Musukuma, kwanini unataka Hayati Dkt. Magufuli asisemwe?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Kwa mara ya Kwanza tunashuhudia watu wakimlinda aliyekuwa Rais wa nchi kiongozi wa umma asizungumziwe. Tulishuhudia akina Christopher Mtikila RIP wakimsema vibaya Mwl. Nyerere RIP bila watu wa Musoma na Butiama kuwajia juu wale wanaomsema mtoto wao, baba Yao na mtu wao. Mbona safari hii ni tofauti sana kwa JPM?

Katika nchi ya kidemokrasia kama yetu kumsema mtu aliyekuwa kiongozi wa umma ni sehemu ya demokrasia yetu. Mpaka Leo wanasemwa akina Hitler lakini sio kweli kwamba Hitler hakufanya kitu kizuri hata kimoja kwa wajerumani. Watu wanamsema idd Amini lakini sio kweli kwamba Amini hakufanya jema hata moja kwa waganda. Mobutu, Banda, nk hivyohivyo.

Mbona ni haramu safari hii kusema ubaya wa JPM kama ulikuwepo na waliouona ubaya huo wapo?

Hizi ni dalili mbaya kwa taifa ambazo taifa lingezipata kama JPM angeendelea kubaki madarakani. Demokrasia ilifutwa awamu ya Tano, na Kuna dalili kuwa huenda makubwa yalikuwa yalifike taifa kwenye nyanja ya demokrasia. Musukuma na wenzake huenda walikuwa wanafahamu nini kilikuwa kinaenda kutokea kwenye demokrasia yetu.

Kama JPM alifanya mazuri matupu wacha wale walioyaona hayo mazuri matupu wawapuuze ambao wanamsema vibaya JPM, kwanini waliokuwa rafiki zake ndio wazuie waliotendewa vibaya wasiseme?

Huu ni ushamba, ulimbukeni na udikteta katika uongozi. Wanataka kuitia kwapani demokrasia yetu. Tusiruhusu upuuuzi huu uote mizizi na kukomaa kwenye taifa letu.

Mazuri na mabaya yote yalikuwepo, mabaya tuyazungemze hadharani ili yasirudiwe na watawala wajao. Hata Hitler wanazungumzia mabaya yake ili fundisho kwa vizazi vijavyo.

Taifa liwe huru watu kutoa tathimini zao katika kila mwisho wa awamu kwa lengo la kuboresha ambayo hayakutugurahisha na yaliyotuumiza kama taifa ili yasirudiwe tena.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom