Muuguzi adaiwa kuua mjamzito, mapacha

Muuguzi adaiwa kuua mjamzito, mapacha

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
hospital-logo.jpg

HOSPITALI ya Serikali mkoani Shinyanga juzi ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kundi la wananchi kuvamia wodi ya wazazi, wakilalamikia uzembe uliofanywa na muuguzi kushindwa kutoa msaada kwa mwanamke aliyekuwa akijifungua na kusababisha kifo chake na watoto wake mapacha aliokuwa anajifungua.

Hali hiyo ilijitokeza saa 12 juzi jioni baada ya wazazi wa mjamzito huyo aliyekuwa akijifungua kulalamikia kitendo cha muuguzi aliyekuwa zamu katika wodi hiyo kutomsaidia binti yao mwenye umri wa miaka 15.

Kutojali kwa muuguzi huyo ndiko kunadaiwa kusababisha vifo vya watoto mapacha hao wawili na mama yao.

Muuguzi huyo anadaiwa kushindwa kumhudumia mjamzito huyo hata pale alipobembelezwa na wazazi wa mjamzito huyo, lakini yeye aliendelea kushughulika na simu yake ya kiganjani, akidaiwa kuwasiliana na watu wengine.

Kwa mujibu wa wazazi wa marehemu huyo, muuguzi huyo aliwajibu kuwa atamshughulikia baadae kwani alishamuona. Baada ya wananchi kupata taarifa hizo waliingia wodini kwa hasira.

Akizungumza kwa uchungu na waandishi wa habari, mama mzazi wa binti aliyejifungua, Mwanahamisi Juma, mkazi wa Mshikamano Manispaa ya Shinyanga, alisema awali binti yao alipelekwa Zahanati ya Kambarage kwa ajili ya kujifungua.

Baadaye alihamishiwa Hospitali ya Mkoa baada ya kubainika kuwa na tatizo. Mwanahamisi alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo saa sita mchana na kupokelewa na wauguzi ilipofika saa 10 jioni alishikwa na uchungu wa kujifungua na aliomba msaada kwa muuguzi aliyekuwa zamu ambaye hata hivyo hakumjali na badala yake aliendelea kuongea na simu yake ya kiganjani.

"Huyu muuguzi alitushangaza maana pamoja na mtoto wetu kuomba msaada ili asaidiwe aweze kujifungua salama, yeye hakuonesha kujali kabisa, aliendelea na shughuli zake za kuchati na simu yake ya mkononi, hali iliyotulazimisha tumfuate na kumlalamikia, hata hivyo alisema tumuache maana mzazi alikuwa akiendelea kusukuma,"alisema na kuongeza;

"Tulilalamika sana na hata baadhi ya wananchi wengine walikuja kutusaidia kumuomba muuguzi huyo amsaidie, lakini hakujihangaisha kabisa, hivyo tulitafuta msaada wa muuguzi mwingine aliyekuwa jirani ili amsaidie binti yetu, alifika na kutoa msaada hata hivyo watoto wote walikuwa wameishakufa," alieleza Mwanahamisi.

"Saa 10 mwanangu alianza kusukuma na kujifungua mtoto wa kwanza wa kike, lakini tayari alikuwa amefariki na muda mfupi baadaye alijifungua mtoto mwingine wa pili wa kiume naye hakuchukua muda pia, alifariki, kwa kweli tulisikitishwa sana na kitendo cha muuguzi huyo,"alisema Mwanahamisi.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Gibson Robert, mkazi wa mjini Shinyanga alielezea kushangazwa kwake na kitendo cha muuguzi huyo kushindwa kutoa huduma kwa mjamzito huyo na kusababisha vifo vya mapacha hao wawili na mama yao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Fredrick Mlekwa, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa alikanusha vifo vya mapacha hao kusababishwa na uzembe wa muuguzi na kwamba mimba hiyo ilikuwa haijatimiza muda wake wa miezi tisa hivyo kitaalam watoto hao wasingeweza kuishi kwa vile hawajakamilika.

