Muungano huu hatuutaki

miftaah

Member
May 31, 2012
30
5
Awali ya yote kwanza napenda Kumsukuru Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Ardhi kwa kutufikisha siku kama ya leo tukiwa wazima na hata waliokua si wazima hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila kitu.

Ningependa kuongea kwa niaba ya wazanzibari wenzangu na hata wabara pia na wote wanaopenda amani katika Tanzania yetu hii..
Ni kipindi kirefu cc wazanzibari tulikua tunalia kuhusu huu Muungano kua hautunufaishi sisi wazanzibari maana jambo lenye faida hua halilizi ila linafurahisha na ndio mana cc wazanzibari tunasema kua hauna faida kwetu sisi huu Muungano.. Na sio kma hatuutaki Muungano napenda niweke wazi kauli hii.. Kua Muungano huu usiokua na faida kwetu sisi hatuutaki lau kama ungekua na faida kwetu wazanzibari tusingepiga kelele, ila tutapiga kelele hadi viongozi wetu watakapokubali kua tunakua na muungano wenye faida kwa nchi zote mbili.

Labda nirudi kidogo nyuma ya pazia la muundo wa serikali yenyewe..mna mm tokea napata akili zangu sijapata kusikia hata siku moja kusikia kua Gavana katoka Zanzibar,sijasiia hata siku moja kusikia kua Mkuu wa jeshi la wananchi au jeshi la polisi kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia wakuuu wa NECTA kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia kua Tanzanite itakua suala la muungano ila nachosikia kua Mafuta ni ya muungano nk.. na ndio mna nasema kua muungano huu hatuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Mwambieni Shein na bunge lenu (baraza la wawakilishi) kwamba hamtaki muungano, sidhani kama wana JF wanaweza kuwasaidia lolote ili muweze kufikia malengo yenu katika hili.
 
awali ya yote kwanza napenda kumsukuru mwenyezi mungu muumba mbingu na ardhi kwa kutufikisha siku kama ya leo tukiwa wazima na hata waliokua si wazima hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kila kitu.

Ningependa kuongea kwa niaba ya wazanzibari wenzangu na hata wabara pia na wote wanaopenda amani katika tanzania yetu hii..
Ni kipindi kirefu cc wazanzibari tulikua tunalia kuhusu huu muungano kua hautunufaishi sisi wazanzibari maana jambo lenye faida hua halilizi ila linafurahisha na ndio mana cc wazanzibari tunasema kua hauna faida kwetu sisi huu muungano.. Na sio kma hatuutaki muungano napenda niweke wazi kauli hii.. Kua muungano huu usiokua na faida kwetu sisi hatuutaki lau kama ungekua na faida kwetu wazanzibari tusingepiga kelele, ila tutapiga kelele hadi viongozi wetu watakapokubali kua tunakua na muungano wenye faida kwa nchi zote mbili..
Labda nirudi kidogo nyuma ya pazia la muundo wa serikali yenyewe..mna mm tokea napata akili zangu sijapata kusikia hata siku moja kusikia kua gavana katoka zanzibar,sijasiia hata siku moja kusikia kua mkuu wa jeshi la wananchi au jeshi la polisi kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia wakuuu wa necta kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia kua tanzanite itakua suala la muungano ila nachosikia kua mafuta ni ya muungano nk.. Na ndio mna nasema kua muungano huu hatuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

bora uvunjike.
 
Halafu watu wengi wanaofanya mambo ya hovyo hovyosiku hizi, wanapenda kunasema wanafanya in the name of merciful God! Mhh
 
mbona majibu umeshayatoa - muungano sio kitu kibaya isipokuwa hayo mambo uliyoyataja yarekebishwe. kuchoma makanisa hakuwezi rekebisha hayo mambo muhimu uliyoyataja. nami nakuunga mkono kwa kasoro hizo ambazo zimo katika uwezo wa kurekebika.
 
kwa dunia ya leo ya grobalization (kijiji kimoja kidogo) alafu eti kuna watu wanataka kuunda ka-jiji kao kadogoo sawa wanaweza kufanikiwa but wao wenyewe wajitasmini je wanaweza kupambana na mikikimikiki ya kiutawala maana siku za usoni wasije wakawa waki......Tanga......ka alafu nchi wakawaachia............wakila bata.Maana kwa sasa hajulikani nzanzibar ni nani na mbara ni yupi eti kigezo dini,lugha na rangi.anyway rejeeni historia labda mtapata jibu.
 
kwa dunia ya leo ya grobalization (kijiji kimoja kidogo) alafu eti kuna watu wanataka kuunda ka-jiji kao kadogoo sawa wanaweza kufanikiwa but wao wenyewe wajitasmini je wanaweza kupambana na mikikimikiki ya kiutawala maana siku za usoni wasije wakawa waki......Tanga......ka alafu nchi wakawaachia............wakila bata.Maana kwa sasa hajulikani nzanzibar ni nani na mbara ni yupi eti kigezo dini,lugha na rangi.anyway rejeeni historia labda mtapata jibu.
 
