Nimekuwa nikifuatilia siasa za chama cha mapinduzi kwa ukaribu sana na kwa miaka mingi nimegundua yafuatayo.
1,Wanafiki,wanasiasa wengi waliomo ndani ya chama hiki ni wanafiki sana,wanajua kuyaongelea ya wengine na kuyaacha yaliyomo ndani ya chama chao,mfano,kwa miaka mingi kulikuwapo na watuhumiwa wa ufisadi katka nchi hii lakini hakuna hata mmoja amewahi kusimama hadharani na kuwataja fulani na fulani mnatuharibia nchi,mfano Chenge,Thibaijuka,Rostam Azizi,Lowasa,na wengine kibao na hadi juzi waliotajwa kwenye ripoti ya makenikia tofauti na musukuma,wabunge wa ccm wengine wamejitoa akili kana kwamba hawawajui waliotajwa,badala yake wanakomaa na wapinzani kana kwamba wapinzani ndo wametajwa na kamati ya osoro,
2,Hawataki kuwa wazi,wanasiasa wengi wa chama hiki,na wengine waliomo ni madokta na maprofesa lakn kwenye ukweli hawataki kusema ukweli,hujitoa akili kwamba linalofanyika hawalijui hivyo hadi kuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa,mfano,bajeti kwa asilimia kubwa huwa hazitekelezeki,badala yake profesa anasimama bungeni anapongeza bajeti kwa kutotekelezeka ,kwel wabunge wa ccm badala ya kuisimamia serikali,muonyeshe ukali kwa kutotekelezeka kwa bajeti hadi serikali ilete majibu yanayoeleweka,badala yake naunga hoja asilimia mia,siyo siri hii nchi haijitambui
Pongezi ziende kwa waheshimiwa hawa wawili,
Musukuma, amethubutu kusema sisi ccm ndo tunafuga wezi,amejitambua hadi na kuwataja,MTU kama Ulega hajitambui anachokifanya anakijua mwenyewe
Pongezi pia zimwendee Bashe,mhe anachangia kwa fact,anaikosoa serikali,hajatumwa kuipambia serikali,anataka serikali ifanye kazi,huwa namkubali sana mh kwenye michango yake,
Ushauri ,Wabunge wa ccm acheni kuipambia serikali,ibane serikali ifanye kazi,huku mtaani hali ni mbaya haijawahi kutokea,wanafunzi kujiunga na elimu ya juu ni shida,watanzania wanashindia uji,nyie pigeni meza lakini siku zenu zinakuja,halafu hawa wabunge wasichokijua ni kuwa,wakiibana serikali,wananchi hawatakuwa omba omba kwa wabunge,maisha yao yatakuwa mazuri,pia mjue serikali haina shukurani hata siku moja,serikali inakutambua wakati ukiifanyia kazi au kama uko hai kwa mbali kidogo,kufa uone,mazishi watafanya halafu wakiondoka,wala hawatajua kwamba familia yako ikoje,kwa hiyo unapoisimamia serikali kwa umahiri na serikali ikafanya kazi,maisha kwa familia yako yatakuwa mazuri,kwa familia ,jamii inayo kuzunguka na Taifa,
Ccm acheni kuliangamiza Taifa