"Ni kweli jana (juzi) palitokea tatizo katika hospitali yetu baada ya wananchi kuvamia wodi namba nane ambayo ni ya wazazi wakilalamikia kitendo cha muuguzi kushindwa kumsaidia mwanamke mmoja aliyekuwa akijifungua na kusababisha vifo vya watoto waliozaliwa," alisema Dkt. Mlekwa na kuongeza;

"Binafsi baada ya kupata taarifa hizo nilikwenda katika wodi hiyo na tulipofuatilia tulibaini kuwa mimba ya mjamzito huyo ilikuwa haijafikisha umri wa kujifungua kwani ilikuwa na umri wa miezi sita... mzazi mwenyewe alikiri muda huo na kitaalamu isingekuwa rahisi kwa watoto hao kuishi," alifafanua Dkt. Mlekwa.

Dkt. Mlekwa aliendelea kufafanua kuwa pamoja na maelezo ya mzazi mwenyewe kukiri umri wa ujauzito wake (miezi sita) walichunguza miili ya watoto waliozaliwa na kuipima ambapo mmoja alikuwa na uzito wa gramu 500 na mwingine gramu 700, hivyo kitaalamu walikuwa hawajakamilika kuitwa binadamu.

"Ni kweli tumefuatilia kuhusu suala la muuguzi wa zamu kuongea na simu, tumemuhoji amekiri muda huo alikuwa akiongea na simu na kufafanua kuwa alikuwa akiwasiliana na daktari wa zamu kwa ajili ya kuomba msaada zaidi wa kumsaidia mzazi huyo,"alisema na kuongeza kwamba suala hilo watazidi kulichunguza.

Dkt. Mlekwa amerejea kutoa wito kwa wakazi wa Shinyanga kuwa na tabia ya kuheshimu taratibu za hospitali zilizopo na kueleza kuwa ni kosa la kisheria kwa wananchi wa kawaida kuingia ndani ya wodi ya wazazi, hali ambayo inaweza kusababisha maambukizo mbalimbali kwa watoto wanaozaliwa kwa vile wanakuwa hawapatiwa chanjo za kinga.

CHANZO: Majira
 
Kiujumla kujifungua sio kifo ni kitendo cha furaha kusubiria kijacho kwa nchi za wenzetu lakini kutokana na siasa zetu chafu afrika kuingia mpaka kwenye utendaji wa kazi uzazi kwa nchi zetu ni pata potea kama kamari .
 
Inasikitisha sana. Huu ni ukatili kama inawezekana afukuzwe kazi na kupelekwa mahakanani iwe fundisho kwa wengine.

Kwa nini watu wanakuwa hawana hata chembe ya huruma na uhai wa wenzao. Kitakachoshangaza ni.kuwa hamna hatua yoyote ya kinidhamu itakayochukuliwa kuhusu huu ukatili.
 
Kwa serikali hii badala ya kumpa adhabu utashangaa wanamuhamisha kituo
 
nani atajali, mganga mkuu mfawidhi ameshaonesha kutojali, hii ni nchi ya wasiojali,kwa hiyo dada ataendelea kupeta kama kawa, pole sana wana familia
 
nani atajali, mganga mkuu mfawidhi ameshaonesha kutojali, hii ni nchi ya wasiojali,kwa hiyo dada ataendelea kupeta kama kawa, pole sana wana familia
muuguzi huyo ata angepokonywa simu,idhibitishwe na mitandao kama mda huu kwel alikuwa akiongea na daktar amsemaye
dokta huyo anatulaghai na maneno mepesi namna hii hiyo kama ni utetez wa uongo je.
nan anajal mwana wa maskin asipotendewa haki
 
Sasa miezi sita mlijua kabisa hao sio binadamu mkampokea na kumpeleka wodi ya wazazi halafu mkamwambia apush? Kweli?
 