Ndahani,
wanasema in the name of mercyful god huku wanachoma makanisa.
Makanisa yana uhusiano gani na muungano?
Issue siyo muungano, issue ni ukristo ndo hautakiwi zenji
Halafu watu wengi wanaofanya mambo ya hovyo hovyosiku hizi, wanapenda kunasema wanafanya in the name of merciful God! Mhh
 
Last edited by a moderator:
Ndahani,
wanasema in the name of mercyful god huku wanachoma makanisa.
Makanisa yana uhusiano gani na muungano?
Issue siyo muungano, issue ni ukristo ndo hautakiwi zenji
Kuufuta ukristu ni ngumu sana kama njia inayotumika ni hiyo ya kuua na kuharibu. Tutumie njia nyingine mbadala. Lakini kweli hatuwezi kuishi pamoja kama wakristu na waislamu? Kwanini tunamkumbatia shetani?
 
Makanisa yanahusika vipi na muungano? Hivi Shamsa Vuai ni mtanganyika? Kabla kuvunjwa kwa baraza la mawaziri si alikuwa waziri wa mambo ya ndani? manasema nini hili?Kuchoma makanisa Hilo halikubaliki kama ni muungano basi chomeni ofisi za ccm na serikali ya mapinduzi kuwa haziwasikilizi aheni mawazo finyu kama ya boko haram, el shabab
 
awali ya yote kwanza napenda kumsukuru mwenyezi mungu muumba mbingu na ardhi kwa kutufikisha siku kama ya leo tukiwa wazima na hata waliokua si wazima hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kila kitu.

Ningependa kuongea kwa niaba ya wazanzibari wenzangu na hata wabara pia na wote wanaopenda amani katika tanzania yetu hii..
Ni kipindi kirefu cc wazanzibari tulikua tunalia kuhusu huu muungano kua hautunufaishi sisi wazanzibari maana jambo lenye faida hua halilizi ila linafurahisha na ndio mana cc wazanzibari tunasema kua hauna faida kwetu sisi huu muungano.. Na sio kma hatuutaki muungano napenda niweke wazi kauli hii.. Kua muungano huu usiokua na faida kwetu sisi hatuutaki lau kama ungekua na faida kwetu wazanzibari tusingepiga kelele, ila tutapiga kelele hadi viongozi wetu watakapokubali kua tunakua na muungano wenye faida kwa nchi zote mbili..
Labda nirudi kidogo nyuma ya pazia la muundo wa serikali yenyewe..mna mm tokea napata akili zangu sijapata kusikia hata siku moja kusikia kua gavana katoka zanzibar,sijasiia hata siku moja kusikia kua mkuu wa jeshi la wananchi au jeshi la polisi kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia wakuuu wa necta kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia kua tanzanite itakua suala la muungano ila nachosikia kua mafuta ni ya muungano nk.. Na ndio mna nasema kua muungano huu hatuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

wewe ni hewa kabisa....kwani muungano upo kwenye secta gani na gani??? Au unakurupuka tu kama unataka kuhara...nyie mzigo sana hata wabara hawawazimiki vilevile sepeni kule....tena mapema mtuachie kariakoo yetu...mnaishi burebure huku af mnanyanyasa ndugu zetu kwenu....tokeni zenu
 
Kanisa la Anglikana lilianzishwa Zanzibar mwaka 1873 baada ya kufutwa kwa biashara ya utumwa, sasa hapa Muungano unaingiaje kuhusu uanzishwaji wa Makanisa Zanzibar?
 
