Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

dala dala

Senior Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
106
Reaction score
105
Habari yenu Watanzania wenzangu,

Kila jambo na wakati wake kwa majira yake. Uchaguzi Mkuu unafanyika Oktoba, 2015 siku ya Jumapili. Si rahisi kubashiri nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais pengine tusubiri kuona nini kitatokea.

Mara baada ya tarehe 25 Oktoba tutakuwa na mjadala mpana juu ya Muundo wa Serikali ambayo Rais Mpya ataiunda. Nina mawazo ambayo ningependa Rais ajaye ayaweke katika fikra zake na kuyafanyia kazi. Nayo ni haya yafuatayo;

1. Serikali iliyopo ni kubwa mno na ufanisi ni Mdogo; hivyo afikirie kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kiwango kikubwa.

2. Muundo wa Utawala hauna tija

Ufafanuzi

1. Ukubwa wa Serikali
Kwa sasa kwa upande wa Tanzania Bara kuna Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wasaidizi wao. Kimsingi hawa wote kazi zao zinashabihiana. Hawa ni Wateule wa Rais na ni wawakilishi wa Taasisi ya Urais katika ngazi zao. Binafsi sioni kitu cha ziada na chenye manufaa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao kwa sehemu wanatumika kama Makada wa CCM. Ushauri wangu ni kuwa Cheo cha RC na DC kiondolewe tubaki na Watendaji ambao ni Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri. Tutaokoa fedha nyingi sana kwa hatua hii tu.

2. Muundo wa Utawala usio na tija
Tumekuwa na Wizara nyingi lakini ufanisi bado mdogo sana. Makusanyo ya kodi na wigo wa kodi bado ni mdogo, Tija katika sekta za uzalishaji bado ipo chini nk. Ushauri wangu ni kuwa na Wizara chache lakini zenye tija. Ninapendekeza Wizara zisizozidi 15 kama ifuatavyo;

1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

Hatuna sababu ya kuwa na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Halmashauri ziwajibike moja kwa moja kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS). Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha nyingi sana na kuwa na utekelezaji wa haraka. Kwa hiyo Elimu bure kwa wote, Afya bure kwa wazee, watoto na wajawazito inawezekana kabisa.

Aidha, Rais akasimu Mamlaka yake ya uteuzi. Si busara kila uteuzi ufanywe chini ya Ofisi ya Rais. Hali hii imesababisha kujikweza na kuwa na kiburi kwa baadhi ya wateule. Mfano RC hawezi kumfanya chochote RAS kwa kuwa Mamlaka ya Uteuzi ni Rais; Wakuu wa Mashirika hawawezi kuwajibika moja kwa moja kwa Waziri husika badala yake hata wakivulunda inasubiliwa Mamlaka ya Uteuzi kutengua Uteuzi. Huu ni urasimu na ni kuchelewesha maendeleo.

Ninashauri Serikali ijayo izingatie haya. Sisi ni nchi changa lazima tuwe na namna bora zaidi ya kutumia raslimali zetu kwa matokeo makubwa.

Asanteni kwa michango yenu wana JF.
 
Mkuu, hilo linawezekana kama Rais anaunda serikali ifanye kazi badala ya kulipa fadhila kwa watu. Wizara 15 ni muafaka kabisa.

La nyongeza, hakuna sababu ya kila wizara kuwa na Naibu Waziri. Ukweli wenyewe wengi huwa hawana kazi za kufanya zaidi ya kulipwa fadhila na Rais. Ikibidi kabisa, manaibu waziri wasizidi watano.
 
Nimeeipenda sana hiyo, Magufuli akiingia la kwanza ni kupunguza wizara ambazo hazina kichwa wala miguu kama ulivoonesha ndugu mleta mada
 
Nimeeipenda sana hiyo, Magufuli akiingia la kwanza ni kupunguza wizara ambazo hazina kichwa wala miguu kama ulivoonesha ndugu mleta mada

// WEWE unaye sema Magufuli - chukua hiyo hapo mpelekee tuone kama hata kura utapiga ( - Lumumba ipo wazi leo // Wahi usije ukasema wamefunga.
 
No 6 inapendeza ikiwa hivi:wizara ya afya na ustawi wa jamii,,no.9 isomeke wizara ya viwanda,biashata na masoko;
 
Naunga mkono mkuu, lakini angeongeza wizara moja ya mambo ya muungano. Pia manaibu wasiwepo. Tuwe na mawaziri 16 tu.
 
1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

JF.

16. Mambo ya Nje
17. Mambo ya Muungano

Mawaziri,Makatibu Wakuu, Ras na Wakurugenzi wa Miji,Manispaa na wilaya tosha!
 