Kiujumla kujifungua sio kifo ni kitendo cha furaha kusubiria kijacho kwa nchi za wenzetu lakini kutokana na siasa zetu chafu afrika kuingia mpaka kwenye utendaji wa kazi uzazi kwa nchi zetu ni pata potea kama kamari .

usisahau ni likatiba ndo hilo mnyamwezi keshawatupia
 
umri wenyewe miaka 15. anatakiwa awe shule! via vya uzazi bado havijakomaa! kwa kiherehere chake anafanya ngono tena bila kinga! mwisho lawama mnamtwisha nurse! acheni kujitoa fahamu! kemeeni umalaya utotoni unaoendekezwa na wazazi wenye njaa! mnawatesa wahudumu wetu kwa ujinga wenu! hata Rais alishasema ni viherehere vyao!
 
umri wenyewe miaka 15. anatakiwa awe shule! via vya uzazi bado havijakomaa! kwa kiherehere chake anafanya ngono tena bila kinga! mwisho lawama mnamtwisha nurse! acheni kujitoa fahamu! kemeeni umalaya utotoni unaoendekezwa na wazazi wenye njaa! mnawatesa wahudumu wetu kwa ujinga wenu! hata Rais alishasema ni viherehere vyao!


Mkuu wewe una watoto au ni bachela bado?
 
shy ndo zao
mi nilipelekwa AMANA mdada uchungu umemshika chooni anajibiwa hakuna nesi wa chooni nimesikia kwa masikio yangu mdada anajifungua mwenyewe nesi anafika mtoto ashatoka tena waliwaita wale wa field wa red cross
dada angu alimwambia nesi mwanangu akifa ntahakikisha mnawajibika anaenda mtoto kashatoa kichwa
tz uzazi anasimama MUNGU manesi wachache ndi o wastaarabu
 
Serikali yetu haijaweka kipaumbele kwenye mambo ya msingi kama afya na elimu,vipaumbele vimewekwa kwenye safari za raisi,ufisadi,ujangili na yanayofanana ba hayo,mimi ndio maana naona bora kutumia pesa nyingi kutibiwa private hospitals kuliko huko uchwara
 
Tukio Hilo Limenisababisha Nijawe Na Huzuni Kubwa Ya Kuondokewa Na Dada Yangu Ambae Aliugua Ugonjwa Wa Kisasa Mwaka 2010,mwananyamala akawa anatumia dozi,mimi mwenyewe nilikuwa nampeleka,kitengo cha ukimwi walituhudumia vzr sn,alikuwa na mtoto mchanga nae alihudumiwa vzr, kutokana na dawa alizokuwa anameza siku chache alidondoka saa 12 jioni ya ijumaa,akawa kama kapalalazi mdomo uliachama ukawa haufungi, ndipo nikamkimbiza mwananyamala hospital (siyo kitengo cha ukimwi kwa maelekezo waliokuwa wamenipa) huko wodini nilimkuta nesi Siwa, Ni Nesi Mwenye Roho Chafu Na Ndiye Aliyesababisha Kifo Cha Dada Yangu,nilimfata Zaidi Ya Mara Tisa Aje Amhudumie Dada Yangu Na Nikamweleza Hali Halisi Hakunijali Akasema Atakuja Hakuja,zaidi Ya Mara Tisa!! Nesi Huyo Na Kama Yupo Jamvini Mungu Ndiye Atamuonesha.Unyama Alionifanyia Atawafanyia Wengine Ngumi Mkononi Watamfundisha Adabu. Hata Hl Tukio La Shinyanga Na Mimi Ilikuwa Ni Hvy Hvy,unaenda Kumwita Anakwambia Anakuja Na Haji, Dr, Bingwa Kamtetea Huyo Nesi Muuaji.
 
Kwanza Huyo Anayejiita Dr Bingwa Wa Nini? Au Ni Dr Bingwa Wa Mazezeta? Mi Namuona Kama Zezeta Fulani, Kwa Dr.Makini Kwa Tendo Kama Hilo,huyo Nesi Alitakiwa Awe Ameshamsimamisha Kazi Na Uchunguzi Ufanyike Kwenye Mitandao Ya Sm Ili Kubaini Muda Huo Alikuwa Anaongea Na Sm Ya Nani Na Ilihusu Nini? Et Yeye Anasema Walimhoji Na Kukiri Kweli Alikuwa Anaongea Na Sm Ila Ni Ya Daktari!! Hv Alitegemea Amwambie Alikuwa Anaongea Na Hawara Yake? Hv Mwizi Alishawahi Kukiri Kweli Kaiba? MI NADHANI MH.WAZIRI ACHUNGUZE UHUSIANO WA KIMAPENZI KATI YA HUYO NESI NA HUYO DAKTARI,HUENDA HY SM ALIKUWA ANAONGEA NAE YEYE MWENYEWE HUYO DAKTARI NDO MAANA KAMRINDA, ILA MTAKUFA KIFO KIBAYA SANA,MLAANIWE,NAZUNGUMZA KWA UCHUNGU KWA SABABU NILISHAPOTEZA DADA YANGU KWA UFEDHURI WA HAWA MANESI.
 
