Mustafa R. J. Sabodo ni nani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,832
Naomba tusaidiane kumfahamu kwa undani zaidi huyu Mgeni Mzalendo kuliko wazalendo wenyewe.
Nasikia mdosi hajawahi kukwepa kodi tangu enzi za Nyerere, na bado huwa anatoa mapesa kuisaidia serikali.
 
Shemeji wake Lord Rajpar(mmiliki wa meli iliyoleta sakata wakati ule wa Kambarage & Rashidi)
 
Sikumbuki siku wala tarehe kamili
ambapo serikali ya awamu ya kwanza
ilinishinikiza kurudishwa kwa meli ya M.V
Ruvu mikononi kwa serikali baada ya
kuuzwa kwa mfanyabiashara Akberal
Rajpar kwa bei sawa na gari pijoti
faivuofoo (Peugeot 504)-hapa nimetia
chumvi kidogo kwa makususdi. Meli hii
iliuzwa kwa mizengwe na kugeuzwa jina
kuitwa M.V. Lord Rajpar.
Sakata la M.V. Lord Rajpar lilisimamiwa
kidedea na serikali ama kwa uchungu wa
kitaifa au kwa shinikizo la serikali ya
China ambayo ndiyo iliyokuwa mwekezaji
mwenza katika Shirika la Meli la Tanzania
na China (SINOTA_SHIP). Meli ya M.V. Ruvu
si tu kama ilirudishwa bali wahusika
katika kasheshe hilo waliwajibishwa ama
kwa kufukuzwa kabisa kazi au
kushushwa vyeo. Nadhani baada ya
sakata la M.V. Ruvu ndipo aliyekuwa
Waziri Mkuu wa wakati huo Ndugu
Rashid Mafaume Kawawa alipoondolewa
madaraka ya uwaziri Mkuu na kuwa
Waziri Asiye na Wizara Maalumu na
aliyekuwa Waziri Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Marehemu Edward Sokoine
alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa
Waziri Mkuu Marehemu Sokoine
aliendeleza mapambano na walanguzi na
wahujumu uchumi. Mwaka 1982 au 83
akaendeleza mapambano na walunguzi
na wahujumu uchumi.
Sambamba na kuuzwa kwa M.V. Ruvu
palitokea tena hujuma ya ununuzi wa
ndege mbovu Boeng 737 toka
mfanyabiashara wa Kilebanoni George
Hallack. Sakata hili nalo tulishuhudi
kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa
wakati huo Ndugu Mwingira pamoja na
maofisa wengine wa serikali na wa
Shirika la Ndege la Tanzania.
Ninachota kusema hapa ni kwamba tabia
ya kujihujumu hatujaianza leo: ilikuwepo
na ipo na nisingependa kubashiri
kwamba itaendelea kuwapo.
Ninachosema ilikuwepo na katika serikali
ya kwanza ilikuwa ikichukuliwa hatua
kali.
 
COULD someone tell us more about Lord Rajpar,cause there was a timehuyu jamaa ruled the air waves in tanzania


Sikumbuki siku wala tarehe kamili
ambapo serikali ya awamu ya kwanza
ilinishinikiza kurudishwa kwa meli ya M.V
Ruvu mikononi kwa serikali baada ya
kuuzwa kwa mfanyabiashara Akberal
Rajpar kwa bei sawa na gari pijoti
faivuofoo (Peugeot 504)-hapa nimetia
chumvi kidogo kwa makususdi. Meli hii
iliuzwa kwa mizengwe na kugeuzwa jina
kuitwa M.V. Lord Rajpar.
Sakata la M.V. Lord Rajpar lilisimamiwa
kidedea na serikali ama kwa uchungu wa
kitaifa au kwa shinikizo la serikali ya
China ambayo ndiyo iliyokuwa mwekezaji
mwenza katika Shirika la Meli la Tanzania
na China (SINOTA_SHIP). Meli ya M.V. Ruvu
si tu kama ilirudishwa bali wahusika
katika kasheshe hilo waliwajibishwa ama
kwa kufukuzwa kabisa kazi au
kushushwa vyeo. Nadhani baada ya
sakata la M.V. Ruvu ndipo aliyekuwa
Waziri Mkuu wa wakati huo Ndugu
Rashid Mafaume Kawawa alipoondolewa
madaraka ya uwaziri Mkuu na kuwa
Waziri Asiye na Wizara Maalumu na
aliyekuwa Waziri Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Marehemu Edward Sokoine
alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa
Waziri Mkuu Marehemu Sokoine
aliendeleza mapambano na walanguzi na
wahujumu uchumi. Mwaka 1982 au 83
akaendeleza mapambano na walunguzi
na wahujumu uchumi.
Sambamba na kuuzwa kwa M.V. Ruvu
palitokea tena hujuma ya ununuzi wa
ndege mbovu Boeng 737 toka
mfanyabiashara wa Kilebanoni George
Hallack. Sakata hili nalo tulishuhudi
kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa
wakati huo Ndugu Mwingira pamoja na
maofisa wengine wa serikali na wa
Shirika la Ndege la Tanzania.
Ninachota kusema hapa ni kwamba tabia
ya kujihujumu hatujaianza leo: ilikuwepo
na ipo na nisingependa kubashiri
kwamba itaendelea kuwapo.
Ninachosema ilikuwepo na katika serikali
ya kwanza ilikuwa ikichukuliwa hatua
kali.
 
Back
Top Bottom