Muulizeni haya Maswali Mh. Lowassa

Muulizeni haya Maswali Mh. Lowassa

1. Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo familia yako inamiliki Uingereza. Ukasema ni ya mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu, ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?

2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je kwanini Mwalimu alikukataa?

3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama lakini wanatishiwa. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo? Je kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?

4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya ,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje kuhusu hili?

5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa, lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi zaidi. Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu?
Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatupa picha gani wananchi?

6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond, chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililoanyika?

7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa, ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao yote?

8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa Umma, una lipi jipya ambalo umelisahau, na sasa utalifanya katika huu urais wako unaougharamia kwa pesa nyingi?

9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona wafugaji bado masikini, na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?

10. Umetoa mchango gani kwenye bunge maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia yakipotoshwa na chama chako?


(itaendelea)
Hivi mbona makofili anamiliki kebbsy hotel pale bamaga kulala kwa siku 150,000 je nae alipata wapi hela ya kujenga hotel kubwa namna ileee????
 
Lowasa ✔✔✔
locks ❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌
 
I will live all my life I would ever have.. But there some people who deserve to die for others! Would u sacrifice yourself for others?
Maswali yako hayajaenda shule; nyumba kuchukuliwa na balozi from South Africa!!! Are u serious? The rumor about Baba wa taifa Mwal. Nyerere kumnyima hata uwaziri kwa Mh. Lowasa eti kwakuwa alifuja pesa!
Bi titi Mohamed, aliwahi kuonywa na nyerere kutumia fedha vibaya za umma.. Je, alishindwaje kumfunga Lowasa alipofuja pesa na wakati umesema mwenyewe alinyimwa hata uwaziri enzi za mkapa? Mbona unaibua some stupid accusation ambazo hata unapomuuliza mtu anashindwa akuambieje..
Kwa mfano mdogo, hebu muulize kikwete mimi ni muajiriwa wa serikali iweje mpaka sasa hajatoa mishahara kwa wafanyakazi wake mpaka sasa! Na umeme ameukata huku vijijini mpaka sasa mi naishije?
Na watu kama mimi tupo wengi mno.. Huku vijijini nilipo sasa hakuna hata mtu mmoja anapenda CCM..
Eti Lowasa anatuma picha akiwa na kikwete, so we have to ask 'em why!!? Are u.. I may have to see u maybe I'll get to know u better!
Si kama tunapenda kukiacha chama cha CCM kitape tape tunamuonea huruma mtu wa cite awe mwanasiasa.. Yule ni mtu wa kutumwa na kupangiwa (Magufuli) no way, he can't be president.. Not this year.. Let see after 20years..
We need to pursue further and further.. Mambo ya maisha bora na bado hakuna hata utu ktk maisha duni tulio nayo haifai.. Tena nahasira naweza nikakufuata ulipo!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

wafafanulie na richmond kamanda
 
Thinkers will choose Ukawa...time for change...mtatoka mapovu meeengi lakini haitasaidia...
Thinkers will never take ukawa serious. In fact, what is ukawa? Any legal instrument filed that defines ukawa?
 
Ni afadhali walioizoea hela wachukue nchi watapiga na kupuliza....kuliko akiingia masikini pale ikulu,watafakamia kama ilivyotokea hasa kwenye awamu ya tatu na nne...watanzania mmelogwa na mchawi amejinyonga!!!
 
Ni afadhali walioizoea hela wachukue nchi watapiga na kupuliza....kuliko akiingia masikini pale ikulu,watafakamia kama ilivyotokea hasa kwenye awamu ya tatu na nne...watanzania mmelogwa na mchawi amejinyonga!!!
Hii ndio sera ya ukawa.
 
alls great thinkers they can't votes chadema!!!!b'se ukawa is nonsense!!!!!plse tanzanians!we have to votes ccm candidate dr pombe maguful 4 changes!!to votes chadema is to votes mboye b'se his a last say!!lowasa ni msukule!!speechless
 
Back
Top Bottom