Hata mimi pia nimeipenda,ina maono mapana na kwa maslahi ya nchi yetu,huu ndiyo mchango wa maana siyo ushabiki wa kitoto na bendera fuata upepo watu wamejichetua akili na ufahamu kiasi kwamba utadhani baada ya tarehe 25.10 hakuna maisha tena.
 
Umejitahidi ila mi naona ugumu kwenye wizara mbili:
Wizara ya ujenzi na uchukuzi zinaweza kuunganishwa ila zitahitaji budget kubwa kuliko wizara yoyote. Hizi zina mambo yanayoshabihiana. Ila wizara ua mawasiliano haipaswi kuungana nazo.

Kamq umefuatilia wagombea kila mahala wanapokwenda tatizo la maji ni number one. Hii wizara haipaswi kuunganishwa na wizara yoyote. Halafu hata ardhi ni wizara inayotakiwa kujitegemea kulingana na ukubwa wake.
 
Nimeeipenda sana hiyo, Magufuli akiingia la kwanza ni kupunguza wizara ambazo hazina kichwa wala miguu kama ulivoonesha ndugu mleta mada
Mkuu huna habari kuwa ccm walisha kataa mabadiliko hayo kwenye bunge la katiba?????
 
1. Wizara ya Fedha na Uchumi
2. Wizara ya MaliAsili (Maji Misitu, Utalii,Nishati na Madini,)
3. Wizara ya Mambo ya Ndani
4. Wizara ya Mambo ya Nje
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii
7. Wizara ya Kilimo, Mifugo,
8. Wizara ya Viwanda na Biashara
9. Wizara ya Sheria
10. Wizara ya Utamaduni
11. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
12. Wizara ya Elimu
13, Wizara ya Mipango na Maendeleo

Hakuna haja ya kuwa na Wizara ya Mambo ya Muungano kwa sababu ya mambo hayo kuwa chini ya wizara zitakazokuwa kwenye muungano.

Mikoa itapungua (Nashauri iwe kati ya 8 hadi 12) na itaongozwa na serikali za kuchaguliwa na watu wa mikoa hiyo na kuzigharimia.

Nyingi ya zinazoitwa wizara kwenye hili li serikali zinatakiwa kuwa idara. Ni matumaini yangu Katiba mpya itakuwa na Wizara za Kudumu
 
Mkuu, hilo linawezekana kama Rais anaunda serikali ifanye kazi badala ya kulipa fadhila kwa watu. Wizara 15 ni muafaka kabisa.

La nyongeza, hakuna sababu ya kila wizara kuwa na Naibu Waziri. Ukweli wenyewe wengi huwa hawana kazi za kufanya zaidi ya kulipwa fadhila na Rais. Ikibidi kabisa, manaibu waziri wasizidi watano.

Hilo la kuwandoa naibu mawaziri linahitaji mjadala kidogo kwa muundo wa sasa wa serikali na bunge. kumbuka waziri ndiye anayewajibika kuwasilisha na kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali zinazohusu wizara. Sasa endapo waziri hayupo bungeni kwa sababu yoyote ile atawakilishwa na nani? Kumbuka waziri au naibu waziri ni lazima uwe mbunge!
 
Mkuu huo ni upotoshwaji wa kazi za waziri uliofanywa makusudi na CCM. Mtendaji na mwenye majibu ya serikali ni katibu mkuu wa waizara. Waziri anawajibika kisiasa. CCM wameteka wajibu wa serikali na kuifanya serikali kuwa idara ya CCM.

Lazima mfumo ufumuliwe wote TUANZE UPYA tukiwa na machungu ya toka 1983 mfumo ulipouawa. Na 1977 CCM kuasisiwa na kuunganisha utendaji wa serikali na chama
 
Hilo la kuwandoa naibu mawaziri linahitaji mjadala kidogo kwa muundo wa sasa wa serikali na bunge. kumbuka waziri ndiye anayewajibika kuwasilisha na kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali zinazohusu wizara. Sasa endapo waziri hayupo bungeni kwa sababu yoyote ile atawakilishwa na nani? Kumbuka waziri au naibu waziri ni lazima uwe mbunge!

Waziri anaweza kuwakilishwa na waziri mwingine wa wizara yoyote. Je unajua kwamba Waziri akisafiri kaimu waziri anakuwa waziri mwingine na sio Naibu Waziri? Mara nyingi sana siku za nyuma Foreign Minister akisafiri, waziri wa sheria alikuwa akikaimu labda kwa kuwa walikuwa jengo moja wakati huo.

Isitoshe, Naibu Waziri haingii kwenye baraza la mawaziri hata siku moja. Katiba hairuhusu!
 
Back
Top Bottom