neba
Senior Member
- Nov 19, 2008
- 173
- 139
Nawasalimu wana JamiiForums.
Jana nilikuwa nyumbani, nikapata wasaa wa kukumbuka nyimbo zetu (sisi wahenga), nikasikiliza wimbo wa Ndalla Kasheba, Dunia msongamano.
Wimbo huo niliusikia tokea ulivyotolewa, lakini jana ulinipa mtazamo tofauti. Kuna kipande cha wimbo huo kinasema "Naelekea uzeeni sasa, lazima niwe na utulivu. Sababu kuishi kwingi ni kuona mengi, kuelimisha wanaobaki, waishi kwa heshima".
Nilijiunga rasmi na JamiiForums mwaka 2008. Kabla ya hapo nilikuwa naingia na kutoka. Tangu mwaka huo nimekuwa na posti chache mno.( Mimi mhenga, sipendi matusi na kejeli). Ila kwa siku naweza kuingia zaidi ya mara nne.
Nimesoma posti za mabigwa wengi mno, na zipo ambazo zilikuwa nzuri mno. Za kufundisha na kuelimisha. Baadhi ya memba waliokuwa wakiposti sasa, siwaoni katika majukwaa mbalimbali humu.
Wapo ambao wapo sasa, wanaposti mada fikirishi. Kaka Mshana jr najaribu kuelewa mada zako, japo ni ngumu mno na pia yupo Habibu Hanga (Bold) kwa kweli akiandika naelewa mno.
Kuna wanaoposti ili wapate likes. Lakini posti zao, ni tatanishi mno. Nakumbuka kuna waliokuwa wanatambiana kupigana. Hayo mambo ya ajabu mno kwa kizazi kipya.
Kuna ambao hueneza uvumi, uongo na uchonganishi na kudharau, mpaka Utaifa wao. Hawa ndio wanaomtesa Maxence Mello na wenzake. JamiiForums inateseka na habari ambazo hazina vyanzo vya kuaminika.
Nimekuta mijadala humu ndani, na nje. Moja iliyowahi kunishangaza sana, ni ile ya ulinzi wa sehemu nyeti, kuwa chini ya wageni. Ina maana kizazi hiki hakijui kuwa nchi yetu ni waalimu (trainers)?
Je hawajui kuwa tunafundisha watu toka nje ya mipaka yetu? Hawajui kuwa tuna waaminifu, watiifu na wa kweli wengi tu?Hawajui pia kwamba kuna watu wenye weledi wa juu mno?
Niliwahi pia kukuta mada nyingine mahali. Kuna kiongozi wa Taifa kubwa, alitembelea Tanzania. Watu walidai kuwa kiongozi huyo analindwa na robot. Kwa kweli nilisikitika mno.
Ukiachia hayo, napenda kuwaomba wana forum, waposti kwa akili. Nawakumbusha wakati sio milele. Kikubwa mno, nawakumbusha tena methali ya kiswahili isemayo, mchuma janga hula na wakwao.
Wakati wa tatizo la kweli, utashangaa, hakuna like wala nini. Watu watajificha.
Nasomaga pia 'research' mbalimbali.Niliona mbili zilizonichekesha mno. Ya kwanza ilisema Watanzania ni watu wasio na furaha kabisa duniani. Nikaona wengi wamesapoti hilo. Nikajiuliza, hivi hatutembei hata kwa jirani zetu tu tuone? Nchi ambazo huruhusiwi kuongea kitu kuhusu viongozi? Nchi ambazo kila leo wafungwa wanauawa rumande?
Nikaona tafiti ya pili humu ndani. Tanzania ni ya 14 kwa uchawi duniani. Nikashangaa mno. Nikasema labda hii tumependekeza wenyewe. Najua mpaka sasa kuna idadi kubwa ya Watanzania, hawatambiki, wala hawarogi. Humtegemea Mungu tu.
Umezaliwa Tanzania, u Mtanzania, hata ufanyeje, hata uikane nchi yako, historia itabaki hivyo.
Nawatakia Mema yote 2020
Sent using Jamii Forums mobile app