Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Muda mfupi baada ya mfanyabiashara Peter Zakaria kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya kujaribu kuua, Jeshi la Polisi limewasilisha na kupata kibali cha kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake mjini Tarime.
Waandishi wa Mwananchi waliopiga kambi katika viunga vya Mahakama ya Hakimu mkazi mjini Musoma wameshuhudia mfanyabiashara huyo tajiri akipandishwa ndani ya gari aina ya Land-cruiser tayari kwa safari ya kwenda nyumbani kwake mjini Tarime kwa ajili ya upekuzi.
Mjini Tarime, Waandishi wengine wa Mwananchi wameshuhudia mfanyabiashara huyo akiingizwa nyumbani kwake Barabara ya Nyamwaga akiwa ndani ya gari iliyokuwa ikisindikizwa na magari kadhaa yakiwemo mawili yaliyojaa askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU), waliojihami kwa silaha na zana za kiulinzi.
Mapema leo asubuhi Julai 5, Zakaria alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili ya kujaribu kuua.