Museven hata wewe?

Museven hata wewe?

Nikikumbuka Rais Kaguta Museveni ameishi hapa Tanzania kwa kipindi kirefu
Kwanza wakati akisoma hapa UDSM
Pili wakati akiwa katika harakati za kumng'oa Idd Amin Dada. Huyu alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mwl Julius Kambarage Nyerere, bila shaka hata yeye alimpenda sana Mwalimu kwani aliunga mkono jitihada zake za kuikomboa Uganda. Museven amekuwa na ndoto za kuja siku moja kuwa Rais wa kwanza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili aje atawale Afrika Mashariki inabidi awepo madarakani hadi hapo akichaguliwa, hii imebidi ageuke kama dictor nchini kwake kwa kitendo chake cha kubadilisha vipengele vya katiba ili kumwezesha azidi kuwepo madarakani. Hilo sisi kama Watanzania halituhusu.

Kilichonisukuma kuandika "Museveni hata wewe?" ni ubaridi wa mahusiano tunaouona toka kwa Mh. Yoweri Kaguta Museveni dhidi yetu Watanzania, ameungana na vijana wadogo kumpiga mawe "Baba yake Mlezi". Tanzania ni Baba mlezi wa Rais Museveni kwani alizaliwa kiakili akiwa UDSM, ikawa asubuhi ikawa jioni Mwl Nyerere akaone ni vema akamwambia Museveni inuka mwanangu nenda hadi nchi nitakayo kuonyesha yaani Bukoba, nenda ukapige kambi hapo ukabiliane na hasimu wako Idd Amini, Museveni akaitikia ndiyo Baba, akafunga safari kuelekea Bukoba. Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini.

Aliweza hatimaye kumkabili akisaidiwa na Mwalimu hadi kumng'a Idd Amini Dada, akaiongoza Uganda hadi leo. Sisi Watanzania hatuwezi kuamini kama naye ameungana na vijana kuihujumu Tanzania kwa kuitenga katika nyanja na harakati za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama ndivyo basi hakika naungana na manabii wa kale waliosema "Shukrani ya punda ni mateke" Ni mateke kwanini kisiwe kichwa. Museveni umetugeuka kwa lipi sisi Watanzania??? Waache hao vijana wacheze makida makida kwa muda halafu wataelewa nini Tanzania ilivyo, wewe ungana na sisi rudi nyumbani mwa Baba yako Mlezi, Tanzania!!!

"Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini."
Na katika vijana wake aliowachukua na kuwaleta walikuwamo akina Kagame. Sasa anakabiliwa na tatizo awakane vijana wake au baba yake!
 
Huu upuuzi wote wa hivi vinchi vidogo vidogo umeletwa na CCM kushindwa kusimamia Uchumi imara bila utegemezi kushinndwa kuikemea RUSHWA Mungu ametupa nchi Yenye kila kitu utajiri mkubwa wa Rasilimali CCM imeshindwa Kuendeleza Bandari ya Dar Es salaam imeshindwa kujenga Reli ya kati hivyo vyote ni Muhimili wa uchumi imekalia longolongo tu Waachezi watutenge Udhaifu wa CCM ndio matunda yake haya
 
Watu wanasema Mda ni jaji mzuri, acheni kupiga kelele, waacheni wafanye watakalo. Tujikiteni ktk tamaduni zenye kuheshemu kazi na miiko ya kazi.

shirikisho halina faida yoyote mara nyingi ni hasara tu. Nchi zilizo ktk EU wana matatizo makubwa kuliko nchi ambazo hazimo EU kama vile Switzerland, Norway nk. Hata UK wanampango wa kupiga kura kujitoa EU. Na angalia hizi nchi zinapata msukomsuko wakati viongozi wake wanafuata miiko ya kazi.

Tupigeni makofi kwa kushangilia kwamba ni wao wenyewe wameamua kututoa, sioni cha kusikitika hapo zaidi ya furahaa. Furahieni na mpige vigelegele
 
Kumtetea JK inabidi uwe na roho ya chuma. Hasa nikikumbuka vijana wa JK walipofanya mambo ya ovyo kwa Mwangosi,Arusha,Morogoro,Mtwara na Ulimboka na mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa wahusika zaidi ya Usanii.Sipendi kuwa mzalendo wa kinafiki.
 
Nikikumbuka Rais Kaguta Museveni ameishi hapa Tanzania kwa kipindi kirefu
Kwanza wakati akisoma hapa UDSM
Pili wakati akiwa katika harakati za kumng'oa Idd Amin Dada. Huyu alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mwl Julius Kambarage Nyerere, bila shaka hata yeye alimpenda sana Mwalimu kwani aliunga mkono jitihada zake za kuikomboa Uganda. Museven amekuwa na ndoto za kuja siku moja kuwa Rais wa kwanza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili aje atawale Afrika Mashariki inabidi awepo madarakani hadi hapo akichaguliwa, hii imebidi ageuke kama dictor nchini kwake kwa kitendo chake cha kubadilisha vipengele vya katiba ili kumwezesha azidi kuwepo madarakani. Hilo sisi kama Watanzania halituhusu.

Kilichonisukuma kuandika "Museveni hata wewe?" ni ubaridi wa mahusiano tunaouona toka kwa Mh. Yoweri Kaguta Museveni dhidi yetu Watanzania, ameungana na vijana wadogo kumpiga mawe "Baba yake Mlezi". Tanzania ni Baba mlezi wa Rais Museveni kwani alizaliwa kiakili akiwa UDSM, ikawa asubuhi ikawa jioni Mwl Nyerere akaone ni vema akamwambia Museveni inuka mwanangu nenda hadi nchi nitakayo kuonyesha yaani Bukoba, nenda ukapige kambi hapo ukabiliane na hasimu wako Idd Amini, Museveni akaitikia ndiyo Baba, akafunga safari kuelekea Bukoba. Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini.

Aliweza hatimaye kumkabili akisaidiwa na Mwalimu hadi kumng'a Idd Amini Dada, akaiongoza Uganda hadi leo. Sisi Watanzania hatuwezi kuamini kama naye ameungana na vijana kuihujumu Tanzania kwa kuitenga katika nyanja na harakati za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama ndivyo basi hakika naungana na manabii wa kale waliosema "Shukrani ya punda ni mateke" Ni mateke kwanini kisiwe kichwa. Museveni umetugeuka kwa lipi sisi Watanzania??? Waache hao vijana wacheze makida makida kwa muda halafu wataelewa nini Tanzania ilivyo, wewe ungana na sisi rudi nyumbani mwa Baba yako Mlezi, Tanzania!!!

Kumbuka Julius Caesar pigo la mwisho kisu na lililommaliza lilitoka kwa rafiki yake Brutus. There is no way we should be trusting Mseven!!
 
Tujifunze kusaidia watu na huu ukarimu wetu mungu aliotupa leo unatucost ila inauma najua rais wetu nae anaumia inamaana kutukanwa na kagame labda ndio ilikuwa mpango wao wote, tujitoe mungu atatusaidia tu pia walivyotutenda sisi nao yatakuja kuwatokea watagombana wenyewe kwa wenyewe
Mkuu mbona majeshi ya M7 na Kagame waliwahi kupigana vikali huko Congo, mahusiano yao si rahisi kuyaelewa - nasikia kuna wakati M7 na Kagame walikuwa hawa pikiki chungu kimoja, walikaa zaidi ya nusu mwaka bila ya kujuliana hali!! Watanzania tutegemee nini kutoka kwa such an odd PAIR ambao wako highly unpredictable.
 
Back
Top Bottom