MUUNDO WA SERIKALI 3: CDM & CUF vs CCM MMEJIANDAAJE UCHAGUZI MKUU 2015

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,270
Rasimu ya pili ya Katiba mpya iliyotolewa na Judge Joseph Warioba imependekeza muundo wa serikali 3. Serikali ya shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar. Pia imependekeza uwepo wa Marais 3, Rais wa Muungano/shirikisho, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar. Hii ndiyo rasimu itakayopelekwa kwenye Bunge la Katiba kujadiliwa.

Ingawa CCM wanapinga uwepo wa Serikali 3, lakini kutokana na msimamo wa Wazanzibari wengi (CCM & CUF) ambao wanataka uhuru zaidi kwa nchi yao, hivyo inaelekea CCM wataacha vichwa ngumu na kukubali uwepo wa serikali 3. Sio nia yangu kuzungumzia faida na hasara za serikali 3. Hiyo ni maada ya siku nyingine.

Kama Bunge la Katiba litaridhia serikali 3, basi hiyo rasimu ndiyo italetwa kwetu Watanzania kwaajili ya kupigiwa kura ya NDIYO au HAPANA. Na kwa kuwa serikali 3 ndiyo angalau inaonekana kukidhi haja ya watanzania wengi, basi kuna uwezekano mkubwa rasimu hiyo ikapata > 50% ya kura za watanzania hivyo ikapita kama katiba mpya ya JMT.

Kwa kauli yake Mh. Rais Jakaya Kikwete anataka hiyo katiba mpya ndiyo itumike kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Maana yake ni kwamba Watanzania tutachagua Rais wa JMT, Watanganyika watachagua Rais wa Tanganyika na Wazanzibari watachagua Rais wa Zanzibar.

Hapa ndiyo linakuja swali langu?, Je vyama vya upinzani CDM na CUF dhidi ya CCM vimejiandaa je kwenye uchaguzi mkuu wa 2015? Ukitafakari vizuri, ingawa muundo wa serikali 3 unapingwa na CCM, lakini kisiasa unaweza kuwa na manufaa kwa CCM kutokana na makundi hasimu ndani ya CCM. Kwa kuwa CCM inafahamika kwa kupenda kulinda mshikamano ndani ya chama, serikali 3 inaweza kuwa fursa pekee kwa CCM kuendelea kuwa wamoja.

Mathalani kundi la Edward Lowassa linaweza kupewa nafasi ya Urais wa JMT. Na kundi la akina Samuel Sitta linaweza kupewa nafasi ya Urais wa Tanganyika. Hivyo tayari CCM itakuwa imetatua mpasuko uliopo ndani ya chama ambao una hatarisha kukimega chama vipande vipande. Ndio maana nikasema kwamba pamoja na muundo wa serikali 3 kupingwa na CCM lakini unaweza kuwa na manufaa kisiasa kwa CCM.

Sasa ngoja nizungumzie geopolitics za vyana vya upinzani CDM na CUF dhidi ya CCM Tanzania. CDM inao wafuasi wengi Tanganyika na tishio kwa mstakhabari wa CCM (ngome ya CDM ni Tanganyika), huo ndiyo ukweli. Lakini wakati huo huo CDM haina au inao wafuasi wachache sana Zanzibar. CUF inao wafuasi wengi sana Zainzibar (ngome ya CUF ni Znazibar), lakini wakati huo huo inao relatively wafuasi wachache sana Tanganyika.

Kwa Mkhutada huo CDM haiwezi kushinda kiti cha URAIS wa Zanzibar. Aidha Pia CUF haiwezi kushinda kiti cha URAIS wa Tanganyika. Lakini CDM inayo nafasi ya kushinda kiti cha Urais wa Tanganyika. Vile vile CUF inayo nafasi ya kushinda kiti cha Urasi wa Zanzibar.

Kuhusu kiti cha URAIS wa JMT ni CCM pekee ndiyo inayo nafasi ya kushinda kiti hicho. Kwanini nasema hivyo, lazima katika katiba mpya kitawekwa kipengele ambacho kitamtaka mgombea wa kiti cha Urais wa JMT kupata angalau asimilia fulani ya kura kutoka kila upande wa Muungano. Mathalani wanaweza kuweka clause inayosema pamoja na mgombea kupata kura nyingi lazima apate at least 1/3 ya kura halali za Zanzibar, ili kuchelea kutopata Rais wa JMT aliyechaguliwa na upande mmoja wa Muungano ambao ni Tanganyika yenye wapiga kura wengi. Mind you wapiga kura wote wa Zanzibar wanaweza kuwa sawa na majimbo mawili ya uchaguzi ya ubunge ya Tanganyika. Wale mnaofahamu vizuri uchaguzi wa Kenya ili uwe Rais wa Kenya lazima uwe umeshinda a certain namba ya majimbo ya Kenya.

Hivyo ni CCM tu inayoweza kutimiza sharti hilo. Sioni kama CDM inaweza kupata 1/3 ya kura za Zanzibar au CUF kupata popular vote za Tanganyika. Hivyo kama kweli vyama vya upinzani vinataka kuiondosha CCM madarakani. Karata yao ni moja tu, kuunganisha nguvu kwenye URAIS wa Tanganyika na Zanzibar. CDM isisimamishe mgombea URAIS Zanzibar na badala yake iiunge mkono CUF. Wakati huo huo CUF isisimamishie mgombea URAIS Tanganyika iiunge mkono CDM.

Kwa Mkakati huo CCM maji yatakuwa ya shingo itabaki na kiti cha URAIS wa JMT tu. Lakini kwa kuwa vyama vya upinzani vina ubinafsi, vyama vya CDM na CUF kila kimoja kinaweza kumsimamisha mgombea wa kiti cha URAIS wa JMT. Lakini hata kwa mtoto mdogo atajua kwamba vitakuwa vinamsindikiza CCM kwenye nafasi hiyo.

Mfumo wa serikali tatu unaweza kuleta mengi katika siasa za Tanzania. Hebu fikiria Rais wa JMT CCM, Rais wa Tanganyika CDM na Rais wa Zanzibar CUF!!
 
Back
Top Bottom