Story Room
Member
- Nov 27, 2020
- 56
- 147
MUUAJI MWENYE BARAKOA - 29
Sultan Uwezo
+255
"Kwangu wewe ni sawa na Maadui wengine Catherine, kuna kitu ambacho ulikuwa hukijui bila shaka mama bibi yako hakuwahi kukueleza vizuri juu yangu. Mimi naitwa Malick Bolenge sina undugu hata chembe na koo yako tambua hilo. Miaka kadhaa huko nyuma wazazi wangu walikuwa 'family friend' na familia ya mama yako ukaribu wao pamoja na ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kifamilia zilipelekea watu kujua ni ndugu.
Hawakukosea kuwaza hivyo hata ungekuwa wewe ungefikiri hivyo hivyo lakini kitumbua kiliingia mchanga miaka kadhaa baadaye baada ya baba yangu kufariki huko nchini Togo kwa kushambuliwa na Chui akiwinda kwenye Kitalu chake. Msiba huu ulikuwa pigo kubwa sana kwangu na mama yangu sijamtaja mdogo wangu ambaye alikuwa mdogo kwa wakati huo na hii ilikuja baada ya babu yako kutupora Mali zetu zote kwa kushirikiana na Kampuni moja ya Kuuza Vinyago nchini Afrika ya Kusini.
Alifanya hivyo baada ya kuahidiwa kupewa makazi na kazi nzuri lakini wapi Mungu hulipa hapa hapa duniani kwani baada ya nyaraka kukamilika na kuwa mikononi mwa Kampuni hii walimtafutia kesi na kumtupa gerezani huko huko Afrika ya Kusini pasipo familia ya mama yako kujua mpaka pale mama yako alipotoka kijijini ambako bibi yako alikimbilia kuficha aibu na kuja mjini ambako alijiunga na Kanisa la Mchungaji Rodney Hauser na kuanza kutumikishwa katika Shuhuda mbalimbali ambazo hazikuwa za uongo na huu ulikuwa ni mpango wangu ambao niliupandikiza pasipo mtu yeyote ndani ya hilo Kanisa lenu kujua maana ilikuwa ni Ahadi ambayo nilimpa marehemu mama yangu kuwa nitalipa kisasi kwa familia ya mzee Kiyosa.
Unataka kujua nini kilifuata kwenye simulizi hii yenye Uchungu? Usiwe na haraka utajua siku ukinikaribia maana naiona bidii yako ya kunisaka." Baada ya kumaliza kusimulia mkasa huu mzee Malick Bolenge alikata simu na kumfanya Catherine kubaki kaitolea macho simu yake. Kitendo kile kilishuhudiwa na Jumbe ambaye alimfuata na kumuuliza.
" Kuna usalama Bosi?"
" Usijali niko poa Jumbe." Alimjibu akiikagua namba iliyotumiwa na mzee Malick Bolenge.
"Una uhakika Bosi? Mbona nakuona hauko sawa?" Jumbe aliendelea kumuuliza.
"Jumbe si kila kitu nitakuambia kuna mengine natakiwa kuyamaliza mwenyewe." Alimjibu na kutoka nje ambako aliingia moja kwa moja kwenye gari na kufunga mlango kisha akaiwasha laptop yake na kuiingiza namba yake kutaka kujua ni namba gani iliyompigia muda huo ambayo iliingia kwa mfumo wa 'private number' lakini hakuambulia chochote akaona isiwe shida akachukua simu yake na kumpigia rafiki yake Uriah Kombo anayefanya kazi ndani ya Kampuni fulani ya mawasiliano na kuongea naye.
"Hi sweetie!" Alimuanza baada ya kupokea simu.
"Maajabu yaani leo umenitafuta dada yangu Catherine tena usiku? Mmh hebu niondoe huu wasiwasi." Uriah Kombo alimjibu akiwa kwenye sauti iliyojaa usingizi mwingi.
"Hebu achana na hayo mdogo wangu najua ni miezi kibao imepita hatujaongea lakini kuna kaupepo kananipitia 'all in all' tuko pamoja." Catherine alijitetea.
"Nimekuelewa dada yangu nipe habari." Uriah alimuelewa.
"Kuna mtu kanipigia simu muda si mrefu na kuniambia mambo yasiyoeleweka hivi kisha akakata simu na nilivyojaribu kumtafuta nikakutana na 'private number' hivyo nahisi mtu huyu hana nia nzuri na mimi na ndiyo maana katumia namba mficho, hivyo katika hili nikaona nikutafute mdogo wangu unisaidie kumsaka." Catherine alimweleza kile ambacho alipanga kumueleza.
" Mmhh mbona ni jambo zito hilo dada, kwanza pole sana na sijui nifanyaje ukizingatia niko nje ya ofisi.. " Uriah alimjibu.
" Hilo nalijua mdogo wangu lakini kwa kuutambua uwezo wako ukiwa kama 'genius' nikajua lazima utafanya jambo hivyo naomba usiende kinyume na mawazo yangu tafadhali."
