Muongozo wa kuangalia tv online kupitia torrent (android na windows)

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,717
39,806
kuna thread za mobdro, uktvnow, kodi, na njia mbali mbali za kuangalia tv online lakini zote hizi zina kitu kimoja zinalingana, zote hutegemea server kukupa wewe data hivyo server inavyokuwa na speed ndogo huku watu wengi wakiwa wanaangalia basi tv inaanza kunata nata na kunakuwa hakuna ladha tena ya kuangalia.

leo tutaangalia namna ya kuangalia tv kwa kutumia torrent, njia hii haitumii server kama hizo hapo juu bali hutumia peer to peer connection kwa lugha rahisi tunaweza kusema nipe nikupe. njia hii inakuwa mwenzako anakupa data unaangalia na wewe unamtumia mwengine naye anaangalia hivyo internet yenu wenyewe ndio hutumika.

njia hii inakula sana data na inahitaji internet yenye speed lakini vile vile kama una internet yenye speed na bundle nzuri ujue utaangalia tv kama vile unatumia dish quality nzuri na hainati.

mahitaji
kwenye wenye pc zenye windows na simu za android nenda link hii kudownload acestream, player ya torrent
Ace Stream
au kwa android unaweza kwenda playstore ipo.

ukishadownload utahitaji links za tv za torrent ambazo huwa mfumo huu
acestream://8109c41fb27e724521668f76557a6081042898c8

links
kupata links za acestream search online kwa wale wa mpira utapata link kwenye site hii
Soccer Streams • /r/soccerstreams

muda wa mechi ndio zinaonekana

jinsi ya kupaste link watu wa windows
utafungua aceplayer yako halafu juu kushoto click media halafu chagua open network stream halafu paste link yako uplay

kwa watu wa android
watu wa android unaweza usifuate kitu chochote nilichoandika juu kuna app nzuri yenye chanell zaidi ya 600 ya torrent fuata njia hizi kuipata

1. nenda website hii halafu bonyeza alama ya download kuna app utaidownload.
Torrent Stream Controller
kama hujaelewa angalia hii picha
wulVw4o.png

hio button ya kibuluu iliozungushiwa nyekundu ndio alama ya download

2. install application ukifungua itataka idownload aceplayer (mb kama 50 hivi) iruhusu idownload

3. hakikisha una player nzuri ya video, narecomend zaidi mx player

4. fungua tena app yako utakuta chanell za kutosha play unayotaka halafu chagua mxplayer utaona inaplay.

5. kama una bundle na speed ya mawazo usichague chanell za HD.

hizi ni baadhi ya proof za picha chanell za cartoon, movie na michezo

zeWSHgn.jpg

KifCPnc.png

IoQmrBh.jpg


kwa wale wenye pc na wanaitaka hii app tumia emulator, ipo emulator ya droid4x ni nzuri sana nyepesi na ni bure.

droid4x simulator-best mobile experience on desktop
 
Chief samahani naomba unieleweshe Mimi ambae natumia window phone nitaanzia wapi na Kama link itakuwa vizuri zaidi,sie watu WA window tupo na hii streamtube ambayo huwa inazingua sana

Sent from mTalk
 
Kwenye hii app ninaona kuna sehemu imeandikwa hd na kuna channels sasa nitajuaje channels ambazo sio hd
 
Thanx chief lakini naona kama mimi nimejaribu kwenye laptop inasumbua, maelekezo tafadhali
kama unataka kutumia hio app kwenye laptop utahitaji emulator.

bila app utahitaji url, mfano now kuna mechi ya psg ukiingia hio link ya reddit utaiona, kuna url hii ya acestream

acestream://416005a60f4f62ff5a0b5643f825d938698999d3

copy and paste kwenye aceplayer yako
tBfQLUD.png
 
kama unataka kutumia hio app kwenye laptop utahitaji emulator.

bila app utahitaji url, mfano now kuna mechi ya psg ukiingia hio link ya reddit utaiona, kuna url hii ya acestream

acestream://416005a60f4f62ff5a0b5643f825d938698999d3

copy and paste kwenye aceplayer yako
tBfQLUD.png
Mkuu, nmeisntall bt inaniambie video cant play, kibaya zaidi inaleta acc, ya kuchagua kuplay kwenye photo player,

Huenda may b sim yangu ya w4 tekno ni ndogo, bt ina vision ya 6.0

Naomba ushauri kama kunakitu cjakiweka vzr
 
Back
Top Bottom