GE2025 Mussa Zungu: Rais Samia ametoa Bilioni 200 ujenzi Mfumo mpya wa maji taka Ilala

GE2025 Mussa Zungu: Rais Samia ametoa Bilioni 200 ujenzi Mfumo mpya wa maji taka Ilala

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Hawa wazee wa CCM wakubali tu wamechoka maana wakienda bungeni watajikuta wanasaini mikataba ya kutuuza kabisa

Zungu jamani kweli ndo kuzuia maji taka kuua samaki barabarani au ndo mradi mpya wa CCM wa makazi mapya ya samaki😕 waachieni wenye afya na nguvu imara ya kuongoza nchi mkalee wajukuu

Hizo fedha na mradi ukute ni uongo ndo maana Aweso kasahau kuongelea

-------------
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Azzan Zungu wakati wa Mkutano wa Kampeni za Rais Samia ambaye pia Mgombea Urais kupitia CCM, leo Oktoba 22, 2025 Kinyerezi, Ilala Dar Es Salaam kwenye Viwanja vya Kecha, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mgombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imetoa jumla ya shilingi Bilioni 200 kwaajili ya usimikaji wa miundombinu mipya ya Majitaka ndani ya Jiji la Ilala ili kuzuia majitaka hayo kuelekezwa baharini kama ambavyo ilikuwa awali

Kulingana na Zungu, tayari mkandarasi yupo kwenye eneo la kazi akiweka miundombinu mipya ya Majitaka kutoka Gymkhana, Malick road, Upanga, Jangwani Sekondari, Mchikichini mpaka buguruni, lengo likiwa ni kuliweka Jiji hilo pia katika hadhi sahihi sambamba na kuyatumia maji taka hayo kwaajili ya kilimo mara baada ya kuwa yamesafishwa

Zungu pia amezungumzia changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Ilala, akisema chanzo cha tatizo hilo imekuwa ni ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka Mkoani Dar Es Salaam, akiwaomba wananchi wa Kivule, Ukonga, Segerea, Ilala na Kinondoni kuendelea kuwa na subira katika kipindi hiki kifupi cha utatuzi wake.

"Tukubali kero hii lakini nina habari njema DAWASA chini ya Aweso usiku na mchana wanahangaika kuhakikisha maji yanarudi na Niipongeze DAWASA kwa namna wanavyojitoa kuhakikisha kero hii inaisha. Nawaomba watu wa Kariakoo, Upanga, Kisutu, Kivukoni, Ilala, Jangwani na Mchikichini, Maji yameanza kutoka, tuwe na uvumilivu." Amesema Zungu.

Katika hatua nyingine Zungu amemshukuru Rais Samia kwa kuamua kuuendeleza mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar Es Salaam maarufu kama DMDP, akisema mradi huo umekuwa chachu ya ujenzi wa miundombinu katika Jimbo na Wilaya ya Ilala


 
Mna Rais tajiri sana Watanzania! Ametoa wapi hizo bilioni 200 na hii hali mbaya ya uchumi!
 
Back
Top Bottom