"Okay sawa dada yangu hebu nipe kama dakika kumi na mbili hivi nifanye kitu fulani hivi ambacho kinaweza kutusaidia kupata namba ya mtu huyo."
"Nitashukuru sana mdogo wangu maana kanichanganya sana kwani masaa kadhaa nyuma nilimnasa kupitia namba yake ambayo kaiondoa mtandaoni na hivyo kunipoteza kwenye signo yangu ambayo nahisi aliishtukia." Catherine aliongeza.
"Atapatikana tu mpaka sehemu alipo." Uriah alimjibu.
"Naomba nikuache uifanye kazi yangu." Catherine alimjibu na kukata simu kisha akawasha gari na kuondoka. Aliendesha gari kama kichaa na hii ilitokana na simu ya mtu ambaye siku zote huamini ni mjomba wake.
" Haiwezekani najua kaamua kusema hivi ili kunichanganya zaidi lakini nikijuacho yeye ni kaka yake marehemu mama yangu. Lakini pamoja na undugu huu lazima nimuoneshe mimi na yeye tupoteza kuaminiana."Aliendelea kuwaza. Alipofika barabara kuu inayoelekea mji wa Abuja aliachana nayo na kuishika ile inayoelekea 'Bamboo Street' ambako kuna makazi ya watu mbalimbali wanaotokea mataifa mengine. Akiwa ndiyo anaishika barabara hiyo akiwa mwendo wa kawaida kabisa mara ilipita pikipiki moja kwa mwendo wa kasi na kwenda kusimama mbele yake na kumfanya ashindwe kuendelea na safari ikabidi asimame na kushusha kioo.
"Oyaa ndiyo nini tunazuiana?" Alimfokea kijana huyo aliyekuwa kavalia nguo za kiraia akiwa anaongea na simu huku anamfuata, na badala ya kumjibu alimpa tu ishara ya kushuka. Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa Catherine akaona achukue tahadhari kabla ya kutoka nje hivyo akachukua bastola yake na kisu kimoja kisha akajiweka sawa na kushuka.
"Tufahamiane tafadhali." Alimwambia baada ya kushuka.
"Una maana gani kusema hivyo?" Yule kijana aliyekuwa hana wasiwasi wowote japokuwa ilikuwa ni usiku alimuuliza.
"Huoni kama ni usiku kiasi hiki halafu unauliza, nahitaji kufahamu nimesimamishwa kuna tatizo gani na wewe ni nani pia."
"Kiufupi mimi ni Askari Doria wa eneo hili na nimekusimamisha baada ya kukutilia mashaka." Alijitambulisha.
"Kunitilia mashaka kivipi? Siruhusiwi kutembea usiku maeneo haya?" Catherine alimuuliza.
"Dada yangu kumshakia mtu hakumaanishi amevunja sheria tunachofanya ni kutimiza majukumu yetu tu hivyo unachotakiwa muda huu ni kusubiri utaratibu wetu na iwapo itaonekana huna kosa lolote lile tutakuachia tu." Alimjibu kisha akamtaka amkabidhi ufunguo wa gari.
Catherine alimuangalia kwa muda kijana huyo kisha akaipapasa bastola yake ambayo alitaka kuitoa lakini kuna wazo lilimuijia akaamua kuacha na kuitoa funguo mfukoni na kutaka kumkabidhi lakini akasita kidogo.
" Naomba kitambulisho chako kwanza nijiridhishe usije ukawa Kanjanja." Alimwambia kijana huyo ambaye bila kusita alitoa kitambulisho na kumkabidhi Catherine ambaye baada ya kukikagua alimkabidhi ufunguo.
"Naomba na kitambulisho changu si tayari umekiangalia."
"Nimekiangalia lakini bado nina mashaka na wewe hivyo usiwe na wasiwasi nitakupa tu." Alimjibu.
"Unajua wewe dada unachekesha sana kwa hiyo nikiamua kukufanyia kitu chochote kibaya hicho kitambulisho kitakusaidia nini maana utakuwa ni mfu." Kijana huyo ambaye ni Askari wa Doria alimjibu akicheka.
"Nawajua sana ninyi Maaskari wa usiku mnashirikiana na Wahalifu kwa kiasi kikubwa japo si wote hivyo tahadhari ni muhimu." Catherine alimwambia.
"Tuachane na hayo umetokea wapi na unakwenda wapi muda huu?" Catherine aliulizwa.
"Sasa muda wote ulikuwa wapi kuuliza maswali ya msingi tunabaki kupotezeana muda tu hapa, mimi nielekea mjini kufurahi na wenzangu nilikotoka ni kwenye hicho Chuo." Alimjibu akimkabidhi kitambulisho.
"Kwa hiyo wewe unasoma pale St. Marino University?" Alimuuliza baada ya kukiangalia kitambulisho.
"Ndiyo niko pale." Alimjibu akiwa kamkazia macho.
"Wanachuo wa siku hizi hakuna masomo ni Umalaya na Starehe tu." Alimwambia akimrudishia kitambulisho chake.
