Muulizeni haya Maswali Mh. Lowassa

Muulizeni haya Maswali Mh. Lowassa

Vipi hotel ya mama kikwete iliyoko doha? Amepta wapi pesa za kujenga hotel kubwa?
 
Hivi mlitaka lowasa awe kapuku au mbona hata kwy kumi bora ya matijiri wa afrika tu hayupo? Acheni wivu. Umaskini sio sifa. Mkapa hana nyumba south afrika? Maccm ovyo kweli kisa kaama tu ndio gere. Watu wameelimika bwana poleni sana magamba
 
Thinkers will choose Ukawa...time for change...mtatoka mapovu meeengi lakini haitasaidia...
 
Huwa hawa jamaa hawayapendi maswali ya aina hii wanakurupuka na propaganda za mabadiliko wakatimhawana hoja wala mwelekeo kwa kifupi hawana KICHWA CHA HABARI wanakimbizwa na mkumbo kama nyumbu.
 
Huwa hawa jamaa hawayapendi maswali ya aina hii wanakurupuka na propaganda za mabadiliko wakatimhawana hoja wala mwelekeo kwa kifupi hawana KICHWA CHA HABARI wanakimbizwa na mkumbo kama nyumbu.

Umelenga penyewe Kiongozi
 
1. Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo familia yako inamiliki Uingereza. Ukasema ni ya mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu, ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?

2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je kwanini Mwalimu alikukataa?

3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama lakini wanatishiwa. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo? Je kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?

4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya ,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje kuhusu hili?

5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa, lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi zaidi. Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu?
Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatupa picha gani wananchi?

6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond, chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililoanyika?

7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa, ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao yote?

8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa Umma, una lipi jipya ambalo umelisahau, na sasa utalifanya katika huu urais wako unaougharamia kwa pesa nyingi?

9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona wafugaji bado masikini, na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?

10. Umetoa mchango gani kwenye bunge maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia yakipotoshwa na chama chako?

(itaendelea)

Mkuu tegemea mvua ya matusi kutoka kwa MANYUMBU
 
Hivi mlitaka lowasa awe kapuku au mbona hata kwy kumi bora ya matijiri wa afrika tu hayupo? Acheni wivu. Umaskini sio sifa. Mkapa hana nyumba south afrika? Maccm ovyo kweli kisa kaama tu ndio gere. Watu wameelimika bwana poleni sana magamba

Kwisha Habari yako. Kumbe mnapenda Ufisadi
 
Khaaa muulizeni na chenge basi... na ngeleja je.. na ridhiwani miaka 10 ya uongozi wa baba yake mali zote hizo mpaka vilima vya arusha na masheli baba yake angekaa miaka kumi na tano si angechukua mlima kilimanjaro
 
Hawawezi wameshapewa pesa za kwenda kununua peremende huwezi kuwashika, ngoja ziishe pale madukani utawaona.
 
Wewe jamaa unamawazo ya kimaskini na unapenda sana kila mtu awe anakuwa maskini kama wewe
 
Khaaa muulizeni na chenge basi... na ngeleja je.. na ridhiwani miaka 10 ya uongozi wa baba yake mali zote hizo mpaka vilima vya arusha na masheli baba yake angekaa miaka kumi na tano si angechukua mlima kilimanjaro

Uwiiii nimecheka sanaa
 
Khaaa muulizeni na chenge basi... na ngeleja je.. na ridhiwani miaka 10 ya uongozi wa baba yake mali zote hizo mpaka vilima vya arusha na masheli baba yake angekaa miaka kumi na tano si angechukua mlima kilimanjaro
Those you mentioned are not running for the highest office.
 
Back
Top Bottom