Zikomo Songea
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 670
- 580
Leo hii ukizungumzia nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo hawezi kuacha kuitaja Japani. Lakini iliwezaje kufikia hatua hii? Historia inasema nini kuhusu maendeleo ya Japani? Nitazungumzia kiufupi.
Hadi kufikia miaka ya 1850, Japani ilikuwa si lolote katika maendeleo ikilinganishwa na nchi kama Uingereza, Ujerumani na Marekani. Uchumi ulikuwa duni, idadi ya watu ilikuwa ni ndogo na ukabaila (feudalism) ulikuwa ndio mfumo mkuu wa uzalishaji mali. Kiufupi, mfumo wa kubepari ulikuwa bado.
Mabadiliko makubwa katika uchumi wa Japani yalianza mwaka 1867 chini ya mtawala aliyeitwa Mutsuhito (au Meiji). Huyu alileta mabadiliko mengi ambayo yalikuwa msingi wa Japani ya Kisasa. Alikomesha ukabaila na kuanza kuhodhi madaraka ya kisiasa ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijijini.
Pia aliwapeleka maofisa wake Ulaya Magharibi na Marekani ili kujifunza taasisi za kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia kwa lengo la kuharakisha maendeleo. Alifunga pia mabadiliko makubwa ya kijeshi kwa kuanzisha kikosi cha majini (navy), kutoa makundi rasmi kwa maofisa wa jeshi na kuanzisha utaratibu wa kujiunga na jeshi kwa mujibu wa sheria (hii aliiga kutoka jeshi la Ujerumani).
Mutsuhito hakuishia hapo. Aliweka misingi idara ya maendeleo ya viwanda akiiga mifukoni ya viwanda vya Kisasa kutoka Uingereza, Ujerumani na Marekani. Chini ya utawala wake mapenzi yalianzishwa ili kutoa mikopo kwa viwanda, reli zilijengwa kuunganisha nchi nzima, migodi ikafunguliwa na kilimo kikaboreshwa na kuwa cha kibiashara.
Chini ya utawala wake Wizara ya Viwanda ikaundwa mwaka 1870, na elimu ya ufundi ilipanuliwa sana. Kufikia mwaka 1900, tayari Japani ikawa kati ya mataifa yaliyoendelea sana duniani.
Maendeleo haya yote yalitletwa katika kipindi cha takribani miaka 30 tu! Tukitaka tujifunze kwao pia.