MURO TRANS, laacha barabara na kupinduka mara tatu

habari nzuri ila imejaa chumvi! kwa hali ya kawaida basi lenye mwendo kasi likianguka mara tatu haliwezi kuwa kama linavyoonekana kwenye picha. Labda limeanguka mara tatu kwenye magodoro likiwa kwenye mwendo kasi wa kinyonga!
 
kutoka stendi nyegezi - mkolani/buhongwa ni kama 1 km sasa uyu dereva sijui alipata wapi huo mwendo within 1km mpaka ashindwe kulicontrol bus. Tulisha yajadili haya mabasi siku chache zilizopita nikiwamo mimi mchangiaji wa ile mada
 
Poleni sana abiria;

Kumbukumbu zangu zinasema kuwa kuna mada ililetwa hapa kuhusu haya mabasi ya MURO TRANS tulisha yajadili hapa kuwa ni mabovu. Sasa leo yametokea mengine haya kwa uzembe wa dereva. Huenda na ubovu wa basi nao umechangia.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Kweli kabisa, niliyeleta mada ni miye, wengine wakanipuuza kwa kuona kwamba nimeleta thread ya hovyo na kuniambia sina fedha za kupanda ndege, kweli ilikuwa ni kejeli lakini sasa tunalia, kama tungeichukulia kwa taadhari yale niliyosema mwanzo hali hii isingetokea. Watanzania! poleni sana majeruhi.
 
Back
Top Bottom