TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Jan 8, 2015
128
90
Wakuu,

Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

=====
UPDATES:

JamiiForums imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed na amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Asema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Rev.Mtikila amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.


Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

Mtikila.jpg
Gari lililopata ajali likiwa limembeba Mchungaji Mtikila.

BAADA ya kutokea kifo cha Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila maeneo ya Msolwa, Chalinze, mkoa wa Pwani, kuliibuka hisia nyingi kutokana na chanzo cha kifo hicho, ifuatayo ni taarofa ya jeshi la Polisi mkoa wa Pwani:-


TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA

Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni "B" Dar Salaam.


Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.

Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.

Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.

Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.

Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.

Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:


  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.

Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.
Mtikila ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba 2014, aliwahi kuandaa waraka wa kutaka nyongeza ya posho za wabunge hao na kutaka mchakato wa katiba mpya usitishwe kwa madai kuwa umeingiliwa na viongozi.

Alitaka serikali ikubali kutoa posho kwa wajumbe ya Sh. 500,000 kwa siku kwa madai kuwa ndicho kiwango walicholipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba kwa siku ya usafiri na nyuma, hivyo siyo sawa wabunge kulipwa kidogo kuliko Tume.


Mahakama ya Kadhi

Wakati Serikali ilipojiandaa kuwasilisha muswada wa Mahakama ya Kadhi katika mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mch. Mtikila akiw akama mwenyekiti wa (DP), alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, akipinga hatua hiyo.


Maisha yake yalikuwa ni ya harakati muda wote

Mchungaji Mtikila alizaliwa mwaka 1950 mkoani Njombe, Kusini mwa Tanzania, ambapo pamoja na shughuli za siasa, pia alikuwa mwanzilishi na Mkuu wa Kanisa la Kipentekoste la Full Salvation.

Kwa muda mwingi wa maisha yake amekuwa anajihusisha na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho "Liberty Desk". Kanisa lake ni moja ya makanisa machache hapa Tanzania yenye vitengo vya namna hiyo.

Soma zaidi -Mchungaji Mtikila afariki kwa ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani


Mada mbalimbali zinazomhusu Mchungaji Mtikila


Mijadala mingine:

Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa wangu...
Man of the moment: Reverend Christopher Mtikila
Mchungaji Mtikila kufungua kesi mahakamani kudai Tanganyika Huru
Mchungaji Mtikila asema CHADEMA wanahusika na kifo cha Chacha Wangwe; kumfikisha Lowassa mahakamani
Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100!
Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi!. Watanzania Sasa Tugomee...!

Mtikila: Dr. Slaa na Prof. Lipumba ni wazalendo, Lowassa hatoshi Urais
Mtikila kumshitaki Lowassa Mahakamani, adai Afya haimruhusu kuwa Rais wa JMT
Mtikila kumshitaki Lowassa kwa kukwepa kodi
Mch. Mtikila kuzuia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 Mahakamani, 2015
Mtikila azuia Muswada wa Mahakama ya Kadhi Kujadiliwa
Waraka wa Mchungaji Mtikila kwa Edward Lowassa
Mahojiano ya Mchungaji Mtikila (Kiingereza)
Rev. Mtikila Confirms Hosting FDLR Commanders in Dar es Salaam
Mchungaji Mtikila: CCM ni Manyani - Epidomea
Mchungaji Mtikila anusurika kuuawa
Mtikila: Kagame amepenyeza Wanyarwanda 35,000 Tanzania
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya Africa
Mtikila aibua mapya tume ya katiba
Mtikila amfungulia Mch. Getrude Rwakare kesi 69/2011 high court
Mchungaji Mtikila kwenda Mahakamani kupinga mchakato wa Katiba Mpya!
Mtikila: Slaa alishinda kwa 71%
Mchungaji Mtikila atoa Kali
Mtikila atishia kumshtaki AG
Hukumu ya mgombea binafsi hii hapa (AG vs Mtikila)
Serikali yaamriwa kuanzisha mchakato wa mgombea binafsi, ni baada ya Mtikila kushida kesi
Mtikila atangaza kugombea Urais kama mgombea binafsi
Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki
Mtikila: Nitaenda mahakama ya kimataifa kwa ajili ya kufungua kesi kuhusu Rasimu ya Katiba


 
Last edited by a moderator:
Kama ndivyo.. Mungu ametenda kazi yake poleni sana Watanganyika..
 
Back
Top Bottom