umri wenyewe miaka 15. anatakiwa awe shule! via vya uzazi bado havijakomaa! kwa kiherehere chake anafanya ngono tena bila kinga! mwisho lawama mnamtwisha nurse! acheni kujitoa fahamu! kemeeni umalaya utotoni unaoendekezwa na wazazi wenye njaa! mnawatesa wahudumu wetu kwa ujinga wenu! hata Rais alishasema ni viherehere vyao!

kwani wote wanaopata matatizo wakati wa uzazi wanakuwa na miaka 15?

dah haya maneno yameniuma maana nimepoteza mtoto wakati wa kujifungua kwa sababu ya hizo hizo dharau za manesi
 
Huu uzembe upo mwingi sana, lkn kosa kubwa lilitokea pale walipoanza yale mambo ya mtu akifeli ndo anaenda kuwa nurse, so watu walienda kule kwa sababu kafeli na hana pa kwenda, wauguzi wengine hata ukiangalia sura zao wamekaa kikatili katili sana..
 
shy ndo zao
mi nilipelekwa AMANA mdada uchungu umemshika chooni anajibiwa hakuna nesi wa chooni nimesikia kwa masikio yangu mdada anajifungua mwenyewe nesi anafika mtoto ashatoka tena waliwaita wale wa field wa red cross
dada angu alimwambia nesi mwanangu akifa ntahakikisha mnawajibika anaenda mtoto kashatoa kichwa
tz uzazi anasimama MUNGU manesi wachache ndi o wastaarabu
Kuna nurses wengi sana wanachangia huduma za afya kuwa mbovu tz..
 
Kwanza Huyo Anayejiita Dr Bingwa Wa Nini? Au Ni Dr Bingwa Wa Mazezeta? Mi Namuona Kama Zezeta Fulani, Kwa Dr.Makini Kwa Tendo Kama Hilo,huyo Nesi Alitakiwa Awe Ameshamsimamisha Kazi Na Uchunguzi Ufanyike Kwenye Mitandao Ya Sm Ili Kubaini Muda Huo Alikuwa Anaongea Na Sm Ya Nani Na Ilihusu Nini? Et Yeye Anasema Walimhoji Na Kukiri Kweli Alikuwa Anaongea Na Sm Ila Ni Ya Daktari!Hv Alitegemea Amwambie Alikuwa Anaongea Na Hawara Yake? Hv Mwizi Alishawahi Kukiri Kweli Kaiba? MI NADHANI MH.WAZIRI ACHUNGUZE UHUSIANO WA KIMAPENZI KATI YA HUYO NESI NA HUYO DAKTARI,HUENDA HY SM ALIKUWA ANAONGEA NAE YEYE MWENYEWE HUYO DAKTARI NDO MAANA KAMRINDA, ILA MTAKUFA KIFO KIBAYA SANA MLAANIWE NAZUNGUMZA KWA UCHUNGU KWA SABABU NILISHAPOTEZA DADA YANGU KWA UFEDHURI WA HAWA MANESI.Hv Kama Ingekuwa Ni Sm Ya Daktari Ya Kuomba Msaada Zaidi Si Angewajibu Ndugu Wa Huyo Mgonjwa Kuwa Nawasiliana Na Daktari Ili Atoe Maelekezo,Haya Mbona Nesi W Wodi Ya Jiran Alienda Akatoa Msaad Yeye Alishindw Nini?Huyo Nesi Na Huyo Daktari Ni Mt Na Hawara Yk
 
Kazi ya kuzalisha sio ya nesi ni kazi yamkunga (midwife} hawa manesi ndo wale hata mtoto akitanguliza mkono wao wanavuta tu.
 
Back
Top Bottom