbele zaidi kuliko hata hawa viongozi wetu wa sasa hebu imagin mtu aliyekuwa hakusoma lakini alikuwa na vision kiasi gani hata aka plan kujenga nyumba za maendeleo magorofa ya michezani, wete pemba na nyumba za vijiji, hoteli ya bwawani na mambo kadhaa ya kuonesha kama ni mwana maendeleo.

  kila la kheri
   
 11. Z

  Zahir Salim Member

  #11
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akili ni Nywele kila mtu ana zake, na ndio maana ya wengi wa Walimwengu walimshangaa Julius Nyerere Kuitambuwa Biafra kama Nchi ilihali akijuwa kuwa ni jimbo la Nigeria licha yakuwa yeye ni msomi alishindwa na Umbumbumbu wa Karume alieheshimu Mipaka ya wenzake.
   
 12. N

  Nkazahau Member

  #12
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika sifa moja aliyokuwa nayo mzee Karume basi ilikuwa ni kutoa speech ambayo ikiweza kufahamika na kila mtu, hebu ziombeni hotuba zake muzisikilize au munaogopa mutamsikia akisema " muungano ni kama koti" au "azimio la Arusha mwisho Chumbe" maana hivi ni vitu vitakatifu kwenye JMT na watu hawatakueleweni wakimsikia muasisi wa muungano akiukandia au?
   
 13. N

  Nkazahau Member

  #13
  Apr 28, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ayaaa, yaani huyu Nyerere mtaka umoja wa Afrika, muasisi wa muungano alitaka wa Nigeria wa Biafra wajitoe katika nchi yao - afanalek, sababu ilikuwa nini? dini au?.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna sababu ya kutumia hotuba za Karume na Nyerere kuamua hatima ya muungano leo? Muungano una mapungufu yake na hakuna anayebisha.Cha kushangaza ni kwanini kuna ligi kubwa ambayo haina tija kwetu. Inalea kupiga domo na kusahau kujiletea maendeleo kwa kufanya kazi mana mara nyingi watu wapiga domo sana hawana maendeleo.

  Dawa ni kurekebisha kasoro hizo ili kuuboresha.Kama Zenj hawataki hilo, basi wao wajitwike hiyo kazi kubwa ya kuua muungano.Ingekuwa bora tuwaache Karume na Nyerere wapumzike kwa amani maana mkataba wa muungano haukuwa kitabu kitakatifu kisichowezwa kubadilishwa. Tukishindwa leo, tutachekesha kama tutatoa sababu juu ya Nyerere na Karume.Wao waliweza kufanya kile walichokifanya. Tufanye nasi yale tunayoweza kufanya ili uonekane bora zaidi.

  Tusidharau huu muungano. Umetusitiri sana kuliko tunavyofikiria. Tukikurupuka na kuudharau tutajilaumu wenyewe.Kama hujui kufa we kachungulie kaburi. Tusianze kufanya mambo yenye kuleta majuto mjukuu
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ndo skuozote tunasema kile kizee kilikuwa kinafik
   
 16. TONY_BLUE

  TONY_BLUE Member

  #16
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba mwenye voice records video or mp3 za SHEIKH ABEID AMANI KARUME au nnaweza kwenda kwenye web gani??
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Lazima zitakuwepo ila zimefichwa kimaksudi ili kuficha ukweli wa muungano.

  Hizo ni janja za wabara
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Sauti ya Zanzibar wana nafasi gani katika hili?
   
 19. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nilipata kumsikia siku moja akiongea kwenye hadhara fulani, sijui ilikuwa wapi, ila nilipata picha na kujua ni kwa nini jamaa hotuba zake mbalimbali huwa hazisikiki. Ni kwamba siku hiyo pamoja na mengine aliuliza ni nani anajiita mtaalamu? mtaalamu wa nini atuambie,hakuna kitu kama mtaalamu na aje hapa atuambie.
  Kwa kifupi ni kwamba hakuwa na mvuto wowote, hotuba zilijaa majigambo na ubabe wa kikulikuli tu ndiyo maana leo hii kuzirusha hewani inaweza kuonekana kituko.
  Kipindi / hotuba hicho kilikuwa TBC na hata hivyo kilikatishwa nafikiri kwa sababu za kimaadili tu kama kuna mtu anamjua mtu wa tbc aombe msaada huenda tutazipata walau chache. Kusema kweli hata mimi nina kiu nazo sana maana ni kwa kumsikiliza ndiyo tunaweza jua alikuwa mtu wa aina gani.

  ........................................
  Amani yetu inatumiwa vibaya
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Barubaru ukisema wabara unakosea, sema CCM yote bara na visiwani kwa sababu SMZ ipo na iko kimya pamoja na kuwa na STZ.
   
Loading...