Muungano kitu kingine kushirikishwa ktk uongozi kitu kingine kabisa! ushirikishwaji wa mafuta ya hadithi kitu kingine! Waislam wa Zanzibar nia yenu kijitawala kwa SHARIA au KUJIUNGA KUWA TAIFA LA IRAN? Vijana wetu wapo huko kunusa vitajulikana. Muhimu leteni hoja ktk mkondo sitahiki wala sikuchoma makanisa au kuchoma barabara! Huku bara hakuna hata mtumishi mmoja wa umma anayetamani kufanya kazi huko kwenu!
 
Vunjeni mungangano. Wale wapemba walioko Kyela kununua mpunga kipindi hiki hawatarudi tena Uzenjini kwenu. Tutawatumbukiza ndani ya mto songwe,kiwira na mmbaka.
 
Awali ya yote kwanza napenda Kumsukuru Mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Ardhi kwa kutufikisha siku kama ya leo tukiwa wazima na hata waliokua si wazima hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila kitu.

Ningependa kuongea kwa niaba ya wazanzibari wenzangu na hata wabara pia na wote wanaopenda amani katika Tanzania yetu hii..
Ni kipindi kirefu cc wazanzibari tulikua tunalia kuhusu huu Muungano kua hautunufaishi sisi wazanzibari maana jambo lenye faida hua halilizi ila linafurahisha na ndio mana cc wazanzibari tunasema kua hauna faida kwetu sisi huu Muungano.. Na sio kma hatuutaki Muungano napenda niweke wazi kauli hii.. Kua Muungano huu usiokua na faida kwetu sisi hatuutaki lau kama ungekua na faida kwetu wazanzibari tusingepiga kelele, ila tutapiga kelele hadi viongozi wetu watakapokubali kua tunakua na muungano wenye faida kwa nchi zote mbili..
Labda nirudi kidogo nyuma ya pazia la muundo wa serikali yenyewe..mna mm tokea napata akili zangu sijapata kusikia hata siku moja kusikia kua Gavana katoka Zanzibar,sijasiia hata siku moja kusikia kua Mkuu wa jeshi la wananchi au jeshi la polisi kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia wakuuu wa NECTA kutoka zanzibar, sijapata hata kusikia kua Tanzanite itakua suala la muungano ila nachosikia kua Mafuta ni ya muungano nk.. na ndio mna nasema kua muungano huu hatuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Dah kweli... maana hata mimi cjawahi kusikia rais/makamu wa rais wa zanzibar katoka bara na hilo hata silielewi kwa nini kwa kweli na wao wanakuwa makamu wa rais pamoja na vyeo vingine vikubwa kubwa.. Tanganyika yetu ni bora irudi tu kama ni mapenzi ya Mungu na zazibar ihamie uarabuni maana hao ndo wanawachanganya - mtumwa na mtwana. by the way hao wazenji wenyewe minyamwezi na misukuma na machinga kibao iliyokuwa mitumwa sasa wanajiona sijui ni waarabu?!! kweli waarabu wamewachanganya. Nasupport Tanganyika irudi lakini kama Mungu wa kweli anataka na si mungu wa kipagani...
 
Kanisa la Anglikana lilianzishwa Zanzibar mwaka 1873 baada ya kufutwa kwa biashara ya utumwa, sasa hapa Muungano unaingiaje kuhusu uanzishwaji wa Makanisa Zanzibar?

wamechanganyikiwa hawa jamaa... sio wao ni mapepo yao wanayoyatengeneza yamewachanganya.. badala ya kufata mkondo sahihi wao wanafanya fujo na huo ndo ushetani wenyewe na matokeo ya Rabdi (wao wanajua ni nini).... wanahitaji maombi kwa sana tu otherwise.....
 
Mkuu kisichotakiwa ni Makanisa, si Muungano! Hii vita dhidi ya Muungano ni vita isiyo rasmi dhidi ya Kanisa, get the point clear!

jee hii ilikuwa vita ya niniii???chini ya baba yenu wa taifa

Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza. Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini. Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar. Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini. Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu.

Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini."

Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini. Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia. Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini. Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza!

Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko. Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhaalimu ya Tanzania. Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere. Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa? Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini. Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo. Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere? Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini. Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda. Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika. Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.

Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada. Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama. Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo. Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni. Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini". Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani. Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika. Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa. Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika. Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma. Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.

Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba. Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara. Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza. Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula. Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo. Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso. Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma. Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo.

Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena. Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao. Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza. Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka. Lakinibasi, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhaahir shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani. Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani. Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.

Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake. Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu. Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu. Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu. Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda. Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.

Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?" Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake. Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao. Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao. Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa. Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa. Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.
 
Back
Top Bottom