Muswaada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswaada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Dec 22, 2009.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ofisi ya waziri mkuu imetoa kwenye gazeti la Daily News la leo , kwa taarifa ya wananchi, miswaada miwili inyotegemewa kuletwa bugeni, nadhani kwa minajili ya uchaguzi mkuu ujao wa wabunge na madiwani.

  Miswada hiyo ni ule unaokusudia kufanya marekebisho katika sheria ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vile vile sheria ya Gharama za uchaguzi, ( ambayo ni mpya)

  Pamoja na mambo memngine katika muswada wa kwanza kuna vitu vingi vya msingi ambavyo vimepigiwa kelele lakini haviwekwa kwenye marekebisho kama vile:
  1. Wagombea binafsi uraisi ubunge na udiwani.

  2. Haki ya watanzania wenye miaka 18 walio nje ya nchi kuruhusiwa
  kupiga kura.

  3. Kupunguza nguvu za tume ya uchaguzi.

  Kwa upande mwingine muswada wa pili umesahau kubainisha nini kitafanyika kwa wagombea kutumia rasilimali za serikali wakati wa uteuzi na kampeni.

  Tatu taarifa imetolewa kwenye gazeti ambalo linasomwa na watanzania wachache sana sijaona kwenye magazeti ya kiswahili ni nini kinafichwa????

  Mwenye uwezo wa kutuwekea miswada hiyo jamvini afanye hivyo ili wananchi waujadili kwa kina kabla haujapelekwa bungeni na kuwa sheria
   
Loading...