Museven umepotoka kulaani bila kufuata taratibu azimio la mwendesha mashtaka wa ICC kuichunguza Burundi

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,642
2,000
Kulaani azimio la kumwelekeza mwendesha mashtaka wa ICC kuichunguza Burundi si hoja kuu, bali umelaani bila kufuata taratibu tunadhani Museven angepaswa kuzifuata.

Angeitisha kikao cha wanajumuiya ya Afrika Mashariki kisha wajadili jambo hilo na matokeo ya mjadala ndio mwenyekiti Museven angeutangaza hadharani.
Tamko la Museven halina uhalali wa kisiasa kuwa wana Afrika Mashariki tunalaani uchunguzi wa kijinai Burundi.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,921
2,000
Burundi watu wanafanyiana unyama hawa Wakuu wanataka icc wakae kimyaa tu!
Haya ni maajabu mengine ya dunia

Ova
 

momaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
423
500
Sidhani kama ICC inafanya kosa kuchunguza! Kwanini viongozi wa afrika hatutaki kuchunguzwa!?? Hivi ni kosa kuchunguza jinai kama imifanyika au la. Nilitegemea kama viongozi wangesema uchunguzi uendelee ili ukweli ufahamike!!???
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,642
2,000
Sidhani kama ICC inafanya kosa kuchunguza! Kwanini viongozi wa afrika hatutaki kuchunguzwa!?? Hivi ni kosa kuchunguza jinai kama imifanyika au la. Nilitegemea kama viongozi wangesema uchunguzi uendelee ili ukweli ufahamike!!???
Kwa serikali yenye kufuata utawala wa sheria wangeukaribisha uchunguzi huu kwa mikono miwili.

Wanalaani kuchunguzwa kanakwamba wao ni malaika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom