Sijui, lakini pengine ni kujisahaulisha tu. Kwani akina Mwigulu Nchemba historia zao zipoje?
Binafsi naona uteuzi wa aina hii kwa wakati huu ni kama fursa nzuri kwa nchi yetu.
Kama unayo mashaka, au huelewi ninachozungumzia usisite kutafuta ufafanuzi.
Tusiwe wepesi wa kulaani tu kila mara, panapostahili pongezi kwa aina yoyote ile, iwe nzuri au mbaya tusisite kuwapongeza hawa watawala wetu.
Mimi nauona uteuzi huu kuwa wa manufaa kwa mwelekeo wetu kama taifa. Tukishindwa, tusilaumu tu wengine, tujilaumu sisi wenyewe tuliokosa kutumia fursa tuliyopewa kuitumia ipasavyo.
Labda nikuulize: ulitaka ateuliwe mtu wa aina gani ndipo ufurahie?