"Kwa hiyo wewe ni nani mpaka useme hayo? Maisha yetu Wanafunzi yanakuhusu nini wewe?" Alimsogelea na kumuuliza.
"Au nimekugusa kwenye ukweli mbona unakuwa mkali?" Badala ya kujibu alimuuliza.
"Achana na mimi wewe shika yako."
"Isije kuwa tabu bure hebu shika funguo yako nipe kitambulisho changu nenda kalambwe na mijibwa ya usiku." Askari huyo alimwambia Catherine akimpa ufunguo.
"Yaani mijitu mingine sijui inakuwaje? Kwa hiyo wewe inakuhusu nini mimi kwenda kulambwa na hiyo Mijibwa?" Catherine alimuuliza akiivuta funguo yake na kisha alimrushia kitambulisho chake na kuingia garini.
"Nenda huko wewe Malaya unajiona mzuriii mwenyewe." Askari huyo alimwambia Catherine akiwa anapandisha kioo. Catherine aliishia kumuangalia tu huku akimbetulia midomo na kuondoka zake huku macho yakiwa kwenye 'site mirror' mpaka alipoona yuko umbali wa kutosha ndipo akasimamisha gari na kujishika kifuani.
"Mwanaharamu huyu sijui kanipandisha presha kiasi cha kutaka kuanguka chini kumbe anaongea pumba tu." Catherine alijisemea mwenyewe kisha akawasha gari na kuondoka tairi za gari lake ziliingia mpaka ndani ya kituo cha mafuta kiitwacho 'NADHIFA PETROL STATION' na kusimama. Alitulia hapo bila kushuka mpaka pale alipokuja mhudumu wa kituo hicho ndipo aliposhusha kioo na kutoa kichwa nje.
"Habari yako dada." Alimsalimu.
"Salama karibu kwa huduma." Alimkaribisha.
"Naomba niwekee lita kumi na saba hapo." Alimwambia akiuruhusu mfuniko wa tenki ufunguliwe na mhudumu huyo. Alifungua akamuwekea kiasi hicho cha mafuta na kisha akaufunga mfuniko na kumfuata Catherine.
"Sijui nimepatia kwa kiasi hicho?" Catherine alimuuliza.
"Mmh ni sahihi na hapa kuna baki yako natakiwa nikurudishie." Alimjibu akizihesabu.
"Ok nashukuru naomba kiasi hicho ubaki nacho wacha mimi niondoke." Catherine alimjibu na akiwasha gari.
"Asante dada yangu na karibu tena." Mhudumu aliagana na Catherine aliyekuwa analiacha eneo la kituo hicho cha mafuta. Alirudi barabarani na kuendelea na safari yake na akiwa anawasha Muziki mara simu iliita na alipoangalia mpigaji alikuwa ni Uriah akatabasamu na kuipokea.
" Niambie Uriah." Catherine alianza.
"Sorry kwa kukuchelewesha lakini haikuwa kwa ubaya ilikuwa ni katika kufanikisha kazi yako." Uriah alimwambia.
"Wala usijali kikubwa kama umefanikiwa tu."
"Nashindwaje Mtaalamu wako." Alimjibu.
"Si ndiyo nilitaka kushangaa yaani wewe ushindwe?"
"Haiwezekani hiyo dada, nimeshaipata namba ya huyo haramia nakutumia sasa hivi." Uriah alimjibu.
"Yaani kati ya vitu ambavyo umenifurahisha siku ya leo ni hilo mdogo wangu, Nakushukuru sana tena sana kwa ulichonifanyia sina cha kukulipa zaidi ya kumuachia Mungu." Catherine alimjibu.
"Tuko pamoja dada yangu na pia usisite kunishirikisha kwa kila jambo ambalo utahisi linahitaji msaada wangu." Uriah alimwambia Catherine ambaye alikuwa mwenye furaha sana muda huo.
"Unanijua vizuri ndugu yako kwenye hilo wala usijali ." Catherine alimjibu kisha akakata simu na hii ni baada ya kuiona pikipiki ikiwa nyuma inakuja hivyo akahisi anaweza kuwa ni yule yule Askari wa Doria.
"Hivi huyu anataka nini tena kwangu? Au anaitaka roho yangu?" Catherine aliongea akiifuatilia ile pikipiki kwenye 'site mirror' ambayo ilikuwa ikisogea taratibu alipokuwa.
JE NI NINI KITATOKEA KATIKA KITIMUTIMU HIKI?
TUKUTANE KATIKA SEHEMU INAYOFUATA.
Sultan Uwezo
+255"Kwangu wewe ni sawa na Maadui wengine Catherine, kuna kitu ambacho ulikuwa hukijui bila shaka mama bibi yako hakuwahi kukueleza vizuri juu yangu. Mimi naitwa Malick Bolenge sina undugu hata chembe na koo yako tambua hilo. Miaka kadhaa huko nyuma wazazi wangu walikuwa 'family friend' na familia ya mama yako ukaribu wao pamoja na ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kifamilia zilipelekea watu kujua ni ndugu.