Museveni aitisha kikao kujadili uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Museveni aitisha kikao kujadili uchumi

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Aug 5, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Rais Yoweri Museveni ameitisha kikao cha dharura cha mawaziri kujadili jinsi ya kukabili nhali mbaya ya uchumi nchini humo.
  [​IMG] Viongozi wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kudorora kwa uchumi


  Baraza hilo la mawaziri linakutana katika kipindi ambacho viongozi wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kupanda kwa gharama za maisha.
  Bidhaa muhimu kama vile sukari zimeanza kukosekana madukani hali ambayo inawaathiri watu wenye kipato cha chini nchini humo.
  Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema bei ya sukari imepanda kiasi kwamba kile kiasi kilichoko aidha kinafichwa ama kuniauzwa bei kali ambayo sio ile ya kawaida.
  katika maduka makubwa watu hawakubaliwi kununua zaidi ya kilo moja.
  Hali hii inatishia uchumi wa taifa ambao kwa sasa kwa mujibu wa gavana wa benki kuu ya taifa kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Uganda kitadidimia kwa asili mia 5 kutokana na kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei za bidhaa.
  Mfumuko wa bei unakaribia asili ia 20, kiwango kikubwa zaidi kwa kipindi cha maiaka 10.
  Pia kiwango cha ubadilishanaji wa pesa za Uganda kwa dola kumepanda kiasi kuwa dola 1 inanunua shilling za Uganda 2,634.
  Msemaji wa serikali na waziri wa habari bi Mary okurut amesema kikao hicho maalum cha mawaziri kitajadili mikakati ya kukabili hali hii ya uchumi.
  Kuhusu kutoweka kwa sukari madukani, waziri Okurut amesema kuwa serikali imeomba ruhusa kutoka jumuiya ya Afrika mashariki ikubaliwe kuagizia sukari kutoka nje ya ukanda huu.
  Uganda ina viwanda vitatu vinavyozalisha sukari, lakini ni kimoja tu kwa sasa kinachofanya kazi.
  Viwili vilivyosalia, kimoja kimefungwa kwa sababu mitambo yake inafanyiwa ukarabati ilhali kingine kwa kuwa hakipati miwa inayotosheleza uzalishaji.

   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Museven = Monduli = Magamba!! Sera zile zile, aina ile ile ya uchakachuaji! Walifanya madhambi mengi mno mwaka jana wakati wa uchaguzi, na walitumia pesa nyingi sana kuingia madarakani!! shida nyingine waafrika tutazitafuta wenyewe bila kujiuliza kwa nini!!
   
 3. K

  Karry JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  sukari muhimu sana kuagiza ss hivi mpaka kibali cha EAC?
   
Loading...