Museven hata wewe?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,548
Nikikumbuka Rais Kaguta Museveni ameishi hapa Tanzania kwa kipindi kirefu
Kwanza wakati akisoma hapa UDSM
Pili wakati akiwa katika harakati za kumng'oa Idd Amin Dada. Huyu alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mwl Julius Kambarage Nyerere, bila shaka hata yeye alimpenda sana Mwalimu kwani aliunga mkono jitihada zake za kuikomboa Uganda. Museven amekuwa na ndoto za kuja siku moja kuwa Rais wa kwanza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili aje atawale Afrika Mashariki inabidi awepo madarakani hadi hapo akichaguliwa, hii imebidi ageuke kama dictor nchini kwake kwa kitendo chake cha kubadilisha vipengele vya katiba ili kumwezesha azidi kuwepo madarakani. Hilo sisi kama Watanzania halituhusu.

Kilichonisukuma kuandika "Museveni hata wewe?" ni ubaridi wa mahusiano tunaouona toka kwa Mh. Yoweri Kaguta Museveni dhidi yetu Watanzania, ameungana na vijana wadogo kumpiga mawe "Baba yake Mlezi". Tanzania ni Baba mlezi wa Rais Museveni kwani alizaliwa kiakili akiwa UDSM, ikawa asubuhi ikawa jioni Mwl Nyerere akaone ni vema akamwambia Museveni inuka mwanangu nenda hadi nchi nitakayo kuonyesha yaani Bukoba, nenda ukapige kambi hapo ukabiliane na hasimu wako Idd Amini, Museveni akaitikia ndiyo Baba, akafunga safari kuelekea Bukoba. Mwalimu Nyerere akaona ni vema ikawa jioni ikawa asubuhi Mwalimu akamwambia Museveni chukua vijana wako wa uzao wako walete hapa kambini Bukoka nao wawe pamoja nawe wakipata mafunzo pamoja nawe kumkabili hasimu wako Idd Amini.

Aliweza hatimaye kumkabili akisaidiwa na Mwalimu hadi kumng'a Idd Amini Dada, akaiongoza Uganda hadi leo. Sisi Watanzania hatuwezi kuamini kama naye ameungana na vijana kuihujumu Tanzania kwa kuitenga katika nyanja na harakati za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama ndivyo basi hakika naungana na manabii wa kale waliosema "Shukrani ya punda ni mateke" Ni mateke kwanini kisiwe kichwa. Museveni umetugeuka kwa lipi sisi Watanzania??? Waache hao vijana wacheze makida makida kwa muda halafu wataelewa nini Tanzania ilivyo, wewe ungana na sisi rudi nyumbani mwa Baba yako Mlezi, Tanzania!!!
 
Tujifunze kusaidia watu na huu ukarimu wetu mungu aliotupa leo unatucost ila inauma najua rais wetu nae anaumia inamaana kutukanwa na kagame labda ndio ilikuwa mpango wao wote, tujitoe mungu atatusaidia tu pia walivyotutenda sisi nao yatakuja kuwatokea watagombana wenyewe kwa wenyewe
 
Babu msemaovyo kilio chako kimenikumbusha mbali zamani sana, Kilio kama hicho cha hata wewe aliwahi kulia Mtawala wa ROMA Julius Caesar akimlilia mshirika wake wa ndani kabisa aliyekuwa anamwamini bwana Marcus Junius Brutus,siku anauwawa tarehe 15 March 44 BC jioni ile kati ya wauwaji wake alimwona huyo bwana Brutus neno lake la mwisho kabla hajafa ndio kilio hicho "HATA WEWE BRUTUS. Basi mambo ya usaliti hajaanza Mseveni yameanza siku nyingi, huwa wanasema hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
 
Hawezi achana na vijana hao maana wote interest yao ni moja - huko DRC.

TZ kupeleka jeshi kulinda amani huko DRC kunawavurugia mambo yao - si unaona tayari M23 yameshaua mwanajeshi wetu huko?
 

Ardhi ya Tanzania walioitaka sana pindi tungekubali kipengele cha ardhi kuwa huru kwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumilikishwa imewauma sana. Kwetu sisi tutulie kama tulivyo, hakuna marefu yasiyo na ncha.

Nashukuru sana Mkuu ebaeban kwa maelezo mazuri ya kihistoria ambayo yanaashiria kwamba hata kabla Yesu Kristo usaliti ulikuwepo tena nadhani huo ulikuwa usaliti wa kikatili sana, maana angalau huu wa Museveni unahuruma kiasi maana anajificha sura kwa pama lake.
 
Tatizo sisi waafrika wote akili zetu zimeinama, kila kiongozi anachotaka apate maslaha yake mwenyewe. Tumepewa uhuru lakini hakuna hata kiongozi hata mmoja wa kiafrika anayeitetea nchi yake kwa maslaha
 
Wanamuonea wivu kwa sababu jk hafungamani na upande wowote. Anahudhuria mikutano ya g8,un,etc sasa wao kutwa wamo 2 kwenye nchi zao nialiko kidogo ya kwenda nje
 
Chamuhimu tudumishe amani. Kuna nchi nyingi tu wanaona wivu kwa amani yetu, meza mmoja utaona makabila 5 tofauti wamekaa pammoja na kufurahi na vinywaji vyao kitu ambacho nchi zingine si rahisi kutokea. Amani na maendeleo inaleta maendeleo wache wao wa twangane
 
Simlaumu mseveni, KIKWETE amejisahau sana, kila siku yeye ni kiguu na njia tuu mara ulaya, mara asia mara marekani, hatumsikii akifanya ziara ya kikazi kenya, uganda au burundi na rwanda. Wakati wenzie wakitembeleana, yeye ni kujipendekeza tu kwa white people. Mtu wa namna hiyo unategemea watamfanyaje?? anafurahia coridor za Wazungu kiliko rest room za waafrica wenzie.

Kama jirani yako kila siku anashinda mtaa wa saba, kwako haji, akitembelewa na watu wake wa mtaa wa saba anakutambia weee,Huduma unazopata kwake mbovu..utafanya nini??? UNAACHANA NAE NA KUUNGANA NA WENYE NIA KAMA YAKO..FAST JET anatulostisha SANAAAAAAA.
 

Waache waende ma dikteta Kagame na Museveni,namuhurumia Kenyatta anavyoingizwa mkenge kwa kisingizio cha East African "integration"


Mu7 Siku zake za kutawala Uganda zimekwisha anajiandaa kupandikiza mwanae,Kagame yeye siku yoyote atakapotembeza
sanduku la kura ataanguka.Ndio maana tuligundua hila zao mapema hauna viongozi wa maana pale
 
Mleta uzi sikia, kama ningelikuwa M7 ningelijiweka ktk nafasi hiyo aliyohamua kujiweka no matter what Tanzania did for him! Tanzania ya sasa imepadilika sana....wewe unajua what has been going around since Mwl died....Lakini pia ktk mlinganyo wa haki, 'interests' za M7 ktk Congo ni kubwa kuliko alizonazo Tanzania. Nashauri waTanzania wahache kuendeshwa na mhuemko wa uzalendo na badala yake waongozwe na hekima na busara kwa kila jambo zaidi ktk masuala yenye faida. Kabla yakuingilia migogoro yoyote razima tupime faida na hasara za kujiingiza kwetu.
 

Wote tunamawazo kama yako na tungependa tuendeleee hivyo but.....ishara zinaonesha hali hiyo si muda mlefu itatoweka: Ukabila, udini, utaifa (unyarwanda, utanzania, ututsi, uhutu, uhindi....)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…