Murji huru kwa dhamana

Murji huru kwa dhamana

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
6,359
Reaction score
2,389
MURJI HURU KWA DHAMANA: Mbunge wa Mtwara aliyeshtakiwa kwa uchochezi, Hasnain Murji (CCM), ameachiwa kwa dhamana leo mchana. Kesi yake itasomwa tena Julai 4.
 
Ubabe na vitisho vya serikali juu ya suala la gesi havitosaidia kamwe.
 
Hapo ni vunga tu ya maccm ili ionekane kwa wananchi kuwa mmbunge wao anawatetea ili ccm isikataliwe moja kwa moja na wananchi.
 
MURJI HURU KWA DHAMANA: Mbunge wa Mtwara aliyeshtakiwa kwa uchochezi, Hasnain Murji (CCM), ameachiwa kwa dhamana leo mchana. Kesi yake itasomwa tena Julai 4.

Ndiyo mapembe hayo, hata kama ni mbunge wao watayafyeka tu.
 
Ahamie tu kwa waliberali wenzake. Ushauri tu.
 
Pole Mbunge!ila hilo ni fundisho msiingilie mikataba ya maeneo yenu inayosainiwa dar es salaam mahotelini!nyie inatakiwa muwe mnawapokea tuu wawekezaji,msihoji chochote juu ya uwekezaji.na kwenye maslahi ya wananchi yatakiwa usimame upande wa serikali sio bunge kama mhimili wa kuisimamia serikali
 
Isijekuwa aliomba kukamatwa ili kulinda nyumba zake dhidi ya petroli...
 
Hili suala linam "cost" huyu muheshimiwa kwasababu alishusha posho ya study tour ya kutembelea nchi zinazozalisha gesi,kisha akaigeuka wizara ya madini na nishati. Hii ilizungumzwa na waziri husika wakati mgogoro wa gesi unaanza!
 
Hapo ni vunga tu ya maccm ili ionekane kwa wananchi kuwa mmbunge wao anawatetea ili ccm isikataliwe moja kwa moja na wananchi.

Uko sawa GT hili watu wengi hawajalijua,alafu nashangaa hii kuwa breaking news
 
MURJI HURU KWA DHAMANA: Mbunge wa Mtwara aliyeshtakiwa kwa uchochezi, Hasnain Murji (CCM), ameachiwa kwa dhamana leo mchana. Kesi yake itasomwa tena Julai 4.
Hii ni baada ya Katibu wake kulalamika? Nimesoma kwenye magazeti leo.
 
Dhamana anapewa alokamatwa juzi wakati wale wa tlp,cuf na nccr bado wameswekwa rumande, usawa uko wapi?
 
Katani, ahmadi katani, nae kesho anapandishwa kizimban. Labda anaeza pata dhamana. Mungu amsaidie.
 
Back
Top Bottom