Kwanza lazima uwe na Kompyuta yako binafsi,mf Laptop,au hata Desktop yenye uwezo mkubwa (Program nyingi za Music Production ni Kubwa).Pili tafuta(omba,nunua) Program za Qubase,Au Fruitloops au kwa kuwa unaanza siyo mbaya ukaanzia kuitumia Hip Hop E -Jay, baadae ukishazizoea hizo program anza kutembelea studio mbali mbali, usiogope masimango au dharau, (kwani ndo tabia ya 'Maprodyuza' wengi wanaojiona wako juu).Halafu usikifiche kipaji chako,onesha ulicho nacho popote inapotokea nafasi.Kila kitu kizuri kina usumbufu wake.Kwa Arusha watafute watu kama Nah Reel(Pah One) au John B(John Blaze) au Maproducer wadogo wadogo unaweza kutimiza ndoto yako ukijituma.All the Best